Mekanika kaniwekea Diesel Engine Oil kwenye gari langu la Engine ya Petrol. Je kuna madhara!?

Mekanika kaniwekea Diesel Engine Oil kwenye gari langu la Engine ya Petrol. Je kuna madhara!?

Mafundi chin ya miembe angalia kwenye engine kuna kibati kina detail had aina ya recommended oil to use for your car ... never put other oil for longevity of your engine.. huyo jamaa aliyoweka itapiga kaz but safari ya kuharibu lifetime ya engine ndo umeaza ... diesel engnie and petrol engine n vitu tofaut sana
 
Asante kunipa moyo mkuu, nawaza hasara ila ungenidadavulia kama uliwahi kutumia gari la petrol kwa engine oil ya diesel nipate moyo zaidi nitumie hata kwa kilometa 1500 tu nimwage
Itakua ni Kampuni ya Toyota. Case kama hiyo kwa Nissan au Subaru au gari za Ulaya, muda huu ungekua unazungumza uite Breakdown
 
Wataalam, natanguliza shukrani.

Leo ilikua muda wa kufanya service gari yangu ( SUV) ambalo ni gari la engine ya Petrol, sasa nikafika garage na hapo hapo wanauza oil, mekanika nikamwambia na kwa uzoefu wake anajua magari madogo kama hilo langu ni gari la petrol hivyo nikamwacha afanye yake na akaenda kuchukua oil mimi nikalipia akafanya service kubadili kusafisha kila kitu muhimu kwa service ya gari.

Sasa nilipofika nyumbani lile dumu la oil nilonunua ie kubadilisha kabla sijalitupa kulitoa kwa gari nikasema baada ya kujisikia tu nilisome kidogo... niliposoma

Nikashangaa limeandikwa
Diesel Engine Oil
na kampuni ni
TotalEnergies
Rubia S
SAE 40
API CF/SF

Nikashangaa kwa nini hakuniwekea Petrol Engine Oil!?
Nikampigia simu akasema eti hiyo oil haina shida yeyote wala haiwezi kuharibu engine ya gari yangu ni kawaida wao kuitumia kwa magari ya petrol mimi sio wa kwanza.

Kwa kweli, sijamuelewa maana sijawahi kuweka kitu tofauti na matumizi yake hii ni mara ya kwanza,
Nimetembea na gari hilo kutoka garage mpaka home ni kilometa 6 tu nimepaki sina amani kulitumia mpaka nisikie maoni ya ninyi wadau.

Je ni kweli kuwa hakuna tatizo nitapata kwa gari yangu baada ya kuweka hii diesel engine oil kwa gari la engine ya petrol!?

Nisaidieni
Madhara ya kutumia diesel engine oil kwenye injini ya petrol:

1. Over-detergent effect (kusafisha kupita kiasi): Inaweza kusafisha sana hadi kuondoa protective coatings ndani ya injini.

2. Viscosity tofauti: Diesel oils mara nyingi ni nzito zaidi (high viscosity) – hii inaweza kufanya mafuta yasisambae vizuri kwenye injini ya petrol, hasa ikiwa ni gari ndogo au engine ndogo.

3. Kupunguza ufanisi wa engine: Injini inaweza kufanya kazi kwa ugumu zaidi, kuongeza moshi, au kupunguza nguvu.

4. Catalytic converter damage: Additives nyingi zinaweza kuharibu catalytic converter, sehemu muhimu kwenye gari za petrol.

5. Check engine light kuwaka: Mfumo wa ECU unaweza kugundua tofauti ya lubrication na kutoa tahadhari.
 
7B6B8494-9328-4347-899F-FB9566ACB7C8.jpeg
 
Kwa hiyo unanishauri nisiitumie hata kwa kilometa kadhaa ndo nibadili oil!? Au ni kwa kipindi gari madhara hayo yatatokea!?
Maana kaniambia kama sina amani next service date ikifika ndo niweke oil niitakayo ya petrol...nisimwage leo leo
MWITE FUNDI AJE AMWAGE HIYO OIL HAPO HOME NA ASAHIHSHE MAKOSA
 
Wataalam, natanguliza shukrani.

Leo ilikua muda wa kufanya service gari yangu ( SUV) ambalo ni gari la engine ya Petrol, sasa nikafika garage na hapo hapo wanauza oil, mekanika nikamwambia na kwa uzoefu wake anajua magari madogo kama hilo langu ni gari la petrol hivyo nikamwacha afanye yake na akaenda kuchukua oil mimi nikalipia akafanya service kubadili kusafisha kila kitu muhimu kwa service ya gari.

Sasa nilipofika nyumbani lile dumu la oil nilonunua ie kubadilisha kabla sijalitupa kulitoa kwa gari nikasema baada ya kujisikia tu nilisome kidogo... niliposoma

Nikashangaa limeandikwa
Diesel Engine Oil
na kampuni ni
TotalEnergies
Rubia S
SAE 40
API CF/SF

Nikashangaa kwa nini hakuniwekea Petrol Engine Oil!?
Nikampigia simu akasema eti hiyo oil haina shida yeyote wala haiwezi kuharibu engine ya gari yangu ni kawaida wao kuitumia kwa magari ya petrol mimi sio wa kwanza.

Kwa kweli, sijamuelewa maana sijawahi kuweka kitu tofauti na matumizi yake hii ni mara ya kwanza,
Nimetembea na gari hilo kutoka garage mpaka home ni kilometa 6 tu nimepaki sina amani kulitumia mpaka nisikie maoni ya ninyi wadau.

Je ni kweli kuwa hakuna tatizo nitapata kwa gari yangu baada ya kuweka hii diesel engine oil kwa gari la engine ya petrol!?

Nisaidieni
Hakuna tatizo mimi nilikuwa na Noah toka nimeinunua nilikuwa natumia oil ya diseal wala hakuna tatizo lililotokeza
 
Kwa hiyo unanishauri nisiitumie hata kwa kilometa kadhaa ndo nibadili oil!? Au ni kwa kipindi gari madhara hayo yatatokea!?
Maana kaniambia kama sina amani next service date ikifika ndo niweke oil niitakayo ya petrol...nisimwage leo leo


Kesho mwite aje kwako na engine cliner then amwage hiyo oil akuwekee 5W-30 ya petrol

Ushauri tu usiendeshe hiyo gari, aje abadilishe hapo home kwako
 
umeshawahi kusikia usemi 'asiyesikia la mkuu huvunjika guu' au 'asiyefunzwa na mama yake hufunzwa na ulimwengu'?
Nimegoogle nakuta mawazo mkanganyiko mzee, nawaza hizi hasara tunatiana siku kwa siku sio poa, nimejikaza kupata hii pesa ya service leo ni hasara tupu kuja kurudia kitu kwa makosa ya mtu mwingine...
Mtandaoni naona kuna watu wanasema wao wanatumiaga diesel engine oil kwenye magari yao ya petrol bila shida yeyote
 
Back
Top Bottom