Mekanika kaniwekea Diesel Engine Oil kwenye gari langu la Engine ya Petrol. Je kuna madhara!?

Mekanika kaniwekea Diesel Engine Oil kwenye gari langu la Engine ya Petrol. Je kuna madhara!?

Mfalme_wa_Nyika👇👇👇

Huyu hapa CHATGPT. Soma kwa uangalifu!

Swali zuri sana! Kuweka mafuta ya injini ya dizeli kwenye injini ya petroli kunaweza kusababisha matatizo kadhaa, hasa kwa muda mrefu. Ingawa yote ni "engine oil," zimetengenezwa kwa mahitaji tofauti ya injini za dizeli na petroli. Hapa chini ni baadhi ya hasara zinazoweza kutokea:
--
🔧 1. Mafuta yana additives tofauti

Mafuta ya dizeli huwa na additives (viambato) zaidi kwa ajili ya kusafisha chembechembe nyingi za kaboni zinazozalishwa na dizeli.

Hii inaweza kusababisha kusafisha kupita kiasi kwenye injini ya petroli, na hivyo kusababisha kutokana au kuvunjika kwa sehemu nyeti za injini.
---
🌡️ 2. Tofauti ya viscosity (unene wa mafuta)

Mafuta ya dizeli mara nyingi huwa mazito zaidi (higher viscosity).

Hii inaweza kufanya mafuta yasisambae vizuri kwenye injini ya petroli, hasa wakati wa baridi, na hivyo kusababisha uchakavu wa haraka wa sehemu kama vile pistoni na camshaft.
---
⚠️ 3. Uwezekano wa kuziba filter au passages

Additives nyingi za mafuta ya dizeli zinaweza kusababisha mabaki (sludge) ambayo huziba njia za mafuta kwenye injini ya petroli.

Hii huzuia lubrication, na kuharibu injini.
---
🔩 4. Gharama ya matengenezo huongezeka

Ikiwa hili litatokea mara kwa mara, unaweza kuona injini ina kelele isiyo ya kawaida, joto kupanda, au hata kuungua gasket.

Hii inapelekea matengenezo ya mara kwa mara au hata uhitaji wa overhaul ya injini.
---

✅ Je, kuna wakati inaweza kutumika?

Katika hali ya dharura kabisa na kwa muda mfupi sana, huenda isilete madhara makubwa mara moja. Lakini si salama kwa matumizi ya kawaida.
---

➡️➡️➡️ 🔁 Nini cha kufanya ukigundua umetumia oil isiyo sahihi:

1. Badilisha mafuta mara moja – drain completely.

2. Weka oil filter mpya.

3. Ikiwezekana, osha injini (engine flush) kabla ya kuweka oil sahihi.

4. Tumia oil inayopendekezwa kwenye manual ya gari lako (kwa mfano: 5W-30, 10W-40 nk).

---
Ukiniambia jina la gari lako na mwaka wake, naweza kusaidia kukushauri oil sahihi.

Unataka nifanye hivyo?
 
Watanzania jaribuni kujifunza vitu hata kama sio fani yako mambo ya brake pad,size ya tairi,service kit ya gari lako ni vitu vya lazima kuvijua kesi zingine ukisoma humu unabaki kushangaa tu..
Fundi anaweka diesel oil kwenye gari inayohitaji petrol oil kwa sababu zipi hata kama akisema hakuna shida unauliza hiyo oil ya petrol car haipatikani kama haipatikani nenda ukafate mwenyewe kwenye duka la oil waambie gari lako wao wakupe oil sahihi ndio unampelekea fundi hizi kesi zenu zinasikitisha sana aisee hao mafundi wanawaroga nini au mwambie fundi mwingine aje kumwaga hiyo oil na ikiwezekana ununue zaidi ingine lita moja baada ya kuwamga hii unaisafisha kwa kuweka ya petrol unamwaga harafu unaweka ambayo hautamwaga.
 
Hii ni kesi ya manufacturer na Fundi killer majaji wataamua ushindi apewe nani.
Na ww usikubali kuwa shahidi wa fundikila ,wala usikubali kutembea kwa maelekezo ya walioelekezwa na Fundikila,kuna siku mtajikuta gereza moja.
Tafuta mwendesha mashtaka asiyependelea,sisi mawakili tupo hapa kukupa mwelekeo wa ushindi wa kesi yako,
Endelea kusoma comments.
 
Wataalam, natanguliza shukrani.

Leo ilikua muda wa kufanya service gari yangu ( SUV) ambalo ni gari la engine ya Petrol, sasa nikafika garage na hapo hapo wanauza oil, mekanika nikamwambia na kwa uzoefu wake anajua magari madogo kama hilo langu ni gari la petrol hivyo nikamwacha afanye yake na akaenda kuchukua oil mimi nikalipia akafanya service kubadili kusafisha kila kitu muhimu kwa service ya gari.

Sasa nilipofika nyumbani lile dumu la oil nilonunua ie kubadilisha kabla sijalitupa kulitoa kwa gari nikasema baada ya kujisikia tu nilisome kidogo... niliposoma

Nikashangaa limeandikwa
Diesel Engine Oil
na kampuni ni
TotalEnergies
Rubia S
SAE 40
API CF/SF

Nikashangaa kwa nini hakuniwekea Petrol Engine Oil!?
Nikampigia simu akasema eti hiyo oil haina shida yeyote wala haiwezi kuharibu engine ya gari yangu ni kawaida wao kuitumia kwa magari ya petrol mimi sio wa kwanza.

Kwa kweli, sijamuelewa maana sijawahi kuweka kitu tofauti na matumizi yake hii ni mara ya kwanza,
Nimetembea na gari hilo kutoka garage mpaka home ni kilometa 6 tu nimepaki sina amani kulitumia mpaka nisikie maoni ya ninyi wadau.

Je ni kweli kuwa hakuna tatizo nitapata kwa gari yangu baada ya kuweka hii diesel engine oil kwa gari la engine ya petrol!?

Nisaidieni
Kama ni Yale magari ya kizamani hayana tatizo, ila haya ya kisiasa yenye senor lazima itasumbua tu. Tumeshachanganya sana na mwendo ni mdundo mbele kwa mbele.
Huko vijijini hakuna hizo choices na maisha yanaendelea. Kuna watu hata service hawafanyi wapo busy kujazilia iliyopungua.
 
Hiyo siyo oil ya diesel engine pekee inatumika pia kwa petrol engine.Hapo kuna hizo herufi CF/SF hiyo "C" inamaanisha 'Compression ignition"-ambayo ni diesel engine na "S" inamaanisha "Spark ignition" ambayo ni petrol engine kwa hiyo ondoa wasi huyo Makanika ni mmbobevu.
 
Back
Top Bottom