Mkuu kwanza thanks for sharing with us hi kitu; miongoni mwa maada ambazo waumini wengi hua wanapata sana TABU basi ni story ya huyu mtu uliyemsema hapa, but kwa kusoma kwangu Biblia, huyu Melkizedeki ni mtu tu kama walivyo pata kua watu wengine, au niweke hivi, Melkizedeki alikua mtumishi wa Mungu kama walivyo pata kutokea wengine na hata waliopo( Yesu anabakia kua ndio kila kitu katika Imani ya Kikristo and may be na zingine ( huko kwingine sina interest nako cause sijasoma sana vitabu vyao) Kwenye huo mstari uliutaja, hebu rudi nyuma mstari 2, utaona imeanza hivi kwa kufungia mabano, "huyo Melkizedeki ( tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Salem, maana yake mfalme wa Amani; ...inaendelea kama ulivyo copy hapo then akafungia mabano. KWahiyo huyu mtu sio kwamba hakuana na baba wala mama na wala hakua mfalme wa milele bali, tafsiri ya jina lake ndio hiyo. Kwa mfano, jina Emmanuel (jina la kwanza kabisa la ahadi la Yesu ) tafsiri yake ni Mungu pamoja na nasi; Kwa hiyo mtu yeyote aitwaye Immanuel hata leo either ana amini katika Mungu au la, hiyo ndio tafsiri ya jina hilo, hivi unajaua jina Yusufu au Joseph kwa kingereza maana yake ni nini? Ni kwamba mtoa jina ana maana hivi, "God you may give me another son" Haijalishi wazazi wanao toa jina hilo Yusufu/Joseph kwa watoto wao kama na wao wanaomba Mungu afanye hivyo au laa but hio ndio maana yake. So huyu Melkizedeki na yeye jina lake ndio lina tafsiri hiyo but yeye hakua kuahani wa milele na ndio maana hapo hapo ulipotoa maandiko, inasema ni mfano wa….., kitu mfano wa… means sio halisi ila kimebeba kitu kingine.
Again, thanks for sharing na huo ndio mchango wangu
Waebrania 7
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
² ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
³ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Tuanzie hapo, ni lini Yesu alipoanza kuitwa
Mwana wa Mungu? Rekodi za mapema kabisa kwenye Biblia ni Mathayo 4:3 ambapo shetani anamjaribu Yesu kusema ukiwa ni Mwana wa Mungu..... Hii ni kusema kwamba kwa kuwa zama za Agano la Kale Kristo alikuwa hajazaliwa, hakutambulika kama Mwana wa Mungu, haikuwa imefunuliwa hivyo. Kufananishwa na Mwana wa Mungu ni kusema Melkisedeki alisimama kama kivuli cha Mwana wa Mungu, a shadow of things to come. Hii bado haithibitishi kuwa ndiye Melkizedeki, tuendelee.
Katika andiko hili ziko sifa ambazo ni za Mungu pekee amepewa Melkizedeki kama ifuatavyo:
1. Hana wazazi - maana yake hakuzaliwa
2. Hana mwanzo wala mwisho wa uhai wake
3. Adumu milele - yaani hafi
Kama kweli Melkizedeki alikuwa na sifa zote hizi basi atakuwa
binadamu wa kwanza kuwa sawa na Mungu. Ukitazama kwa mtazamo huru utagundua kuwa hakuna namna Melkizedeki ni mwanadamu.
⁴ Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.
Hapa ndipo kwa mara ya kwanza tunakutana na
fungu la kumi kwenye Biblia. Fungu la kumi ni agizo lililokuja kutolewa na Mungu baadaye kwa wana wa Israeli, kama sehemu ya sheria yake. Fungu la kumi hutolewa na mwanadamu kwa Mungu ambaye Yeye aliwapa walawi fungu hilo kwa sheria Yake. Sasa Melkizedeki alikuwapo kabla ya sheria kwa sababu mpango wa ukombozi ulianza akiwapo. Pia tumeambiwa tutazame ni jinsi gani mtu huyu alivyo mkuu, kwa sababu alifanya tendo linalopaswa kufanywa na Mungu pekee, kupokea fungu la kumi na kumbariki mwanadamu!!
⁵ Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.
Kama nilivyoeleza hapo juu, fungu la kumi hutolewa kwa Mungu pekee na si wanadamu. Hii ni tangu kuwekwa misingi ya dunia, ndio maana walawi walipokea fungu la kumi kwa agizo la sheria, Mungu ndiye aliyeamuru wapewe. Elewa vema hapo anaposema
"ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahim" kwa lugha nyingine ni kusema ijapokuwa wao ni binadamu tu kama ilivyo kwa Ibrahimu.
⁶ Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.
Bali Melkizedeki ambaye si mlawi, aliyekuwapo kabla ya Lawi, wala hakuupata ukuhani kwa sheria kama ilivyokuwa kwa walawi, ambaye ni kuhani milele, hana mwanzo wala mwisho, alitwaa fungu la kumi toka kwa Ibrahimu, si kwa namna ya sheria kwa sababu yeye ni kuhani hata kabla sheria haijakuwapo.
…
⁸ Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai.
⁹ Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi;
¹⁰ kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.
Huyo ashuhudiwaye kwamba yu hai akipokea fungu la kumi ni Melkizedeki kwa mujibu wa sura hii. Ni huyo ambaye hapo juu anatajwa kuwa hana baba wala mama, mwanzo wala mwisho. Tena ni huyo huyo ambaye anasemwa kupokea fungu la kumi la Lawi (mwanadamu aliyepewa mamlaka kupokea fungu la kumi) kupitia alichotoa Ibrahimu kwa Melkizedeki.
¹¹ Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?
Ukamilifu - yaani upatanisho kamili kati ya Mungu na wanadamu. Kama ungalikuwapo kwa kupitia walawi waliopewa ukuhani kwa sheria - maana yake kwa lugha nyepesi - mwanadamu alipewa sheria ya upatanisho kupitia walawi pekee. Enzi za Melkizedeki hakukuwa na tendo la upatanisho kupitia kuhani, hivyo tujiulize tena, Melkizedeki alikuwa kuhani akimpatanisha nani? Hapa Biblia iko wazi, ukuhani waliopewa wanadamu ni wa walawi pekee, nao haukuweza kuwapa ukamilifu, ndipo ikalazimu uje ukuhani mwingine mbali na huo wa walawi, ukuhani usio kwa jinsi ya sheria. Labda nigusie tena hoja aliyoiandika
Mzee Mwanakijiji kuhusu tafsiri halisi ya neno
kwa mfano.
☆☆☆☆☆
Heb 7:11 - If therefore perfection were by the Levitical priesthood, (for under it the people received the law,) what further need was there that another priest should rise after the order of Melchisedec, and not be called after the order of Aaron?
τάξις, τάξεως, ἡ (τάσσω) - order of
Outline of Biblical Usage
an arranging, arrangement
order
a fixed succession observing a fixed time
due or right order, orderly condition
☆☆☆☆☆
After the order of... imetafsiriwa kama kwa mfano wa, lakini maana halisi ni kwa mpangilio wa..., ama kwa utaratibu wa.. . Kwa hiyo hapa kuna taratibu mbili za ukuhani, mpangilio wa Haruni na mpangilio wa Melkizedeki. Ukuhani wa walawi ambao ndani yake kulikuwa na makuhani wakuu toka uzao wa Haruni ulikuwa mpangilio wa ukuhani wa wanadamu. Huu haukutosha kumkamilisha mwanadamu kwa sababu hata hawa makuhani hawakuwa wakamilifu. Ukuhani kwa mpangilio wa Melkizedeki ulikuwa ukuhani wa milele, haukuja kwa njia ya sheria, bali ukuhani huu hauna mwanzo wala mwisho.
¹² Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.
¹³ Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia madhabahu.
¹⁴ Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani.
Kwa hiyo mpangilio wa ukuhani waliopewa wanadamu, ukuhani wa Haruni, ulishindwa kuwapa wanadamu ukamilifu, badala yake Mungu akaufunua ukuhani wa mpangilio wa Melkizedeki kwa kuzaliwa Kristo. Baada ya kufunuliwa ukuhani huu, ule wa Haruni ukafika kikomo, kwa sababu aliyewapa wanadamu huo ukuhani amekuja kuyatekeleza matakwa yake yeye mwenyewe. Sheria iliwatambua makuhani wa kabila ya Lawi, lakini ukuhani wa Melkizedeki haukuwa na kabila, wala ukoo, wenyewe ulikuwepo, upo na utakuwapo. Aliyeufunua alipitia kwenye kabila la Yuda, tofauti kabisa na matakwa ya sheria, kwa mpangilio wa Haruni. Musa alinena kwa ukuhani wa walawi pekee kwa sababu ulikuwa ni wa kibinadamu, hakuwa na uwezo wa kuongelea ukuhani wa Melkizedeki ambao si wa binadamu.
¹⁵ Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;
¹⁶ asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;
¹⁷ maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.
Kwa hiyo kuhani huyu tuliyeneye sisi amekuwa kwa mpangilio wa kimungu, mpangilio wa Melkizedeki, kuhani kwa uzima usio kikomo.
¹⁸ Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake;
¹⁹ (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu.
²⁰ Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,
²¹ (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani wa milele😉
²² basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Agano la kwanza lilifanywa bila kiapo, agano la ukuhani wa kibinadamu, ukuhani wa mpangilio wa Haruni. Kwa nini bila kiapo? Kwa sababu ulikuwa ukuhani wa sheria, kwamba ukizaliwa katika ukoo huo, basi wewe ni kuhani tayari, hakuna haja ya kuapa popote, ni sheria imesema hivyo. Lakini mpangilio wa Melkizedeki ulikuwa kwa kiapo, kwamba hatatokea tena kuhani mwingine nje ya huyu, anayetekeleza ukuhani wa mpangilio wa Melkizedeki, kuhani uliokuwapo tangu milele, ukafunuliwa kwa kuzaliwa kwake kati ya wanadamu ili kuuondoa ule wa wanadamu na kuutambulisha huu uliokuwapo tangu enzi, kisha unadumu hata milele, Amina.
²³ Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;
²⁴ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
²⁵ Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
Kuhani tuliyenaye kwa mpangilio wa Melkizedeki akaa milele, hafi wala hana ukomo. Walawi walikuwa wengi kwenye ukuhani kwa sababu waliweza kufa kama wanadamu wengine, iliwapasa wawepo wengine wengi kuweza kutimiliza majukumu ya ukuhani. Kwa sababu Melkizedeki akaa milele, hakuna haja ya kuwa na kuhani mwingine tena (Kristu mwingine) kana kwamba iko siku huyu atatoweka. Huyu yu hai tangu enzi na enzi na siku zote amekuwa kuhani. Hatuna makuhani wawili, wala hawajawahi kutokea makuhani wawili kwa mpangilio wa Melkizedeki, vinginevyo Mungu ni mwongo.
²⁶ Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
²⁷ ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.
Melkizedeki aishiye milele alishuka kuja kutukomboa toka utumwa wa dhambi mara moja tu, naye aishi milele damu yake ikifanya upatanisho hata sasa.
²⁸ Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.
Neno la kiapo lilikuja na Kristo ambaye amekuwa kuhani kabla ya Ibrahimu na hata baada. Huyu ndiye asiye na mwanzo wala mwisho, ambaye alishuka kukutana na Ibrahimu ili kusudi achukue sehemu ya kumi, kama toleo kwa ajili ya walawi, ili waje kutekeleza majukumu ya ukuhani kati ya wanadamu, mpaka hapo utimilifu wa nyakati utakapowadia. Na huo utimilifu ulipowadia, alizaliwa na mwanamke, akatwaa namna ya mwanadamu, kusudi ayatekeleze yote yaliyoipasa torati, akauhitimisha ukuhani wa wanadamu kwa kifo chake msalabani, akautambulisha rasmi ukuhani wa milele, ukuhani aliokuwa nao tangu enzi, ukuhani alioshuka nao kuchukua fungu la kumi kwa Ibrahimu kuuanda uzao wake kumshikia zamu yake mpaka ajapo, kisha kuyatimiza hayo akapaa mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu.
Kristu sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu akiwa kama kuhani mkuu, akitupatanisha na Baba. Atakapo rudi mara ya pili atakuja kama mfalme, kufanya hukumu ulimwenguni kote. AMINA.[/I]