Melchizedek na utata unaomzunguka

Melchizedek na utata unaomzunguka

1. Melkizedeki alikuwa kuhani wa Mungu alie juu wala sio kuhani mkuu sawa
2.Ndio Melkizedeki alikuwa juu ya Ibrahim ndio maana akambariki , hili ni jambo la kawaida mkuu ni suala la Mungu tu kumbariki kiumbe wake na kumpa karama nyingi kuliko mwengine

3.Yesu alikuwepo kabla ya msingi wa ulimwengu , hii sikatai lakini njia pekee ya Yesu kujionyesha kwa watu hapa duniani na kuishi nao , ni kuja kuzaliwa na mwanamke , lakini Melkizedeki hii njia ajaipitia kabisa na duniani aliishi na watu bila tabu , vilevile maandiko yanasema huyu Melkizedeki alifananishwa na Mwana wa Mungu lakini Yesu alikuwa mwana wa Mungu kamili , vilevile Melkizedeki alikuwa ni mfalme na kuhani , wakati Yesu alikuwa na vyeo 3(mfalme, kuhani na nabii), ni kweli walifanana lakini sio mtu mmoja
Kwa hiyo njia pekee ya Yesu kujionyesha kwa wanadamu ni kuzaliwa? Kwa ushahidi upi?
 
Missile of the Nation, nitakusaidia tu hapa kidogo. Unafanya kosa moja kubwa. Ni kuwa unadhania waraka wa Waebrania uliandikwa kwa Kiswahili. Niseme tu kuwa ukisoma huo mstari kwa mfano kwenye Kiingereza hausemi You are a priest forever "like" Melkizedech. Kiingereza inasema "You are a priest forever in the order of Melkizedek". Hili neno "in the order of" ndio limepotea kwenye Kiswahili. Lakini hata kwenye Kiingereza utaona limebadilika kidogo nalo hadi uelewa maana ya "order". Kupata mwanga kidogo hapa inabidi usome Waeb 11:7 ambapo hizi "orders" mbili zinalinganishwa. Kuna "order" ya Aaron na order ya Malkizedeki. Sasa makuhani wa Haruni wao wanapata ukuhani wao kwa kurithi kutoka watoto wa kiume wa Haruni tu. Nisikuchoshe; maana yake kwa ufupi ni kuwa order ya Melkizedeki inashikiliwa na Melkizedeki tu na Yesu mwenyewe. Ndio ukuhani pekee wa kifalme (royal priesthood).

Agano Jipya lugha yake ya Asili ni Kigiriki na wala siyo kiingereza kwa hiyo hapa unafanya kosa unalodhani nimefanya.

Biblia ya Kiswahili (agano Jipya) ilitafsiriwa direct kutoka kwenye Kigiriki na siyo Kiingereza.

Hiyo ni point ya kwanza

Lakini lets us use your argument, kwamba badala ya kutumia neno "Kama", tuuangalie huo msitari kwa mantiki ya maneno "In the order of Melkizedek", bado inaprove kuwa hawa ni watu wawili tofauti, mathalani kwa upande wa wana Israel Makuhani wote waliofuata baada ya AARON wanahudumu in "the order of Aaron", inamaanisha wanadumisha huduma ileile iliyokusudiwa na Aaron haimaanishi kuwa wao ndiyo Aaron re-incarnate

Kwa hiyo hata Yesu naye ni Kuhani katika order ya Melkizedeki maana yake ni kwamba kama Jinsi Melkizedeki alivyokuwa Kuhani mtumishi wa Mungu aliyejuu sana ndivyo hivyohivyo jinsi Yesu alivyo Kuhani mtumishi wa Mungu aliyejuu sana.

Tukija kwenye Ishu ya umama, ishu ya Yesu kuwa na mama tangu kuzaliwa,
Ishu ya MAMA ni ishu ya hapa DUNIANI, Ukiondoa Adamu na Eva hakuna aliyewahi kuwa MTU/BINADAMU hapa duniani bila Kuzaliwa na Mwanamke.
Hakuna Ushahidi kuwa Huko Mbinguni viumbe walioko huko huzaliwa na Mwanamke/Mama
Kwa hiyo kujaribu kusisitiza kuwa existence ya Yesu kabla ya kuja duniani ilikuwa bila mama haina maana yoyote kwenye muktadha wa majadiliano yetu maana Ishu ya mama significance yake ni hapa duniani siyo huko Mbinguni

Kuhusu baadhi ya viumbe kuonekana katika umbo la mtu bila kuzaliwa na mwanamke hapa duniani, Malaika wao huonekana kama kuvaa miili ya Watu wakati mwingine lakini Siyo BINADAMU maana hawakuzaliwa na Uzao wa Adamu yaani ( WATU)
 
Hakuna mahali kwenye bible Yesu anatambulishwa kwa sifa ya uungu, hii ni theolojia ya kuunga unga tu kama hii ya kujaribu kumfananisha Yesu na Melkizedeki, lakini theolojia hiyo imebase kwenye logical inferences tu badala ya maandiko!, yaani imebase kwenye watu kuconnect dots badala ya kauli thabiti ya Yesu mwenyewe

Mathayo 24:36 Yesu mwenyewe kwa kauli yake anasema anasema, "hakuna ajuaye saa wala muda wa siku ile SI MALAIKA WALA MWANA AJUAYE ILA BABA PEKE YAKE (3“But concerning that day and hour no one knows, not even the angels of heaven, nor the Son,[a] but the Father only. ")
hili andiko peke yake linakuonyesha kuwa Yesu yuko limited in knowledge, hajui mambo yote na siri zote za ulimwengu huu, na hiyo peke yake ni ushahidi kuwa siyo Mungu
Mkuu Bado unahitaji kuendelea kujifunza Neno la Mungu, wala sishangai vile inaposhindwa kuelewa utofauti wa Mungu, Yesu na Kristo.

"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika." Yohana 1:1- 3.

Mission ya Yesu alipokuja duniani haikuwa kuja kujitangaza kuwa yeye ni Mungu, bali kutangaza wokovu hata kufa kwa ajili ya mwanadamu, ndio maana hutakuta sehemu hata moja alitamka kujiita Mungu, bali alijiweka nafasi ya mwanadamu. Mtu anayehangaika kutafuta mahali Yesu alijiita Mungu ni wazi kuwa bado haelewi Biblia, haelewi mpango wa wokovu.

Yesu angejiita Mungu na kujaribu kujiweka nafasi ya ki-Ungu na heshima yake, hivi unadhani mpango wa wokovu ungekamilika?, unadhani ni mwanadamu gani angesubutu kumkamata?, nani angemshambulia Mungu?.

Ilikuww ni lazima ajiweke mbali na cheo cha Uungu, ili wawepo watu watakaomdharau na kumdhihaki na hata kumsulubisha.

Soma Neno la Mungu, Upate Maarifa.
 
Unachanganya mambo unaposema kuwa KRISTO NDIYE MUNGU
Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu

Yesu alimwabudu Mungu na wala Mungu hakumwabudu Yesu [" Akaenda kwenye bustani ya Gethsemane kuomba, Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, siyo kama mimi nitakavyo bali wewe Utakavyo.."]

Yesu hajui muda wala Saa ya Siku ya Mwisho, Bali Mungu anajua[ Yesu alisema " Hakuna aijuaye saa wa la siku ile si malaika wala mwana bali BABA peke yake"]

Yesu alichosikia kwa Mungu ndicho alichofundisha na wala mafundisho yake hayakuwa kwa utashi wake [Yesu alisema "Nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo na hukumu yangu ni ya haki...."]

Wote wanaomkubali Yesu, ni Mungu ndiye aliyemjaalia wampokee na wamkubali wala si kwa uwezo wake binafsi watu hao kupokea mafundisho yake [Yesu alisema "Baba ulionipa sikumpoteza hata mmoja"]

Yesu anatambua kuwa BABA ndiye Mungu wa pekee [Yesu alisema "Na uzima wa Milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa KWELI na wa PEKEE na Yesu Kristo uliyemtuma"]

Yesu anakiri BABA ni mkuu kuliko yeye [Yesu alisema "BABA yangu ni Mkuu kuliko Mimi"]

Mungu wa Yesu ndiye Mungu wetu, Na Mungu huyo Yesu alipenda kumuita BABA (Yesu alisema "Ninakwenda kwa Baba Yangu naye ni Baba Yenu, MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU")

Utukufu wa Yesu ni BABA ndiye aliyempa wala Yesu hakujipa Mwenyewe [Yesu alisema "Baba Ningependa hawa ulionipa wawe nami nitakapokuwa, wauone utukufu wangu, Utukufu ULIONIPA kabla ya kuumbwa kwa dunia"]

Sasa wewe unaleta habari za Yesu kuwa Mungu wakati maandiko all the time yanakuonyesha kuwa kuna ALIYE JUU YA YESU KIMAMLAKA!

Au unataka kutwambia BABA ni Mungu Mkubwa mkubwa na YESU ni Mungu Mdogomdogo?

Kwa mujibu wa maandiko huwezi kumuequate FATHER (JEHOVAH) na SON (JESUS) yaani utakwama, maandiko hususan Kauli za Yesu mwenyewe zitakukatalia.

Tukubali tu kuna Mungu Mmoja ambaye YESU alikuwa akimuita BABA

Na tukubali tu kuwa Yesu alitumwa na Mungu kuwafunza watu wamjue BABA ili wapate Salvation

Na tukubali tu kuwa Yesu naye ana Mungu, na Mungu mwenyewe ndiye yule alikuwa akimuita BABA

Hili tatizo la kuconnect dots ndo limeharibu sana mafundisho halisi ya Kristo: Badala ya kutwaa mafundisho ya Kristo kama alivyofundisha, watu throughout centuries wakaanza kutengeneza nadharia kuwa "ooh, Yesu ndyo Baba lakini hakujifunua tu, Wengine wanasema hapana BABA na MWANA ni Separate entities lakini wote ni sawa(CO-EQUAL), Wengine wanasema BABA na MWANA ni Walewale tu ila kila mmoja ana role tofauti

Logic/Falsafa/ Nadharia na kuconnect dots kwa baadhi ya watu kumedilute na kupoteza muelekeo halisi wa Mafunzo aliyofundisha Kristo mwenyewe na kuyapeleka so far out of context!

Kristo mwenyewe anasema MY FATHER IS GREATER THAN I (Baba yangu yu Mkuu kuliko mimi), lakini wanakuja watu centuries later wanasema FATHER na SON ni CO-EQUAL and CO-ETERNAL!. hii CO-EQUAL wameipata wapi? wamejitungia wenyewe tu ili kuconnect dots kwao kuweze kumakes sense kwa mujibu wa akili zao za kupenda falsafa!
 
Mkuu kwanza thanks for sharing with us hi kitu; miongoni mwa maada ambazo waumini wengi hua wanapata sana TABU basi ni story ya huyu mtu uliyemsema hapa, but kwa kusoma kwangu Biblia, huyu Melkizedeki ni mtu tu kama walivyo pata kua watu wengine, au niweke hivi, Melkizedeki alikua mtumishi wa Mungu kama walivyo pata kutokea wengine na hata waliopo( Yesu anabakia kua ndio kila kitu katika Imani ya Kikristo and may be na zingine ( huko kwingine sina interest nako cause sijasoma sana vitabu vyao) Kwenye huo mstari uliutaja, hebu rudi nyuma mstari 2, utaona imeanza hivi kwa kufungia mabano, "huyo Melkizedeki ( tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Salem, maana yake mfalme wa Amani; ...inaendelea kama ulivyo copy hapo then akafungia mabano. KWahiyo huyu mtu sio kwamba hakuana na baba wala mama na wala hakua mfalme wa milele bali, tafsiri ya jina lake ndio hiyo. Kwa mfano, jina Emmanuel (jina la kwanza kabisa la ahadi la Yesu ) tafsiri yake ni Mungu pamoja na nasi; Kwa hiyo mtu yeyote aitwaye Immanuel hata leo either ana amini katika Mungu au la, hiyo ndio tafsiri ya jina hilo, hivi unajaua jina Yusufu au Joseph kwa kingereza maana yake ni nini? Ni kwamba mtoa jina ana maana hivi, "God you may give me another son" Haijalishi wazazi wanao toa jina hilo Yusufu/Joseph kwa watoto wao kama na wao wanaomba Mungu afanye hivyo au laa but hio ndio maana yake. So huyu Melkizedeki na yeye jina lake ndio lina tafsiri hiyo but yeye hakua kuahani wa milele na ndio maana hapo hapo ulipotoa maandiko, inasema ni mfano wa….., kitu mfano wa… means sio halisi ila kimebeba kitu kingine.
Again, thanks for sharing na huo ndio mchango wangu

Waebrania 7
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
² ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;
³ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu
); huyo adumu kuhani milele.

Tuanzie hapo, ni lini Yesu alipoanza kuitwa Mwana wa Mungu? Rekodi za mapema kabisa kwenye Biblia ni Mathayo 4:3 ambapo shetani anamjaribu Yesu kusema ukiwa ni Mwana wa Mungu..... Hii ni kusema kwamba kwa kuwa zama za Agano la Kale Kristo alikuwa hajazaliwa, hakutambulika kama Mwana wa Mungu, haikuwa imefunuliwa hivyo. Kufananishwa na Mwana wa Mungu ni kusema Melkisedeki alisimama kama kivuli cha Mwana wa Mungu, a shadow of things to come. Hii bado haithibitishi kuwa ndiye Melkizedeki, tuendelee.

Katika andiko hili ziko sifa ambazo ni za Mungu pekee amepewa Melkizedeki kama ifuatavyo:

1. Hana wazazi - maana yake hakuzaliwa
2. Hana mwanzo wala mwisho wa uhai wake
3. Adumu milele - yaani hafi

Kama kweli Melkizedeki alikuwa na sifa zote hizi basi atakuwa binadamu wa kwanza kuwa sawa na Mungu. Ukitazama kwa mtazamo huru utagundua kuwa hakuna namna Melkizedeki ni mwanadamu.

⁴ Basi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambaye Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara.

Hapa ndipo kwa mara ya kwanza tunakutana na fungu la kumi kwenye Biblia. Fungu la kumi ni agizo lililokuja kutolewa na Mungu baadaye kwa wana wa Israeli, kama sehemu ya sheria yake. Fungu la kumi hutolewa na mwanadamu kwa Mungu ambaye Yeye aliwapa walawi fungu hilo kwa sheria Yake. Sasa Melkizedeki alikuwapo kabla ya sheria kwa sababu mpango wa ukombozi ulianza akiwapo. Pia tumeambiwa tutazame ni jinsi gani mtu huyu alivyo mkuu, kwa sababu alifanya tendo linalopaswa kufanywa na Mungu pekee, kupokea fungu la kumi na kumbariki mwanadamu!!

⁵ Na katika wana wa Lawi nao, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani, ndugu zao, kwa agizo la sheria, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.

Kama nilivyoeleza hapo juu, fungu la kumi hutolewa kwa Mungu pekee na si wanadamu. Hii ni tangu kuwekwa misingi ya dunia, ndio maana walawi walipokea fungu la kumi kwa agizo la sheria, Mungu ndiye aliyeamuru wapewe. Elewa vema hapo anaposema "ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahim" kwa lugha nyingine ni kusema ijapokuwa wao ni binadamu tu kama ilivyo kwa Ibrahimu.

⁶ Bali yeye, ambaye uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.

Bali Melkizedeki ambaye si mlawi, aliyekuwapo kabla ya Lawi, wala hakuupata ukuhani kwa sheria kama ilivyokuwa kwa walawi, ambaye ni kuhani milele, hana mwanzo wala mwisho, alitwaa fungu la kumi toka kwa Ibrahimu, si kwa namna ya sheria kwa sababu yeye ni kuhani hata kabla sheria haijakuwapo.

⁸ Na hapa wanadamu wapatikanao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huko yeye ashuhudiwaye kwamba yu hai.
⁹ Tena yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hata Lawi apokeaye sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi;
¹⁰ kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.

Huyo ashuhudiwaye kwamba yu hai akipokea fungu la kumi ni Melkizedeki kwa mujibu wa sura hii. Ni huyo ambaye hapo juu anatajwa kuwa hana baba wala mama, mwanzo wala mwisho. Tena ni huyo huyo ambaye anasemwa kupokea fungu la kumi la Lawi (mwanadamu aliyepewa mamlaka kupokea fungu la kumi) kupitia alichotoa Ibrahimu kwa Melkizedeki.

¹¹ Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?

Ukamilifu - yaani upatanisho kamili kati ya Mungu na wanadamu. Kama ungalikuwapo kwa kupitia walawi waliopewa ukuhani kwa sheria - maana yake kwa lugha nyepesi - mwanadamu alipewa sheria ya upatanisho kupitia walawi pekee. Enzi za Melkizedeki hakukuwa na tendo la upatanisho kupitia kuhani, hivyo tujiulize tena, Melkizedeki alikuwa kuhani akimpatanisha nani? Hapa Biblia iko wazi, ukuhani waliopewa wanadamu ni wa walawi pekee, nao haukuweza kuwapa ukamilifu, ndipo ikalazimu uje ukuhani mwingine mbali na huo wa walawi, ukuhani usio kwa jinsi ya sheria. Labda nigusie tena hoja aliyoiandika Mzee Mwanakijiji kuhusu tafsiri halisi ya neno kwa mfano.

☆☆☆☆☆

Heb 7:11 - If therefore perfection were by the Levitical priesthood, (for under it the people received the law,) what further need was there that another priest should rise after the order of Melchisedec, and not be called after the order of Aaron?

τάξις, τάξεως, ἡ (τάσσω) - order of

Outline of Biblical Usage

an arranging, arrangement

order

a fixed succession observing a fixed time

due or right order, orderly condition

☆☆☆☆☆

After the order of... imetafsiriwa kama kwa mfano wa, lakini maana halisi ni kwa mpangilio wa..., ama kwa utaratibu wa.. . Kwa hiyo hapa kuna taratibu mbili za ukuhani, mpangilio wa Haruni na mpangilio wa Melkizedeki. Ukuhani wa walawi ambao ndani yake kulikuwa na makuhani wakuu toka uzao wa Haruni ulikuwa mpangilio wa ukuhani wa wanadamu. Huu haukutosha kumkamilisha mwanadamu kwa sababu hata hawa makuhani hawakuwa wakamilifu. Ukuhani kwa mpangilio wa Melkizedeki ulikuwa ukuhani wa milele, haukuja kwa njia ya sheria, bali ukuhani huu hauna mwanzo wala mwisho.

¹² Maana ukuhani ule ukibadilika, hapana budi sheria nayo ibadilike.
¹³ Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kabila nyingine, ambayo hapana mtu wa kabila hiyo aliyeihudumia madhabahu.
¹⁴ Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lo lote juu yake katika mambo ya ukuhani.

Kwa hiyo mpangilio wa ukuhani waliopewa wanadamu, ukuhani wa Haruni, ulishindwa kuwapa wanadamu ukamilifu, badala yake Mungu akaufunua ukuhani wa mpangilio wa Melkizedeki kwa kuzaliwa Kristo. Baada ya kufunuliwa ukuhani huu, ule wa Haruni ukafika kikomo, kwa sababu aliyewapa wanadamu huo ukuhani amekuja kuyatekeleza matakwa yake yeye mwenyewe. Sheria iliwatambua makuhani wa kabila ya Lawi, lakini ukuhani wa Melkizedeki haukuwa na kabila, wala ukoo, wenyewe ulikuwepo, upo na utakuwapo. Aliyeufunua alipitia kwenye kabila la Yuda, tofauti kabisa na matakwa ya sheria, kwa mpangilio wa Haruni. Musa alinena kwa ukuhani wa walawi pekee kwa sababu ulikuwa ni wa kibinadamu, hakuwa na uwezo wa kuongelea ukuhani wa Melkizedeki ambao si wa binadamu.

¹⁵ Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;
¹⁶ asiyekuwa kuhani kwa sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na ukomo;
¹⁷ maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Kwa hiyo kuhani huyu tuliyeneye sisi amekuwa kwa mpangilio wa kimungu, mpangilio wa Melkizedeki, kuhani kwa uzima usio kikomo.

¹⁸ Maana, kuna kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake;
¹⁹ (kwa maana ile sheria haikukamilisha neno); na pamoja na hayo kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwa hayo twamkaribia Mungu.
²⁰ Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,
²¹ (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani wa milele😉
²² basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.

Agano la kwanza lilifanywa bila kiapo, agano la ukuhani wa kibinadamu, ukuhani wa mpangilio wa Haruni. Kwa nini bila kiapo? Kwa sababu ulikuwa ukuhani wa sheria, kwamba ukizaliwa katika ukoo huo, basi wewe ni kuhani tayari, hakuna haja ya kuapa popote, ni sheria imesema hivyo. Lakini mpangilio wa Melkizedeki ulikuwa kwa kiapo, kwamba hatatokea tena kuhani mwingine nje ya huyu, anayetekeleza ukuhani wa mpangilio wa Melkizedeki, kuhani uliokuwapo tangu milele, ukafunuliwa kwa kuzaliwa kwake kati ya wanadamu ili kuuondoa ule wa wanadamu na kuutambulisha huu uliokuwapo tangu enzi, kisha unadumu hata milele, Amina.

²³ Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na mauti wasikae;
²⁴ bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
²⁵ Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.

Kuhani tuliyenaye kwa mpangilio wa Melkizedeki akaa milele, hafi wala hana ukomo. Walawi walikuwa wengi kwenye ukuhani kwa sababu waliweza kufa kama wanadamu wengine, iliwapasa wawepo wengine wengi kuweza kutimiliza majukumu ya ukuhani. Kwa sababu Melkizedeki akaa milele, hakuna haja ya kuwa na kuhani mwingine tena (Kristu mwingine) kana kwamba iko siku huyu atatoweka. Huyu yu hai tangu enzi na enzi na siku zote amekuwa kuhani. Hatuna makuhani wawili, wala hawajawahi kutokea makuhani wawili kwa mpangilio wa Melkizedeki, vinginevyo Mungu ni mwongo.

²⁶ Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;
²⁷ ambaye hana haja kila siku, mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kisha kwa ajili ya dhambi za hao watu; maana yeye alifanya hivi mara moja, alipojitoa nafsi yake.

Melkizedeki aishiye milele alishuka kuja kutukomboa toka utumwa wa dhambi mara moja tu, naye aishi milele damu yake ikifanya upatanisho hata sasa.

²⁸ Maana torati yawaweka wanadamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali hilo neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hata milele.

Neno la kiapo lilikuja na Kristo ambaye amekuwa kuhani kabla ya Ibrahimu na hata baada. Huyu ndiye asiye na mwanzo wala mwisho, ambaye alishuka kukutana na Ibrahimu ili kusudi achukue sehemu ya kumi, kama toleo kwa ajili ya walawi, ili waje kutekeleza majukumu ya ukuhani kati ya wanadamu, mpaka hapo utimilifu wa nyakati utakapowadia. Na huo utimilifu ulipowadia, alizaliwa na mwanamke, akatwaa namna ya mwanadamu, kusudi ayatekeleze yote yaliyoipasa torati, akauhitimisha ukuhani wa wanadamu kwa kifo chake msalabani, akautambulisha rasmi ukuhani wa milele, ukuhani aliokuwa nao tangu enzi, ukuhani alioshuka nao kuchukua fungu la kumi kwa Ibrahimu kuuanda uzao wake kumshikia zamu yake mpaka ajapo, kisha kuyatimiza hayo akapaa mbinguni na kuketi mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu.

Kristu sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu akiwa kama kuhani mkuu, akitupatanisha na Baba. Atakapo rudi mara ya pili atakuja kama mfalme, kufanya hukumu ulimwenguni kote. AMINA.[/I]
 
Agano la Kale lugha yake ya Asili ni Kigiriki na wala siyo kiingereza kwa hiyo hapa unafanya kosa unalodhani nimefanya.

Biblia ya Kiswahili ilitafsiriwa direct kutoka kwenye Kigiriki na siyo Kiingereza.

Hiyo ni point ya kwanza

Lakini lets us use your argument, kwamba badala ya kutumia neno "Kama", tuuangalie huo msitari kwa mantiki ya maneno "In the order of Melkizedek", bado inaprove kuwa hawa ni watu wawili tofauti, mathalani kwa upande wa wana Israel Makuhani wote waliofuata baada ya AARON wanahudumu in "the order of Aaron", inamaanisha wanadumisha huduma ileile iliyokusudiwa na Aaron haimaanishi kuwa wao ndiyo Aaron re-incarnate

Kwa hiyo hata Yesu naye ni Kuhani katika order ya Melkizedeki maana yake ni kwamba kama Jinsi Melkizedeki alivyokuwa Kuhani mtumishi wa Mungu aliyejuu sana ndivyo hivyohivyo jinsi Yesu alivyo Kuhani mtumishi wa Mungu aliyejuu sana.

Tukija kwenye Ishu ya umama, ishu ya Yesu kuwa na mama tangu kuzaliwa,
Ishu ya MAMA ni ishu ya hapa DUNIANI, Ukiondoa Adamu na Eva hakuna aliyewahi kuwa BINADAMU hapa duniani bila Kuzaliwa na Mwanamke.
Hakuna Ushahidi kuwa Huko Mbinguni viumbe walioko huko huzaliwa na Mwanamke/Mama
Kwa hiyo kujaribu kusisitiza kuwa existence ya Yesu kabla ya kuja duniani ilikuwa bila mama haina maana yoyote kwenye muktadha wa majadiliano yetu maana Ishu ya mama significance yake ni hapa duniani siyo huko Mbinguni

Kuhusu baadhi ya viumbe kuonekana katika umbo la mtu bila kuzaliwa na mwanamke hapa duniani, Malaika wao huonekana kama kuvaa miili ya Watu wakati mwingine lakini Siyo BINADAMU maana hawakuzaliwa na Uzao wa Adamu yaani ( WATU)
Agano la kale lilihifadhiwa kwa kiebrania na sio kigiriki.
 
Katika andiko hili ziko sifa ambazo ni za Mungu pekee amepewa Melkizedeki kama ifuatavyo:

1. Hana wazazi - maana yake hakuzaliwa
2. Hana mwanzo wala mwisho wa uhai wake
3. Adumu milele - yaani hafi
Kwanza nashukuru kwa mjadara mzuri, but hapo 1 hadi 3, rudia tena kusoma kwenye Biblia, pameandikwa hivi tena kwa mabano, tafsiri ya jina hilo ( sio huyo mtu ) ndio hizo namba 1 hadi 3 ulio andika. Kasome tu tena uone hata wewe. Kingine ni hiki, mara baada ya Ibrahimu kuonana na huyu mtu, (kasome tena hiyo Mwanzo 14 ) inaonekana kabisa walikua wanafahamiana na ndio maana pameandikwa Melkizedeki mfalme wa Salem maana yake huyo Melkizedeki alikua kiongozi wa mji wa Salem (mji huo ndio Yerusalem/Jerusalem ya leo). So mtu huyu was know kwa wakazi wa mji huo but pamoja na ufalme wake, alikua pia kuhani ( kiongozi wa kidini) So bado nasisitiza huyu hakua mtu unknow, he was known and famous.
 
Agano la kale lilihifadhiwa kwa kiebrania na sio kigiriki.

Waebrania ni kitabu cha agano la kale au jipya?

Agano jipya originally liliandikwa kwa kigiriki

Yes nilikosea kusema Agano la Kale originally liliandikwa kigiriki, Agano jipya ndo lilikuwa Kigiriki bali agano la Kale lilikuwa Kihebrew

Ngoja nikarekebishe chapisho langu la awali
 
Unachanganya mambo unaposema kuwa KRISTO NDIYE MUNGU
Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu

Yesu alimwabudu Mungu na wala Mungu hakumwabudu Yesu [" Akaenda kwenye bustani ya Gethsemane kuomba, Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, siyo kama mimi nitakavyo bali wewe Utakavyo.."]

Yesu hajui muda wala Saa ya Siku ya Mwisho, Bali Mungu anajua[ Yesu alisema " Hakuna aijuaye saa wa la siku ile si malaika wala mwana bali BABA peke yake"]

Yesu alichosikia kwa Mungu ndicho alichofundisha na wala mafundisho yake hayakuwa kwa utashi wake [Yesu alisema "Nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo na hukumu yangu ni ya haki...."]

Wote wanaomkubali Yesu ni Mungu alimjaalia tu wamkubali na wala si kwa uwezo wake [Yesu alisema "Baba ulionipa sikumpoteza hata mmoja"]

Yesu anatambua kuwa BABA ndiye Mungu wa pekee [Yesu alisema "Na uzima wa Milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa KWELI na wa PEKEE na Yesu Kristo uliyemtuma"]

Yesu anakiri BABA ni mkuu kuliko yeye [Yesu alisema "BABA yangu ni Mkuu kuliko Mimi"]

Utukufu wa Yesu ni BABA ndiye aliyempa wala Yesu hakujipa Mwenyewe [Yesu alisema "Baba Ningependa hawa ulionipa wawe nami nitakapokuwa, wauone utukufu wangu, Utukufu ULIONIPA kabla ya kuumbwa kwa dunia"]

Sasa wewe unaleta habari za Yesu kuwa Mungu wakati maandiko all the time yanakuonyesha kuwa kuna ALIYE JUU YA YESU KIMAMLAKA!

Au unataka kuwambia BABA ni Mungu Mkubwa mkubwa na YESU ni Mungu Mdogomdogo?

Kwa mujibu wa maandiko huwezi kumuequate FATHER (JEHOVAH) na SON (JESUS) yaani utakwama, maandiko hususan Kauli za Yesu mwenyewe zitakukatalia.

Tukubali tu kuna Mungu Moja ambaye YESU alikuwa akimuita BABA
Na tukubali tu kuwa YESU ni aliyetumwa na Mungu kuwafunza watu wamjue BABA ili wapate Salvation

Hili tatizo la kuconnect dots ndo limeharibu sana mafundisho halisi ya Kristo: Badala ya kutwaa mafundisho ya Kristo kama alivyofundisha, watu throughout centuries wakaanza kutengeneza nadharia kuwa "ooh, Yesu ndyo Baba lakini hakujifunua tu, Wengine wanasema hapana BABA na MWANA ni Separate entities lakini wote ni sawa(CO-EQUAL), Wengine wanasema BABA na MWANA ni Walewale tu la kila mmoja ana role tofauti

Logic/Falsafa/ Nadharia na kuconnect dots kwa baadhi ya watu kumedilute na kupoteza muelekeo halisi wa Mafunzo aliyofundisha Kristo mwenyewe na kuyapeleka so far out of context!

Kristo mwenyewe anasema MY FATHER IS GREATER THAN I (Baba yangu yu Mkuu kuliko mimi), lakini wanakuja watu centuries later wanasema FATHER na SON ni CO-EQUAL and CO-ETERNAL!. hii CO-EQUAL wameipata wapi? wamejitungia wenyewe tu ili kuconnect dots kwao kuweze kumakes sense kwa mujibu wa akili zao za kupenda falsafa!
Nimekusoma mwelekeo wako na jinsi gani huna elimu ya Mungu kama unavyojionyesha. Hoja zako si mpya ila ni chakula cha wale wenye kukariri tu, wakati neno liko wazi kabisa. Kwa sasa sina muda wa kuandika kuhusu hili, labda hapo baadaye. Ningependa uniambie unaelewa nini kuhusu Agano la kale na Agano jipya na yanahusianaje. Ukinijibu hilo nitapata sehemu ya kuanzia, la hujajibu nitashindwa kuelewa nianzie wapi mjadala huu. Tena nakushauri ufungue thread inayojitegemea ili tujadili kwa mapana
 
Kwanza nashukuru kwa mjadara mzuri, but hapo 1 hadi 3, rudia tena kusoma kwenye Biblia, pameandikwa hivi tena kwa mabano, tafsiri ya jina hilo ( sio huyo mtu ) ndio hizo namba 1 hadi 3 ulio andika. Kasome tu tena uone hata wewe. Kingine ni hiki, mara baada ya Ibrahimu kuonana na huyu mtu, (kasome tena hiyo Mwanzo 14 ) inaonekana kabisa walikua wanafahamiana na ndio maana pameandikwa Melkizedeki mfalme wa Salem maana yake huyo Melkizedeki alikua kiongozi wa mji wa Salem (mji huo ndio Yerusalem/Jerusalem ya leo). So mtu huyu was know kwa wakazi wa mji huo but pamoja na ufalme wake, alikua pia kuhani ( kiongozi wa kidini) So bado nasisitiza huyu hakua mtu unknow, he was known and famous.
Mkuu, unataka tubishane kwa kutumia mtungo wa sentensi? Si vema hata kidogo, lakini nikuulize, unaelewa maana ya semi colon? Alama ;

Hii hapa kwa kiingereza, kama unajenga fundisho kwa kutumia mabano:

Hebrews 7 (KJV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² To whom also Abraham gave a tenth part of all; first being by interpretation King of righteousness, and after that also King of Salem, which is, King of peace;

³ Without father, without mother, without descent, having neither beginning of days, nor end of life; but made like unto the Son of God; abideth a priest continually.

Mabano yaliwekwa na waliotafsiri kiswahili kusaidia msomaji, lakini halikuwa lengo lao kujenga maana potofu kama hicho unachojaribu kufanya

Au labda utusaidie ni neno lipi lenye kubeba maana zote hizo kati ya melkisedeki na salem. Kumbuka haya ni maneno ya kawaida katika lugha ya kiebrania.
 
Kwanza nashukuru kwa mjadara mzuri, but hapo 1 hadi 3, rudia tena kusoma kwenye Biblia, pameandikwa hivi tena kwa mabano, tafsiri ya jina hilo ( sio huyo mtu ) ndio hizo namba 1 hadi 3 ulio andika. Kasome tu tena uone hata wewe. Kingine ni hiki, mara baada ya Ibrahimu kuonana na huyu mtu, (kasome tena hiyo Mwanzo 14 ) inaonekana kabisa walikua wanafahamiana na ndio maana pameandikwa Melkizedeki mfalme wa Salem maana yake huyo Melkizedeki alikua kiongozi wa mji wa Salem (mji huo ndio Yerusalem/Jerusalem ya leo). So mtu huyu was know kwa wakazi wa mji huo but pamoja na ufalme wake, alikua pia kuhani ( kiongozi wa kidini) So bado nasisitiza huyu hakua mtu unknow, he was known and famous.
Hakuna ushahidi uliopatikana kuuhusisha Yerusalem na Salem, isipokuwa wasomi wanajaribu kukisia kuwa huenda Yerusalemu imetokana na Salem. Ni mawazo tu, uwe makini na michango ya kuungaunga.

Kama huyo Melkisedeki alikuwa maarufu kama unavyodai, je kuna nyaraka nyingine zozote zinazomwongelea? Pia ni kwa nini habari zake zionekane kuwa na utata? Usijaribu kusema uongo kwenye mjadala wa kuelimishana. Hatushindani hapa kutafuta mshindi.

Hoja zako hazina bases kimaandiko zaidi ya kujaribu kuhalalisha mtazamo fulani.

Mwanzo 14

²¹ Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe.
²² Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi,
²³ ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala cho chote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;

Mfalme wa Sodoma aliyepigwa na hao maadui wa Ibrahimu, alipomwona alimwendea na kumwomba ampe mateka naye Abram achukue nyara. Lakini Ibrahim alikataa kwa sababu tayari alikuwa ameweka agano na Mungu kuwa atambariki na kumfanya kuwa mwenye utajiri mkubwa. Ndio sababu alisema isijekuwa atakapo tajirika mfalme wa Sodoma aje kujitapa kuwa ni yeye aliye chanzo cha utajiri huo. Hivyo, uelewe kwamba tayari Ibrahimu alikuwa na mahusiano na Mungu wala habari ya kwamba walijuana sio habari mpya.

Soma mlango unaotangulia kujifunza zaidi.
 
Mkuu, unataka tubishane kwa kuumia mtungo wa sentensi? Si vema hata kidogo, lakini nikuulize, unaelewa maana ya semi colon? Alama ;

Hii hapa kwa kiingereza, kama unajenga fundisho kwa kutumia mabano:

Hebrews 7 (KJV)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
² To whom also Abraham gave a tenth part of all; first being by interpretation King of righteousness, and after that also King of Salem, which is, King of peace;

³ Without father, without mother, without descent, having neither beginning of days, nor end of life; but made like unto the Son of God; abideth a priest continually.

Mabano yaliwekwa na waliotafsiri kiswahili kusaidia msomaji, lakini halikuwa lengo lao kujenga maana potofu kama hicho unachojaribu kufanya

Au labda utusaidie ni neno lipi lenye kubeba maana zote hizo kati ya melkisedeki na salem. Kumbuka haya ni maneno ya kawaida katika lugha ya kiebrania.
Mkuu, nimeisoma hiyo KJV ipo sawa na unavyo sema though bado siajona tofauti na Kiswahili, hebu pafikirie hapo kwenye bold, hi ni kutoka kwenye maandishi yako we mwenyewe
 
Hakuna ushahidi uliopatikana kuuhusisha Yerusalem na Salem, isipokuwa wasomi wanajaribu kukisia kuwa huenda Yerusalemu imetokana na Salem. Ni mawazo tu, uwe makini na michango ya kuungaunga.

Kama huyo Melkisedeki alikuwa maarufu kama unavyodai, je kuna nyaraka nyingine zozote zinazomwongelea? Pia ni kwa nini habari zake zionekane kuwa na utata? Usijaribu kusema uongo kwenye mjadala wa kuelimishana. Hatushondani hapa kutafuta mshindi.
OK, ngoja tusome pamoja sura ya 7 ya Waebrania, tuanze msatari 1 hadi 2, pameandikwa hivi, 1 Kwa maana Melkezedeki huyo, mfalmewa Salem, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokua akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki,bali amefananishwa na mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. unadhani kwanini pamewekewa mabano? Na Biblia ipo wazi kabisa hapo, sijui kinacho changanya ni nini? Imesema tafsiri ya hilo JINA ndio hizo sifa. Ni kama kuna kina Immanuel/Emmanuel wengi tu lakini wana bisha kabisa kwamba hakuna Mungu ingawa tafsiri ya jina lao ni Mungu pamoja na sisi. Bado naendelea kuamini (kwa mujibu wa haya maandiko) huyo mtu/Melkizedeki alikua anajulikana na wakazi wa huo mji wa Salem na hata yeye na Ibrahimu walikua wakifahamiana na alikua anazo kazi 2, moja ni kuhani na mfalme wa huo mji wa Salem kama alivyokua Samuel, Eli, wote hawa walikua ni makuhani na wafalme kwa taifa la Israel likiwa bado jipya jipya sana Enzi hizo kabla ya Yesu lakini baada ya Musa
 
Mkuu, nimeisoma hiyo KJV ipo sawa na unavyo sema though bado siajona tofauti na Kiswahili, hebu pafikirie hapo kwenye bold, hi ni kutoka kwenye maandishi yako we mwenyewe
hermēneuō - interpate

Outline of Biblical Usage

to explain in words, expound

to interpret

to translate what has been spoken or written in a foreign tongue into the vernacular
 
OK, ngoja tusome pamoja sura ya 7 ya Waebrania, tuanze msatari 1 hadi 2, pameandikwa hivi, 1 Kwa maana Melkezedeki huyo, mfalmewa Salem, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokua akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki,bali amefananishwa na mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. unadhani kwanini pamewekewa mabano? Na Biblia ipo wazi kabisa hapo, sijui kinacho changanya ni nini? Imesema tafsiri ya hilo JINA ndio hizo sifa. Ni kama kuna kina Immanuel/Emmanuel wengi tu lakini wana bisha kabisa kwamba hakuna Mungu ingawa tafsiri ya jina lao ni Mungu pamoja na sisi. Bado naendelea kuamini (kwa mujibu wa haya maandiko) huyo mtu/Melkizedeki alikua anajulikana na wakazi wa huo mji wa Salem na hata yeye na Ibrahimu walikua wakifahamiana na alikua anazo kazi 2, moja ni kuhani na mfalme wa huo mji wa Salem kama alivyokua Samuel, Eli, wote hawa walikua ni makuhani na wafalme kwa taifa la Israel likiwa bado jipya jipya sana Enzi hizo kabla ya Yesu lakini baada ya Musa
Ok, iko hivi. Tuanze na hiyo mistari, lakini kabla tupate maana ya semi colon (😉.
Semi colon hutumika kuunganisha sentensi mbili ambazo kila moja inaweza kusimama peke yake na kuwa na maana kamili tofauti na nyingine. Mabano yamewekwa kwenye biblia ya kiswahili wala hayamo kwingine.

Sasa soma hapa:

Waebrania 7
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;(.)

² ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (.)

(tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani;(.)

³ hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu);(.)

huyo adumu kuhani milele.(.)

Sijui umeelewa? Mstari wa 3 haufanyi rejeo kwenye jina, bali ni mwendelezo wa mstari wa 2.

Ukisema ni tafsiri ya jina ni uongo, kwa sababu neno Melkisedeki limo kwenye strong, kamusi ya biblia likiwa na maana moja tu na neno salem pia.
 
Agano Jipya lugha yake ya Asili ni Kigiriki na wala siyo kiingereza kwa hiyo hapa unafanya kosa unalodhani nimefanya.

Biblia ya Kiswahili (agano Jipya) ilitafsiriwa direct kutoka kwenye Kigiriki na siyo Kiingereza.

Hiyo ni point ya kwanza

Hapa tena nikusahihishe; lugha ya asili ya Agano la Kale si Kigiriki. Na sikusema ni Kiingereza. Lugha ya AK ni Kiebrania (Hebrew). Lugha ya Agano Jipya (AJ) ndio Kigiriki/Kiyunani. Nashukuru wengine wameshasema hapo juu nawe umekubali kupotea kidogo hapo. Maelezo ya suala la "order" au "mpangilio" au "utaratibu" unakaribia maana ya asili ya Kiebrania. Kuna ndugu yangu mmoja hapo juu kaeleza vizuri zaidi. Ukuhani wa Order ya Melkizedeki una watu "wawili" tu - mtu mmoja tu.

Yesu Kristu kama Neno la Milele, Alfa na Omega, Mwana wa Pekee wa Baba, ametoka kama binadamu katika historia nzima ya wokovu. Hili huitwa kuonekana kwa Yesu kama mwanadamu kabla ya kuzaliwa (Christ's theophanies). Kwa hiyo kwa Ibrahim alionekana kama Melkizedeki (somo la siku nyingine hili).
Lakini lets us use your argument, kwamba badala ya kutumia neno "Kama", tuuangalie huo msitari kwa mantiki ya maneno "In the order of Melkizedek", bado inaprove kuwa hawa ni watu wawili tofauti, mathalani kwa upande wa wana Israel Makuhani wote waliofuata baada ya AARON wanahudumu in "the order of Aaron", inamaanisha wanadumisha huduma ileile iliyokusudiwa na Aaron haimaanishi kuwa wao ndiyo Aaron re-incarnate

Kwa hiyo hata Yesu naye ni Kuhani katika order ya Melkizedeki maana yake ni kwamba kama Jinsi Melkizedeki alivyokuwa Kuhani mtumishi wa Mungu aliyejuu sana ndivyo hivyohivyo jinsi Yesu alivyo Kuhani mtumishi wa Mungu aliyejuu sana.

Shida yako hapa bado iko kwenye lugha na siyo katika kumwelewa Kristo ni nani. Ukifuata lugha unaweza kuwa sahihi; lakini ukifuata ujuzi wa kumjua Kristo ni nani hasa (siyo tu kusema Yesu) utajua kuwa Yesu ni zaidi ya kuwa binadamu. Kuelewa hii Christology (elimu juu ya Kristu) na jinsi gani Wakristu kwa miaka 2000 wamemuelewa Kristu basi utaelewa kwanini Melkizedek anaweza kuwa ni Kristu bila kutupa matatizo yoyote ya kiimani.
Tukija kwenye Ishu ya umama, ishu ya Yesu kuwa na mama tangu kuzaliwa,
Ishu ya MAMA ni ishu ya hapa DUNIANI, Ukiondoa Adamu na Eva hakuna aliyewahi kuwa BINADAMU hapa duniani bila Kuzaliwa na Mwanamke.
Hakuna Ushahidi kuwa Huko Mbinguni viumbe walioko huko huzaliwa na Mwanamke/Mama
Kwa hiyo kujaribu kusisitiza kuwa existence ya Yesu kabla ya kuja duniani ilikuwa bila mama haina maana yoyote kwenye muktadha wa majadiliano yetu maana Ishu ya mama significance yake ni hapa duniani siyo huko Mbinguni

Hapa tena bado unakutana na tatizo hili hili la lugha na kutoelewa Christology. Ngoja nikuulize swali (linahusiana na uelewa wa hii elimu juu ya Kristu). Kwa nini unafikiri Yesu Kristu anaitwa "Mwana" wa Mungu?

Kuhusu baadhi ya viumbe kuonekana katika umbo la mtu bila kuzaliwa na mwanamke hapa duniani, Malaika wao huonekana kama kuvaa miili ya Watu wakati mwingine lakini Siyo BINADAMU maana hawakuzaliwa na Uzao wa Adamu yaani ( WATU)

Hata hapa bado unakaribiwa na tatizo lile lile. Ni wazi unaamini kuwa Yesu ni binadamu wa kawaida tu kama mimi na wewe. Hana upekee wa aina yoyote. Na kama hivi ndivyo unaamini basi utaona asili au chanzo cha shida iliyopo kuhusu Melkizedek na Yesu.
 
Hapa tena nikusahihishe; lugha ya asili ya Agano la Kale si Kigiriki. Na sikusema ni Kiingereza. Lugha ya AK ni Kiebrania (Hebrew). Lugha ya Agano Jipya (AJ) ndio Kigiriki/Kiyunani. Nashukuru wengine wameshasema hapo juu nawe umekubali kupotea kidogo hapo. Maelezo ya suala la "order" au "mpangilio" au "utaratibu" unakaribia maana ya asili ya Kiebrania. Kuna ndugu yangu mmoja hapo juu kaeleza vizuri zaidi. Ukuhani wa Order ya Melkizedeki una watu "wawili" tu - mtu mmoja tu.

Yesu Kristu kama Neno la Milele, Alfa na Omega, Mwana wa Pekee wa Baba, ametoka kama binadamu katika historia nzima ya wokovu. Hili huitwa kuonekana kwa Yesu kama mwanadamu kabla ya kuzaliwa (Christ's theophanies). Kwa hiyo kwa Ibrahim alionekana kama Melkizedeki (somo la siku nyingine hili).

Shida yako hapa bado iko kwenye lugha na siyo katika kumwelewa Kristo ni nani. Ukifuata lugha unaweza kuwa sahihi; lakini ukifuata ujuzi wa kumjua Kristo ni nani hasa (siyo tu kusema Yesu) utajua kuwa Yesu ni zaidi ya kuwa binadamu. Kuelewa hii Christology (elimu juu ya Kristu) na jinsi gani Wakristu kwa miaka 2000 wamemuelewa Kristu basi utaelewa kwanini Melkizedek anaweza kuwa ni Kristu bila kutupa matatizo yoyote ya kiimani.

Hapa tena bado unakutana na tatizo hili hili la lugha na kutoelewa Christology. Ngoja nikuulize swali (linahusiana na uelewa wa hii elimu juu ya Kristu). Kwa nini unafikiri Yesu Kristu anaitwa "Mwana" wa Mungu?

Hata hapa bado unakaribiwa na tatizo lile lile. Ni wazi unaamini kuwa Yesu ni binadamu wa kawaida tu kama mimi na wewe. Hana upekee wa aina yoyote. Na kama hivi ndivyo unaamini basi utaona asili au chanzo cha shida iliyopo kuhusu Melkizedek na Yesu.

Haitoshi kusema Melkizedeki na Yesu ni mtu yuleyule, hiyo ni dhana tu, na kwenye hii mada nzima tumeonyesha kwa rejea ya maandiko kuwa hawa ni watu wawili tofauti na wale wanaojaribu kuwaequate kuwa ni mtu mmoja yule yule wanafuata falsafa, connecting dots lakini hoja zao hazisimami zikatengamaa.

Yesu tunajua alikuja duniani kupitia Bikira Maria kwa mimba ambayo ni Neno la Mungu bila kupitia njia ya kawaida ya tendo la ndoa, Sasa unaamini Yesu huyu huyu amewahi kuja huko nyakati za Abrahamu miaka ya nyuma kidogo kwa jina lingine la Melkizedeki kupitia mwanamke mwingine lakini safari hii kupitia njia ya kawaida ya tendo la ndoa la mwanamke huyo kuingiliwa na mwanaume?
Maana Melkizedeki japo ukoo wake haukutajwa lakini alikuwa ni mtu aliyezaliwa na mwanamke na mwanaume

maandiko yanaposema Melkizedeki hana baba hana mama, ieleweke in context haimaanishi kwamba hakuzaliwa, hakuna Mtu aliyewahi kuexist duniani bila kuzaliwa na mwanamke except ADAMU na EVA peke yao

Tusibebe imani za wapagani za Wahindu za Masuala ya Incarnation tukayaingiza kwenye Bible, ni makosa kufanya hivyo
 
OK, ngoja tusome pamoja sura ya 7 ya Waebrania, tuanze msatari 1 hadi 2, pameandikwa hivi, 1 Kwa maana Melkezedeki huyo, mfalmewa Salem, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokua akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki,bali amefananishwa na mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele. unadhani kwanini pamewekewa mabano? Na Biblia ipo wazi kabisa hapo, sijui kinacho changanya ni nini? Imesema tafsiri ya hilo JINA ndio hizo sifa. Ni kama kuna kina Immanuel/Emmanuel wengi tu lakini wana bisha kabisa kwamba hakuna Mungu ingawa tafsiri ya jina lao ni Mungu pamoja na sisi. Bado naendelea kuamini (kwa mujibu wa haya maandiko) huyo mtu/Melkizedeki alikua anajulikana na wakazi wa huo mji wa Salem na hata yeye na Ibrahimu walikua wakifahamiana na alikua anazo kazi 2, moja ni kuhani na mfalme wa huo mji wa Salem kama alivyokua Samuel, Eli, wote hawa walikua ni makuhani na wafalme kwa taifa la Israel likiwa bado jipya jipya sana Enzi hizo kabla ya Yesu lakini baada ya Musa

Samweli hakuwahi kuwa mfalme. Zamani za kuhani Samweli taifa la serikali ya wana wa Israeli ilikuwa Theocratic, yaani Mungu mwenyewe alikuwa akitawala kama mfalme. Kumbuka ni wakati wa Samweli waisraeli walilazimisha wawe na mfalme kama mataifa mengine, ndipo akachaguliwa mfalme wa kwanza aitwaye Sauli. Hoja ni hiyo hoyo kwa Eli kuhani.

Kuhani na mfalme ni Yesu Kristo peke yake, tafuta biblia nzima.

Nijibu hili swali, ukuhani kati ya wanadamu ulianza lini? Lengo la ukuhani huo lilikuwa lipi?
 
Kwa hiyo njia pekee ya Yesu kujionyesha kwa wanadamu ni kuzaliwa? Kwa ushahidi upi?
" kujionyesha kwa wanadamu na kuishi nao ". hii ni lazima azaliwe ndivyo utabiri unavyotaka rejea ISAYA , hivyo ni watu wawili tofauti hapa naweka kumbukumbu sawasawa
 
Back
Top Bottom