Melchizedek na utata unaomzunguka

Bible ni tofauti na Quraan. Huwezi tumia maneno ya quraan kulinganisha na Bible. Sijaona sehem kuwa rahabu aliwapoteza wapelelezi wa israel.
 

takbirrrr ..
Pale muislam utapotaka kuonekana unajua vyote Qur-an na Bible.
Yako Qur-an mkuu, bible huelewi na ndio maana points zako ni kakariri kama mlivyozoea kukariri qur-an.
Bible inahitaji uelewa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu, sasa mkuu wewe sijui unaongozwa na nini katika kuielewa Bible wakati hata huyo Roho mtakatifu muhuamini.
 

Huku ndo kuishiwa hoja sasa!, Ukiona mtu anaanza kushambulia mtu badala ya hoja ujue kaishiwa!

Au hujui kuwa katika vyuo vya Theolojia hata Qur'an hufundishwa na mafundisho ya dini nyingine pia?(Ni somo linaloitwa Comparative religion)

Akina Pengo wale wako fiti mafundisho yote usiwaone vile

Na bahati mbaya sasa hujui miye nani!.Ndo uzuri wa JF huo, usije ukakuta wewe ndo ulikuja juzi kuungama!!
 
Kwa kusema hivyo mkuu zitto Unamaanisha Henoko alikufa.
 
Mkuu kuwa flexible kidogo naona unajichanganya mkuu. Inamaana Eliya naye alinyofolewa kwenye nyama mkuu Kuna mengine Mwenyezi Mungu Aliya Fanya kuonesha uwezo wake tu mkuu.
 
Kwa kusema hivyo mkuu zitto Unamaanisha Henoko alikufa.
Hakufa as kufa hapa duniani ila hauwezi muona Mungu kwa mwili wetu huu wa damu na nyama so nachoamini either alibadilishwa au mwili wake ulichomolewa ukawekwa mahali ili Roho yake iingie mbinguni.

Otherwise Biblia itacontradict maana ipo clear kuwa ukimuona Mungu na mwili huu UTAKUFA ila kuanzia Ufunuo 22 huko tutamuona Mungu sababu tutakuwa tumefufuliwa na miili mipya ambayo sio hii ya sasa midhaifu inayozeeka!!

Kama ambavyo Musa aliuacha mwili wake mlimani ukaenda zikwa na Malaika basi naamini pia Henoko alipitia the same kwa muktadha huu.
 
Mkuu kuwa flexible kidogo naona unajichanganya mkuu. Inamaana Eliya naye alinyofolewa kwenye nyama mkuu Kuna mengine Mwenyezi Mungu Aliya Fanya kuonesha uwezo wake tu mkuu.
Basi biblia itakua inajichanganya maana inasema mtu akimuona Mungu atakufa na hata manabii wote kuanzia Ezekiel mpaka Yohana alieandika ufunuo walikuwa wakienda mbinguni waliona kama maono tu na walikuwa "in spirit" sio kimwili hivyo kma tukichukua principle hyo ambayo Musa aliambiwa inamaanisha Elia naye ni inclusive.

Hapa ni kwa mujibu wa Biblia mkuu unless mniambie Biblia ina contradict kuwa sio lazima ufe ukimuona Mungu na mnisaidie na mstari.
 
Kwa kusema hivyo mkuu zitto Unamaanisha Henoko alikufa.
1 Wakorinto 15
50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika

Elia atarithi ufalme wa mbinguni kwa mwili wake wa damu na nyama??? Bible inajikosoa?? Embu tusaidiane
 
Tutakushukuru mkuu
 
Yesu Kristu ni mfalme na kuhani. Musa alotabiri kuwa atainuka nabii kati ya waisraeli kama yeye ambaye atatoka kwa Mungu, sifa aliyokuwa nayo Yesu. Sasa sijui hiki kinahusiana nini na mada iliyopo mezani
Melkizedeki umemuweka sawa na Yesu kwa kuwa alikuwa mfalme na kuhani , mimi nakuongezea sifa nyingine kuwa Yesu alikuwa nabii , kwa sifa hii ya unabii tu Melkizedeki anakuwa sio Yesu maana hakuna mahala popote Melkizedeki aliwai kutajwa kama nabii , maana nimekueleza huyu Melkizedeki alikuwa anafananishwa tu na mwana wa Mungu lakini sio Mwana wa Mungu kama Yesu lakini uelewi , umekazania mtu mmoja
 
Ni sawa, ila fahamu kuwa Yesu amekuja kwa baadhi ya wanadamu wakati wa agano la kale, isipokuwa hakuja kama Masihi, unajua hilo?
Kutokuja kwake kama Masihi akukufanyi wewe utafasiri maandiko kwa hisia zako , lazima maandiko yatafasiriwe kwa uhalisia wake , nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi
 
Kutokuja kwake kama Masihi akukufanyi wewe utafasiri maandiko kwa hisia zako , lazima maandiko yatafasiriwe kwa uhalisia wake , nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi
Hiyo utaipata huko kwenu, huku na maji marefu, hakuhitaji akili nyepesi nyepesi. Nikutakie swala njema
 
Kina korefu kwako, waambie wakukaririshe aya nyingine za kubishania uje. Kwa sasa unajidhalilisha tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…