Melchizedek na utata unaomzunguka

Melchizedek na utata unaomzunguka

JIBU LANGU NI KWAMBA KWENYE MAANDIKO FUATA KWANZA KAULI YA YESU MWENYEWE ILIYO CLEAR KABISA KABISA ISIYO NA MAWAA KABLA YA KUAFUATA KAULI AU OPINION YA MTU YEYOTE HATA KAMA MTU HUYO NI MWANAFUNZI WA YESU AU ANAYEDAI KUTOKEWA NA YESU NJIANI AKIELEKEA DAMASCUS (PAULO)

Ngoja nikuulize, hivi wewe kwa mtizamo wako maneno aliyoyasema Paulo, James, Petro au mtu yeyote yakikinzana na maneno halisi ya Yesu yapi unayapa precedent?. Maneno ya nani yanakuwa Final Finito?

Kwa mfano, ukisoma bible vizuri utaona mara kadhaa James ambaye ni mwanafunzi wa Yesu, aliyeishi na Yesu na ni ndugu wa Yesu akigombana mara kibao na Paulo juu ya mafundisho ya Paulo, James analalamika kuwa Paulo analeta baadhi mafundisho mapya na si yale aliyoyafundisha Yesu mwenyewe hususan mafundisho ya kuendelea kuheshimu Sheria za torati vs kuachana na sheria hizo!

Kwa mfano James anatofautiana na Paulo kwenye suala la nani mwenye kuhesabiwa haki, Paulo anasema kwenye Warumi 4:1-5 kuwa mtu anahesabiwa haki kwa IMANI yake na si Matendo yake, akaenda mbele kutoa mfano wa Abrahamu kuwa alihesabiwa haki mbele ya Mungu kwa Imani yake na si matendo yake japo matendo yake mazuri ni kitu cha kujivunia yeye binafsi.

James akamjibu Paulo kwenye James 2:24 kuwa Imani bila MATENDO imani hiyo Imekufa!, James akaenda mbali kutoa mfano wa kwenye agano la Kale juu ya yule kahaba Rahabu aliyewapoteza wapelelezi waliokuja kupeleleza katika nchi yao kwa kuwadanganya njia, na kwa kitendo cha kufanya hivyo tu huyo kahaba akahesabiwa haki!

Kwa hiyo Unaona hawa ni watu wawili wenye mawazo tofauti juu ya kuhesabiwa haki mbele ya Mungu kwa hiyo point yangu ni kwamba, kwa kuwa hata wao wana mitizamo inayokinzana juu ya mambo ya Mungu Sembuse Mmoja apingane na Kauli ya Wazi ya Yesu Mwenyewe?


Yesu kajiita Mtu, Kasema wazi kuwa na yeye pia ana Mungu anayemwabudu, Kasema BABA yake ni Mungu wake na pia ni Mungu wetu THEN baadae atokee mtu mmoja anayeitwa Paulo au Yeyote yule kisha aseme "Jamani eeeh Hapana, Yesu naye ni Mungu", anatoa kauli opposite kabisa na Yesu mwenyewe, mimi nasema Kauli ya kusikiliza hapo ni KAULI YA YESU MWENYEWE, HAWA WENGINE WAMETOA OPINION YAO TU!, OPINION YAO ITAKUWA NA UZITO IKIFANANA NA MAFUNDISHO YA KRISTO MWENYEWE ,IKIENDA AGAINST NAYE SISI TUNACHUKUA MANENO YA KRISTO NDO YANAKUWA FINAL!
Bible ni tofauti na Quraan. Huwezi tumia maneno ya quraan kulinganisha na Bible. Sijaona sehem kuwa rahabu aliwapoteza wapelelezi wa israel.
 
Unachanganya mambo unaposema kuwa KRISTO NDIYE MUNGU
Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu
Yesu alimwabudu Mungu na wala Mungu hakumwabudu Yesu [" Akaenda kwenye bustani ya Gethsemane kuomba, Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, siyo kama mimi nitakavyo bali wewe Utakavyo.."]
Yesu hajui muda wala Saa ya Siku ya Mwisho, Bali Mungu anajua[ Yesu alisema " Hakuna aijuaye saa wa la siku ile si malaika wala mwana bali BABA peke yake"]
Yesu alichosikia kwa Mungu ndicho alichofundisha na wala mafundisho yake hayakuwa kwa utashi wake [Yesu alisema "Nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo na hukumu yangu ni ya haki...."]
Wote wanaomkubali Yesu, ni Mungu ndiye aliyemjaalia wampokee na wamkubali wala si kwa uwezo wake binafsi watu hao kupokea mafundisho yake [Yesu alisema "Baba ulionipa sikumpoteza hata mmoja"]
Yesu anatambua kuwa BABA ndiye Mungu wa pekee [Yesu alisema "Na uzima wa Milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa KWELI na wa PEKEE na Yesu Kristo uliyemtuma"]
Yesu anakiri BABA ni mkuu kuliko yeye [Yesu alisema "BABA yangu ni Mkuu kuliko Mimi"]
Mungu wa Yesu ndiye Mungu wetu, Na Mungu huyo Yesu alipenda kumuita BABA (Yesu alisema "Ninakwenda kwa Baba Yangu naye ni Baba Yenu, MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU")
Utukufu wa Yesu ni BABA ndiye aliyempa wala Yesu hakujipa Mwenyewe [Yesu alisema "Baba Ningependa hawa ulionipa wawe nami nitakapokuwa, wauone utukufu wangu, Utukufu ULIONIPA kabla ya kuumbwa kwa dunia"]
Sasa wewe unaleta habari za Yesu kuwa Mungu wakati maandiko all the time yanakuonyesha kuwa kuna ALIYE JUU YA YESU KIMAMLAKA!
Au unataka kutwambia BABA ni Mungu Mkubwa mkubwa na YESU ni Mungu Mdogomdogo?
Kwa mujibu wa maandiko huwezi kumuequate FATHER (JEHOVAH) na SON (JESUS) yaani utakwama, maandiko hususan Kauli za Yesu mwenyewe zitakukatalia.
Tukubali tu kuna Mungu Mmoja ambaye YESU alikuwa akimuita BABA
Na tukubali tu kuwa Yesu alitumwa na Mungu kuwafunza watu wamjue BABA ili wapate Salvation
Na tukubali tu kuwa Yesu naye ana Mungu, na Mungu mwenyewe ndiye yule alikuwa akimuita BABA
Hili tatizo la kuconnect dots ndo limeharibu sana mafundisho halisi ya Kristo: Badala ya kutwaa mafundisho ya Kristo kama alivyofundisha, watu throughout centuries wakaanza kutengeneza nadharia kuwa "ooh, Yesu ndyo Baba lakini hakujifunua tu, Wengine wanasema hapana BABA na MWANA ni Separate entities lakini wote ni sawa(CO-EQUAL), Wengine wanasema BABA na MWANA ni Walewale tu ila kila mmoja ana role tofauti
Logic/Falsafa/ Nadharia na kuconnect dots kwa baadhi ya watu kumedilute na kupoteza muelekeo halisi wa Mafunzo aliyofundisha Kristo mwenyewe na kuyapeleka so far out of context!
Kristo mwenyewe anasema MY FATHER IS GREATER THAN I (Baba yangu yu Mkuu kuliko mimi), lakini wanakuja watu centuries later wanasema FATHER na SON ni CO-EQUAL and CO-ETERNAL!. hii CO-EQUAL wameipata wapi? wamejitungia wenyewe tu ili kuconnect dots kwao kuweze kumakes sense kwa mujibu wa akili zao za kupenda falsafa!

takbirrrr ..
Pale muislam utapotaka kuonekana unajua vyote Qur-an na Bible.
Yako Qur-an mkuu, bible huelewi na ndio maana points zako ni kakariri kama mlivyozoea kukariri qur-an.
Bible inahitaji uelewa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu, sasa mkuu wewe sijui unaongozwa na nini katika kuielewa Bible wakati hata huyo Roho mtakatifu muhuamini.
 
takbirrrr ..
Pale muislam utapotaka kuonekana unajua vyote Qur-an na Bible.
Yako Qur-an mkuu, bible huelewi na ndio maana points zako ni kakariri kama mlivyozoea kukariri qur-an.
Bible inahitaji uelewa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu, sasa mkuu wewe sijui unaongozwa na nini katika kuielewa Bible wakati hata huyo Roho mtakatifu muhuamini.

Huku ndo kuishiwa hoja sasa!, Ukiona mtu anaanza kushambulia mtu badala ya hoja ujue kaishiwa!

Au hujui kuwa katika vyuo vya Theolojia hata Qur'an hufundishwa na mafundisho ya dini nyingine pia?(Ni somo linaloitwa Comparative religion)

Akina Pengo wale wako fiti mafundisho yote usiwaone vile

Na bahati mbaya sasa hujui miye nani!.Ndo uzuri wa JF huo, usije ukakuta wewe ndo ulikuja juzi kuungama!!
 
Mkuu ndio maana nikasema exceptions zisitumike kudicredit hoja nzima.....

Henoko aliondolewa ila obvious hakwenda na mwili wa nyama huu mbinguni so at some point Roho yake ilitolewa mwili ukatupwa maana mwanadamu hawezi muona Mungu akaishi na hata Musa aliambiwa hivo na ndio maana hata baada ya resurrection ukisome 2 korinto 15 na Ufunuo 20-22 utaona tutavaa miili mipya ili kuishi milele na kumuona Mungu. Kama ingekuwa kila nafsi inaishi milele kivipi Yesu aahidi TUTAISHI MILELE baada ya UFUFUO Kwenye Yohana 6:40 if at all hata tukifa tunaishi milele hta sasa??

Nachosema ni hiki kwakuwa Bible inasema Wenye dhambi wataenda Motoni je ikitokea kuna mwenye dhambi ukimkuta Mbinguni utasema ndio Biblia imedanganya?? Nachosema kuwa kuna uwezekano wa exceptions mbili tatu mfano Mungu aliahidi kutowaacha wayahudi no matter what lakini wote tunajua Kabila la DANI lilifutwa kwenye list ya makabila ya Israel je ina maana Mungu aliwasaliti alichoahidi??

Margin of Error/ Exceptions/0.00001% na vitu kama hivyo haviwezi kudiscredit hoja ya kuwa wenye dhambi wataenda kuzimu ama binadamu hawezi ishi milele (Yaani before birth and after life)

NB: Hoja zako nzito mkuu I appreciate that
Kwa kusema hivyo mkuu zitto Unamaanisha Henoko alikufa.
 
1. Kuhusu Yesu kuwa na mwili tofauti nmekwambia soma 1 korintho 15 sura nzima inasema damu na nyama haziwezi gusa ufalme wa mbinguni ndio maana Yesu alipofufuka aliweza kutoweka na kutokea mahali pengine n.k tofauti na mwanzoni alipokua na element za kibinadamu kabisa.

2. Kuhusu Melchizedek kuwa Mungu hakuna mahala nimesema hivyo, ila waliotoa hoja wengine wanasema alikuja kwa mfano mwanadamu kma melchizedek, au wale "wageni" walioenda kwa Abraham au Yesu yaani alikuja kwa taswira ya kibinadamu ndio maana hao wakamuona. Ila akiwa katika UTUKUFU wake yatatokea yale ya Radi za Mlima Sinai hadi watu wakasepa!!

3. Yesu alikuja kwa taswira ya binadamu ila naye angeshuka kwa utukufu wa kiMungu asingeweza exist hapa duniani either wangemkimbia au ndio wangekufa!! Hta Leo Mungu anaweza shuka in different forms ili atuguse kwa namna tofauti ila kumuona face to face haiwezekani Exodus 33:12!!
Mkuu kuwa flexible kidogo naona unajichanganya mkuu. Inamaana Eliya naye alinyofolewa kwenye nyama mkuu Kuna mengine Mwenyezi Mungu Aliya Fanya kuonesha uwezo wake tu mkuu.
 
Kwa kusema hivyo mkuu zitto Unamaanisha Henoko alikufa.
Hakufa as kufa hapa duniani ila hauwezi muona Mungu kwa mwili wetu huu wa damu na nyama so nachoamini either alibadilishwa au mwili wake ulichomolewa ukawekwa mahali ili Roho yake iingie mbinguni.

Otherwise Biblia itacontradict maana ipo clear kuwa ukimuona Mungu na mwili huu UTAKUFA ila kuanzia Ufunuo 22 huko tutamuona Mungu sababu tutakuwa tumefufuliwa na miili mipya ambayo sio hii ya sasa midhaifu inayozeeka!!

Kama ambavyo Musa aliuacha mwili wake mlimani ukaenda zikwa na Malaika basi naamini pia Henoko alipitia the same kwa muktadha huu.
 
Mkuu kuwa flexible kidogo naona unajichanganya mkuu. Inamaana Eliya naye alinyofolewa kwenye nyama mkuu Kuna mengine Mwenyezi Mungu Aliya Fanya kuonesha uwezo wake tu mkuu.
Basi biblia itakua inajichanganya maana inasema mtu akimuona Mungu atakufa na hata manabii wote kuanzia Ezekiel mpaka Yohana alieandika ufunuo walikuwa wakienda mbinguni waliona kama maono tu na walikuwa "in spirit" sio kimwili hivyo kma tukichukua principle hyo ambayo Musa aliambiwa inamaanisha Elia naye ni inclusive.

Hapa ni kwa mujibu wa Biblia mkuu unless mniambie Biblia ina contradict kuwa sio lazima ufe ukimuona Mungu na mnisaidie na mstari.
 
Kwa kusema hivyo mkuu zitto Unamaanisha Henoko alikufa.
1 Wakorinto 15
50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika

Elia atarithi ufalme wa mbinguni kwa mwili wake wa damu na nyama??? Bible inajikosoa?? Embu tusaidiane
 
Hii ni mojawapo ya masomo ambayo nimeyapitia kwa undani kidogo. Sijui kama kuna nafasi ya kutosha. Lakini kwa ufupi niseme tu Mwandishi wa Waebrania, wa Zaburi na yule wa Mwanzo wote wanamzungumzia mtu yule yule; Yesu Kristu. Kumbuka Waebrania ina mstari mmoja muhimu sana Waeb. 13.8 ambayo inasema "Yesu Kristu ni yule yule, Jana, na leo, na hata milele". Na kama unakumbuka katika unabii wa Isaya kuhusu kuzaliwa kwa Yesu tunaambiwa kati ya majina yake mengi mojawapo ataitwa "Mfalme wa Amani"... Mfalme wa Amani ni Mfalme wa Salemu (Salemu ni "amani").

Hii ndio sababu Ibrahim alipokutana na Melkizedek alimpa fungu la kumi (kumbuka hii ilikuwa kabla ya zaka kuingizwa katika sheria za wayahudi). Ukitaka kuelewa hili rejea maneno ya Yesu ambayo anawaambia Wayahudi kuwa "Ibrahim baba yenu aliitamani kuiona siku yangu, aliiona na akafurahi (Yoh 8:56). Na utaona kuwa Yesu hamuiti Ibrahimu "baba yetu" bali "baba yenu"... Lakini pia alitoa dai moja sehemu nyingine (mistari miwili tu chini) ambalo nusura wayahudi wampige. Alisema katika mstari mwingine maarufu "Kweli kweli nawaambia" Yesu akasema, "kabla Ibrahim hajazaliwa mimi Niko" (Yoh 8:58).

Basi hapo kwa ufupi tu; ni sehemu ya tafiti yangu moja ndefu sana; labda siku moja ikimpendeza Mungu nitawashirikisha.
Tutakushukuru mkuu
 
Yesu Kristu ni mfalme na kuhani. Musa alotabiri kuwa atainuka nabii kati ya waisraeli kama yeye ambaye atatoka kwa Mungu, sifa aliyokuwa nayo Yesu. Sasa sijui hiki kinahusiana nini na mada iliyopo mezani
Melkizedeki umemuweka sawa na Yesu kwa kuwa alikuwa mfalme na kuhani , mimi nakuongezea sifa nyingine kuwa Yesu alikuwa nabii , kwa sifa hii ya unabii tu Melkizedeki anakuwa sio Yesu maana hakuna mahala popote Melkizedeki aliwai kutajwa kama nabii , maana nimekueleza huyu Melkizedeki alikuwa anafananishwa tu na mwana wa Mungu lakini sio Mwana wa Mungu kama Yesu lakini uelewi , umekazania mtu mmoja
 
Ni sawa, ila fahamu kuwa Yesu amekuja kwa baadhi ya wanadamu wakati wa agano la kale, isipokuwa hakuja kama Masihi, unajua hilo?
Kutokuja kwake kama Masihi akukufanyi wewe utafasiri maandiko kwa hisia zako , lazima maandiko yatafasiriwe kwa uhalisia wake , nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi
 
Melkizedeki umemuweka sawa na Yesu kwa kuwa alikuwa mfalme na kuhani , mimi nakuongezea sifa nyingine kuwa Yesu alikuwa nabii , kwa sifa hii ya unabii tu Melkizedeki anakuwa sio Yesu maana hakuna mahala popote Melkizedeki aliwai kutajwa kama nabii , maana nimekueleza huyu Melkizedeki alikuwa anafananishwa tu na mwana wa Mungu lakini sio Mwana wa Mungu kama Yesu lakini uelewi , umekazania mtu mmoja
Kina korefu kwako, waambie wakukaririshe aya nyingine za kubishania uje. Kwa sasa unajidhalilisha tu
 
Back
Top Bottom