JIBU LANGU NI KWAMBA KWENYE MAANDIKO FUATA KWANZA KAULI YA YESU MWENYEWE ILIYO CLEAR KABISA KABISA ISIYO NA MAWAA KABLA YA KUAFUATA KAULI AU OPINION YA MTU YEYOTE HATA KAMA MTU HUYO NI MWANAFUNZI WA YESU AU ANAYEDAI KUTOKEWA NA YESU NJIANI AKIELEKEA DAMASCUS (PAULO)
Ngoja nikuulize, hivi wewe kwa mtizamo wako maneno aliyoyasema Paulo, James, Petro au mtu yeyote yakikinzana na maneno halisi ya Yesu yapi unayapa precedent?. Maneno ya nani yanakuwa Final Finito?
Kwa mfano, ukisoma bible vizuri utaona mara kadhaa James ambaye ni mwanafunzi wa Yesu, aliyeishi na Yesu na ni ndugu wa Yesu akigombana mara kibao na Paulo juu ya mafundisho ya Paulo, James analalamika kuwa Paulo analeta baadhi mafundisho mapya na si yale aliyoyafundisha Yesu mwenyewe hususan mafundisho ya kuendelea kuheshimu Sheria za torati vs kuachana na sheria hizo!
Kwa mfano James anatofautiana na Paulo kwenye suala la nani mwenye kuhesabiwa haki, Paulo anasema kwenye Warumi 4:1-5 kuwa mtu anahesabiwa haki kwa IMANI yake na si Matendo yake, akaenda mbele kutoa mfano wa Abrahamu kuwa alihesabiwa haki mbele ya Mungu kwa Imani yake na si matendo yake japo matendo yake mazuri ni kitu cha kujivunia yeye binafsi.
James akamjibu Paulo kwenye James 2:24 kuwa Imani bila MATENDO imani hiyo Imekufa!, James akaenda mbali kutoa mfano wa kwenye agano la Kale juu ya yule kahaba Rahabu aliyewapoteza wapelelezi waliokuja kupeleleza katika nchi yao kwa kuwadanganya njia, na kwa kitendo cha kufanya hivyo tu huyo kahaba akahesabiwa haki!
Kwa hiyo Unaona hawa ni watu wawili wenye mawazo tofauti juu ya kuhesabiwa haki mbele ya Mungu kwa hiyo point yangu ni kwamba, kwa kuwa hata wao wana mitizamo inayokinzana juu ya mambo ya Mungu Sembuse Mmoja apingane na Kauli ya Wazi ya Yesu Mwenyewe?
Yesu kajiita Mtu, Kasema wazi kuwa na yeye pia ana Mungu anayemwabudu, Kasema BABA yake ni Mungu wake na pia ni Mungu wetu THEN baadae atokee mtu mmoja anayeitwa Paulo au Yeyote yule kisha aseme "Jamani eeeh Hapana, Yesu naye ni Mungu", anatoa kauli opposite kabisa na Yesu mwenyewe, mimi nasema Kauli ya kusikiliza hapo ni KAULI YA YESU MWENYEWE, HAWA WENGINE WAMETOA OPINION YAO TU!, OPINION YAO ITAKUWA NA UZITO IKIFANANA NA MAFUNDISHO YA KRISTO MWENYEWE ,IKIENDA AGAINST NAYE SISI TUNACHUKUA MANENO YA KRISTO NDO YANAKUWA FINAL!