Melchizedek na utata unaomzunguka

Mkui sio mwizi tu hta ww ukifa utaenda "mahali".... Swali linakuja HUKO UNAFANYA NNI?? Nachojua function zote za duniani unaziacha hapa huko unasubiri hukumu tu whether ur conscious or not sasa kivp Yesu/Melchizedek waendelee na ukuhani ilihali hawapo duniani??? Embu nisaidie hapa

Elia hakufa kimwili ila alizaliwa so ana mwanzo.... Pia hakuna mahala inasema Elia anaendelea kuwa nabii huko mbinguni?? Let alone spirit ya Elia ilirudi wakati wa Yohana mbatizaji ambaye naye alikufa!! Whatever it is ila Elia ana mwanzo na ana Baba na Mama maana ameexist akiwa tumboni mwa ***** ila Yesu na Melchizedek tunaambiwa walikuwepo before tumboni kwa mama zao wa duniani.

So mpaka hapa sioni mwanadamu aliyeishi milele na ambaye anaendelea na function zake za kibinadamu baada ya kifo.

So as it stands ni wawili tu Yesu na Melchizedek as kwa hii hoja
 

Hakuna andiko linalosema kuwa Yesu huko aliko anafanya Ukuhani, kama una andiko la hilo suala lilete mkuu

Yohana aliulizwa kuwa wewe ni Eliya akakataa (Yohana 1:21), kwa hiyo hapa muondoe Eliya kwenye equation maana Eliya siyo Yohana mbatizaji unless otherwise utwambie kuwa Yohana alikuwa muongo

Sasa basi mpaka sasa Eliya yuko huko mbinguni na hatujui kama keshauvua mwili wake au la, Kwa hiyo kama Eliya ni mwanandamu na alipaa na mwili wake, basi maana yake bado ni binadamu kamili unless uje na uthibitisho mwingine wa maandiko.

Eliya akiwa na Musa pia wamewahi kumtokea Yesu, Kuna siku Yesu alisali sana, akatokewa na Musa na Eliya mpaka Petro akataka ajenge vibanda vitatu kimoja cha Musa, kingine cha Yesu na Kingine cha Eliya.

Kwa hiyo bwana Zittojuniour, Kwa mujibu wa biblia watu wanaishi huko waliko na huko waliko wataishi milele hawafi!

NADHANI HOJA YA UMILELE TUMEIMALIZA, LABDA TUJE KWENYE HOJA YA UMWANZO
 
1. Andiko la Yesu kufanya ukuhani milele soma Hyi waebrania 7:17 au Zaburi 112

2. Yohana mbatizaji alikuwa na Roho ya Elia na Yesu alithibitisha hilo Mathayo 17:12

3. Elia hatuambiwi kama anaendelea na Unabii wake mbinguni so naye ni dormant tu mpaka hukumu. Ila melchizedek na Yesu tumeambiwa wazi kuwa wana exist milele kwa function yao ya ukuhani irrespective ya kuondoka duniani. Nipe mstari wa Elia ili mjadala uwe sawia otherwise tusitoe assumption!!

4.milele nimesema Roho kuwepo baada ya kifo sio KUISHI mpaka hukumu ije ndio kuna watakoishi ishi milele kuzimu ama mbinguni not otherwise. Nmekupa hapo hyo 1 peter 2:19 hujanijibu.

5. Ukishakufa unasubiri hukumu according to Ufunuo ila kuishi means unafulfill function zako kama kawaida bila kujali upo Kiroho au kimwili......

So mpaka hapa no one lives forever consistently apart from Jesus (Tuache exceptions za kukisia cjui Elia cjui Mwizi) ila twende generally kuwa 99% ya wanadamu wakifa hawaishi tena mpaka HUKUMU.

Nawasilisha
 
OK asante
 

Unajua Zitto Junior unachokifanya ni "Transliteration" yaani kutwist tafsiri ya mambo kifalsafa, kwa mfano unapotafsiri kuishi maana yake nini ni pure opinion yako haibase kwenye maandiko. Unaposema kuishi maana yake ni kufulfil function zako kama kawaida maana yake nini kwa mfano, kula?, kunywa?, kulala?, kutambua?, kuhisi?, kujua? n.k

Unaposema kuwa 99% ya watu wakifa hawaishi mpaka hukumu, tayari unakuwa unamaanisha kuwa 1% ya watu inaishi hadi hukumu, na wakishahykumiwa wataendelea kuishi ama motoni au peponi milele. Kwa hiyo hoja yako ya UMILELE ina fall flat, yaani inavunjika vunjika kwa maana UMEKIRI kuwa kuna watu baada ya kuzaliwa na kufa kimwili hapa duniani Wangali wakiishi, wewe umewapa 1% ila tofauti yangu na wewe ni kwamba mimi nawapa 100%

Hii hoja ya UMILELE tumeimaliza, wewe mwenyewe umekiri kuwa 1% wanaishi huko waliko now sasa Naurudisha Mjadala kwenye UMWANZO!
 
Mkuu naona hatuelewani maana mie nmetoa mstari huo wa Waebrania 7:17 au Zaburi 112 inayosema hao wawili wanaishi milele kama Makuhani ikimaanisha kabla hawajaja dunia walifunction huko mbinguni na duniani wakapita tu ila walipoondoka wakaendelea na function zao za KIMBINGUNI kama malaika unavyoona n.k

Ila hakuna mwanadamu ambaye anazaliwa then akifa anaondoka na cheo chake, uchungaji cjui ukuhani mwisho duniani tu so that's distinguishing sababu huwezi sema unaishi wakati umelala kwenye kaburi kama bible inavyosema kwenye Ufunuo kuwa wataamka baada ya parapanda kulia na hukumu soma Rev 20.

Hiyo 99% nayoongelea ni ww kujengea hoja kwa mtu mmoja ili udiscredit 99% yote..... Yaani huwezi sema kwa kuwa Elia hakufa basi ndio inaprove wanadamu wanaishi milele wakati nmekuuliza unipe mstari unaosema Elia ni Nabii Milele kma nlivyoweka wa melchizedek/Yesu.

So far ww ndio upo subjective....
Conclusion: Hakuna maisha baada ya kifo mpaka kwanza hukumu Rev 20
Hakuna mwanadamu anaendelea na function zake baada ya kifo.

Karibu great thinker
 
Andiko la bibilia chimbuko lake ni miaka 7000 iliyopita. Imebainika kuwa umri wa dunia ni miaka billion kadhaa iliyopita. Kwa hiyo kuna uwezekano dunia ilikaliwa na wakazi miaka million nyingi iliyopita.
UCHAMBUZI WANGU;
Kuna uwezekano kuwa dunia imekuwa ikifika mwisho na kuanza upya kila baada ya miaka elfu kadhaa na mara zote amekuwa akitokea super human mfano wa Yesu kuwatahadharisha watu habari za mwisho huo, kwa kusema ivi namaanisha kuwa Yesu amekuwa akija duniani kila mara kabla ya dunia kuumbwa upya na tarehe kuanza hesabu upya. Namaanisha nini hapa, ni kwamba Melchizedek, Nuhu na Yesu mwenyewe yawezekana ni mtu mmoja aliyerudi duniani kwa nyakati tofauti ila kwa lengo linalofanana. Mwisho wa dunia ni mwanzo wa dunia! Inaingia akilini hii theory??
 

Wewe Unasema: nanukuu

"Hakuna maisha baada ya kifo mpaka kwanza hukumu Rev 20
Hakuna mwanadamu anaendelea na function zake baada ya kifo".

Lakini mbona hutuelezi kuhusu waliokwenda mbinguni bila kufa hapa duniani, Je huoni kuwa uwepo wao huko tayari hoja yako inafall flat?

Kwa mfano biblia inasema Enoch aliondolewa hapa duniani bila kufa
 
Yesu alikuja akaondoka kama alivyo tabiliwa na manabii walio kuja kabla yake huyo kuhani mkuu sio yesu chamsingi bible kuna vitabu vingi havipo so kuna mambo mengi hatuyajui
 
Mkuu ndio maana nikasema exceptions zisitumike kudicredit hoja nzima.....

Henoko aliondolewa ila obvious hakwenda na mwili wa nyama huu mbinguni so at some point Roho yake ilitolewa mwili ukatupwa maana mwanadamu hawezi muona Mungu akaishi na hata Musa aliambiwa hivo na ndio maana hata baada ya resurrection ukisome 2 korinto 15 na Ufunuo 20-22 utaona tutavaa miili mipya ili kuishi milele na kumuona Mungu. Kama ingekuwa kila nafsi inaishi milele kivipi Yesu aahidi TUTAISHI MILELE baada ya UFUFUO Kwenye Yohana 6:40 if at all hata tukifa tunaishi milele hta sasa??

Nachosema ni hiki kwakuwa Bible inasema Wenye dhambi wataenda Motoni je ikitokea kuna mwenye dhambi ukimkuta Mbinguni utasema ndio Biblia imedanganya?? Nachosema kuwa kuna uwezekano wa exceptions mbili tatu mfano Mungu aliahidi kutowaacha wayahudi no matter what lakini wote tunajua Kabila la DANI lilifutwa kwenye list ya makabila ya Israel je ina maana Mungu aliwasaliti alichoahidi??

Margin of Error/ Exceptions/0.00001% na vitu kama hivyo haviwezi kudiscredit hoja ya kuwa wenye dhambi wataenda kuzimu ama binadamu hawezi ishi milele (Yaani before birth and after life)

NB: Hoja zako nzito mkuu I appreciate that
 

Hahaha Zittojuniour
I rest my case

Ila kabla sijafunga mjadala
Ni vyema Tusilete assumptions zetu wenyewe bila back up ya maandiko
Si vizuri kuwaza kwa mfano Enoko alivyoondoka mwili wake ulivuliwa ikabaki roho au la, maadamu tunajua aliondoka na mwili basi ufahamu wetu unaishia hapohapo, nje ya hapo ni speculations tu.

Au tunajua Yesu aliondoka duniani na mwili wake ule ule, leo ukisema huko mbinguni aliuvua mwili akabaki kwenye state ya roho hiyo pia inabaki ni speculations tu hatuna ushahidi wa kimaandishi kuwa aliuvua mwili na alipouvua ameuweka wapi kwa hilo hatujui.

Niko tayari kuufungua Mjadala wa UMWANZO!
 
Nimejaribu kuainisha hizi aya za Melkizedeki kuhani mkuu ambazo ukizipitia kwa uangalifu wa kihekima unajifunza kitu na kugundua kuwa Melkizedeki kuhani mkuu ndio utangulizi Kristo kama neno la Mungu

Mungu huweka majira yake kwa sababu zake mwenyewe nadhani Melkizedeki ni katika neno la Mungu kutengeneza mapito ya mwanzo.

Kristo Yesu neno la Mungu katika majira ya Nyakati za ukamilisho zama hizi tunazoishi.



Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana.
Mwanzo 14:18

Bwana ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.
Zaburi 110:4

kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani wa milele Kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 5:6

kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 5:10

alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 6:20

Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki;
Waebrania 7:1

kwa maana alikuwa katika viuno vya baba yake, hapo Melkizedeki alipokutana naye.
Waebrania 7:10

Basi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi; (maana watu wale waliipata sheria kwa huo); kulikuwa na haja gani tena ya kuhani mwingine ainuke, kwa mfano wa Melkizedeki, wala asihesabiwe kwa mfano wa Haruni?
Waebrania 7:11

Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine mithili ya Melkizedeki;
Waebrania 7:15

maana ameshuhudiwa kwamba, Wewe u kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.
Waebrania 7:17
 
Mkuu kwa kuhitimisha labda niweke kitu sawa
1. Henoko hawezi kwenda na mwili sababu Bible imesema Kutoka 33:12 kuwa hatuwezi muona Mungu tukaishi. Jibu linatoka Yohana 4:24 Kuwa Mungu ni Roho so anakuwa approached Kiroho tu basi na hii inathibitika Ufunuo 22:4 kuwa tutamuona uso wake ila tukishapata MWILI mpya sio hii ya kibinadamu 2 Kor 15 sura nzima inaelezea miilo mipya. So kwakuwa Henoko hakuelezewa kama alipata mwili mpya hivyo we can conclude kwamba hakuna binadamu anamuona Mungu including Henoko.

Kuhusu Yesu iko wazi kabisa alipata mwili mpya baada ya kufufuka hta hyo sura ya 15 imeeleza kabisa.... Kwamba yye ndio kaset precedence ya watu kufufuka na mwili mpya na ndio maana hata aliporudi kuna watu hawakumtambua akiwemo Mama yake!! Hivyo lile mwili la nyama linalozeeka aliliacha anapojua yeye ila HAKUONDOKA NAO.

Hivyo hapa hamna speculation bali ni kufuata precedence tu ya matukio mengine kuconclude kuhusu life after Death.

UMWANZO!!!
 

Yesu hakupata mwili mpya baada ya "kufufuka" ndiyo maana walipoenda kaburini siku ya tatu walikuta mwili wa Yesu uleule waliouzika haupo kaburini maana yake aliendelea kuwa na mwili ule ule

Na pia kitendo cha kuwaonyesha wanafunzi wake wamguse mwili wake wajionee ilikuwa ni kuwaonyesha yeye ni yesu yuleyule ili wasidhani ni mzimu!. Kama Yesu angekuwa na mwili tofauti na wa zamani basi ingekuwa sababu ya Wanafunzi wake kumuona kuwa siyo yule original

Pili hoja ya Kumuona Mungu,
Kama mnasema kuwa Melkizedeki ni Mungu aliyeshuka duniani akiwa ndani ya mwili wa kibinadamu basi kuna watu walimuona enzi hizo akiwa ni mfalme wa Salem, mtu mmojawapo aliyemuona ni Ibarahim, Kwa hiyo kama kweli Melkizedeki ni Mungu aliyekuwa ameshuka duniani akaonwa na watu basi hataEnoko naye pia huko aliko aweza kumuona!

The other thing, Kama Yesu ndiye Melkizedeki na Yesu pia mwasema ni Mungu, basi wanadamu akina Petro walimuona na hivyo basi hata Enoko huko aliko kama Yesu ni Mungu kweli basi huenda akamuaona kama vie akina Petro, mathayo, Mariamu magdalena walivyomuona hapa duniani, Sasa kwa nini Enoko mwenye mwili asimuone Yesu aliyepaa na mwili wakati wengine wamemuona huyo Yesu na hawakudhurika?
 
Mh
 
Huenda ni tafsiri za wasomaji Biblia katika katika utohoaji wa maana na lengo la maandiko kukinzana kulingana na mtazamo binafsi naamini mbinguni kinachoenda ni Roho

Soma Biblia

23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
Yohana 4:23

24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
Yohana 4:24


23 Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza,
Mathayo 22:23

24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
Mathayo 22:24

25 Basi, kwetu kulikuwa na ndugu saba; wa kwanza akaoa, akafariki, na kwa kuwa hana mzao, akamwachia nduguye mke wake.
Mathayo 22:25

26 Vivyo hivyo wa pili naye, na wa tatu, hata wote saba.
Mathayo 22:26

27 Mwisho wa wote yule mwanamke akafa naye.
Mathayo 22:27

28 Basi, katika kiyama, atakuwa mke wa yupi katika wale saba? Maana wote walikuwa naye.
Mathayo 22:28

29 Yesu akajibu, akawaambia, Mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.
Mathayo 22:29

30 Kwa maana katika kiyama hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika mbinguni.
Mathayo 22:30
 
Mi nafikiri Enock, Melkizedek na Yesu ndiyo roho moja iliyokuja katika nyakati tofauti
 
1. Kuhusu Yesu kuwa na mwili tofauti nmekwambia soma 1 korintho 15 sura nzima inasema damu na nyama haziwezi gusa ufalme wa mbinguni ndio maana Yesu alipofufuka aliweza kutoweka na kutokea mahali pengine n.k tofauti na mwanzoni alipokua na element za kibinadamu kabisa.

2. Kuhusu Melchizedek kuwa Mungu hakuna mahala nimesema hivyo, ila waliotoa hoja wengine wanasema alikuja kwa mfano mwanadamu kma melchizedek, au wale "wageni" walioenda kwa Abraham au Yesu yaani alikuja kwa taswira ya kibinadamu ndio maana hao wakamuona. Ila akiwa katika UTUKUFU wake yatatokea yale ya Radi za Mlima Sinai hadi watu wakasepa!!

3. Yesu alikuja kwa taswira ya binadamu ila naye angeshuka kwa utukufu wa kiMungu asingeweza exist hapa duniani either wangemkimbia au ndio wangekufa!! Hta Leo Mungu anaweza shuka in different forms ili atuguse kwa namna tofauti ila kumuona face to face haiwezekani Exodus 33:12!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…