joefrancy
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 792
- 550
Weka linki mkuu Niki downloadTafuta kitabu cha william marrion branham kinaitwa.
WHO IS MELKIZEDECK
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Weka linki mkuu Niki downloadTafuta kitabu cha william marrion branham kinaitwa.
WHO IS MELKIZEDECK
Mkui sio mwizi tu hta ww ukifa utaenda "mahali".... Swali linakuja HUKO UNAFANYA NNI?? Nachojua function zote za duniani unaziacha hapa huko unasubiri hukumu tu whether ur conscious or not sasa kivp Yesu/Melchizedek waendelee na ukuhani ilihali hawapo duniani??? Embu nisaidie hapaMkuu , huyo mwizi aliyekuwa msalabani pembeni mwa Yesu alipopewa ahadi kuwa angekuwa peponi na Yesu jioni ile humo peponi angekuwemo bila kujitambua?. Maana naye aliuliwa msalabani na alizikwa kama wanavyozikwa wafu wengine.
Pili Elia huko aliko yuko vague?
Maana Elia hajawahi kufa
Mkui sio mwizi tu hta ww ukifa utaenda "mahali".... Swali linakuja HUKO UNAFANYA NNI?? Nachojua function zote za duniani unaziacha hapa huko unasubiri hukumu tu whether ur conscious or not sasa kivp Yesu/Melchizedek waendelee na ukuhani ilihali hawapo duniani??? Embu nisaidie hapa
Elia hakufa kimwili ila alizaliwa so ana mwanzo.... Pia hakuna mahala inasema Elia anaendelea kuwa nabii huko mbinguni?? Let alone spirit ya Elia ilirudi wakati wa Yohana mbatizaji ambaye naye alikufa!! Whatever it is ila Elia ana mwanzo na ana Baba na Mama maana ameexist akiwa tumboni mwa ***** ila Yesu na Melchizedek tunaambiwa walikuwepo before tumboni kwa mama zao wa duniani.
So mpaka hapa sioni mwanadamu aliyeishi milele na ambaye anaendelea na function zake za kibinadamu baada ya kifo.
So as it stands ni wawili tu Yesu na Melchizedek as kwa hii hoja
1. Andiko la Yesu kufanya ukuhani milele soma Hyi waebrania 7:17 au Zaburi 112Hakuna andiko linalosema kuwa Yesu huko aliko anafanya Ukuhani.
Yohana aliulizwa kuwa wewe ni Eliya akakataa (Yohana 1:21), kwa hiyo hapa muondoe Eliya kwenye equation.
Kwa hiyo mpaka sasa Eliya yuko huko mbinguni na hatujui kama keshauvua mwili wake au la, Kwa hiyo kama Eliya ni mwanandamu na alipaa na mwili wake, basi maana yake bado ni binadamu kamili unless uje na uthibitisho mwingine wa maandiko.
Eliya akiwa na Musa pia wamewahi kumtokea Yesu, Kuna siku Yesu alisali sana, akatokewa na Musa na Eliya mpaka Petro akataka ajenge vibanda vitatu kimoja cha Musa, kingine cha Yesu na Kingine cha Eliya.
Kwa hiyo bwana Zittojuniour, Kwa mujibu wa biblia watu wanaishi huko waliko na huko waliko wataishi milele hawafi!
NADHANI HOJA YA UMILELE TUMEIMALIZA, LABDA TUJE KWENYE HOJA YA UMWANZO
Hyo ni painting ya Ethiopia ambayo Kitabu cha Book Of Enoch kipo Kwenye Bible yao ndio kinamuongelea Melchizedek kwa undani kidogo. Na kwa kuwa wao ni weusi hivyo wakatengeneza mfano wa Picha yake kuwa ni mtu mweusi sawa na wazungu tu movie ya Yesu waliweka mzungu mwenye nywele nyeupe (Blonde) ilihali hamna watu wa hivyo mashariki ya kati.
1. Andiko la Yesu kufanya ukuhani milele soma Hyi waebrania 7:17 au Zaburi 112
2. Yohana mbatizaji alikuwa na Roho ya Elia na Yesu alithibitisha hilo Mathayo 17:12
3. Elia hatuambiwi kama anaendelea na Unabii wake mbinguni so naye ni dormant tu mpaka hukumu. Ila melchizedek na Yesu tumeambiwa wazi kuwa wana exist milele kwa function yao ya ukuhani irrespective ya kuondoka duniani. Nipe mstari wa Elia ili mjadala uwe sawia otherwise tusitoe assumption!!
4.milele nimesema Roho kuwepo baada ya kifo sio KUISHI mpaka hukumu ije ndio kuna watakoishi ishi milele kuzimu ama mbinguni not otherwise. Nmekupa hapo hyo 1 peter 2:19 hujanijibu.
5. Ukishakufa unasubiri hukumu according to Ufunuo ila kuishi means unafulfill function zako kama kawaida bila kujali upo Kiroho au kimwili......
So mpaka hapa no one lives forever consistently apart from Jesus (Tuache exceptions za kukisia cjui Elia cjui Mwizi) ila twende generally kuwa 99% ya wanadamu wakifa hawaishi tena mpaka HUKUMU.
Nawasilisha
Mkuu naona hatuelewani maana mie nmetoa mstari huo wa Waebrania 7:17 au Zaburi 112 inayosema hao wawili wanaishi milele kama Makuhani ikimaanisha kabla hawajaja dunia walifunction huko mbinguni na duniani wakapita tu ila walipoondoka wakaendelea na function zao za KIMBINGUNI kama malaika unavyoona n.kUnajua Zitto Junior unachokifanya ni "Transliteration" yaani kutwist tafsiri ya mambo kifalsafa, kwa mfano unapotafsiri kuishi maana yake nini ni pure opinion yako haibase kwenye maandiko. Unaposema kuishi maana yake ni kufulfil function zako kama kawaida maana yake nini kwa mfano, kula?, kunywa?, kulala?, kutambua?, kuhisi?, kujua? n.k
Unaposema kuwa 99% ya watu wakifa hawaishi mpaka hukumu, tayari unakuwa unamaanisha kuwa 1% ya watu inaishi hadi hukumu, na wakishahykumiwa wataendelea kuishi ama motoni au peponi milele. Kwa hiyo hoja yako ya UMILELE ina fall flat, yaani inavunjika vunjika kwa maana UMEKIRI kuwa kuna watu baada ya kuzaliwa na kufa kimwili hapa duniani Wangali wakiishi, wewe umewapa 1% ila tofauti yangu na wewe ni kwamba mimi nawapa 100%
Hii hoja ya UMILELE tumeimaliza, wewe mwenyewe umekiri kuwa 1% wanaishi huko waliko now sasa Naurudisha Mjadala kwenye UMWANZO!
Mkuu naona hatuelewani maana mie nmetoa mstari huo wa Waebrania 7:17 au Zaburi 112 inayosema hao wawili wanaishi milele kama Makuhani ikimaanisha kabla hawajaja dunia walifunction huko mbinguni na duniani wakapita tu ila walipoondoka wakaendelea na function zao za KIMBINGUNI kama malaika unavyoona n.k
Ila hakuna mwanadamu ambaye anazaliwa then akifa anaondoka na cheo chake, uchungaji cjui ukuhani mwisho duniani tu so that's distinguishing sababu huwezi sema unaishi wakati umelala kwenye kaburi kama bible inavyosema kwenye Ufunuo kuwa wataamka baada ya parapanda kulia na hukumu soma Rev 20.
Hiyo 99% nayoongelea ni ww kujengea hoja kwa mtu mmoja ili udiscredit 99% yote..... Yaani huwezi sema kwa kuwa Elia hakufa basi ndio inaprove wanadamu wanaishi milele wakati nmekuuliza unipe mstari unaosema Elia ni Nabii Milele kma nlivyoweka wa melchizedek/Yesu.
So far ww ndio upo subjective....
Conclusion: Hakuna maisha baada ya kifo mpaka kwanza hukumu Rev 20
Hakuna mwanadamu anaendelea na function zake baada ya kifo.
Karibu great thinker
Yesu alikuja akaondoka kama alivyo tabiliwa na manabii walio kuja kabla yake huyo kuhani mkuu sio yesu chamsingi bible kuna vitabu vingi havipo so kuna mambo mengi hatuyajuiMkuu Missile of the Nation huyo melikzedech hapa duniani alipita tu hakukaa,,hata Mungu aliwahi mtokea Ibrahim ila hakukawia kurudi alikotoka,,lakini Yesu aliishi hapa duniani miaka 33.Na kama melikzedech angeishi hapa duniani sharti angeuvaa mwili.Maana dunia haiko compatible na viumbe roho.Kwa nini Yesu ndie melikzedech ni kwa sababu ya ukuhani na uhusiano wa mwili wake na agano jipya ambalo limefungamana na damu yake.
Mkuu ndio maana nikasema exceptions zisitumike kudicredit hoja nzima.....Wewe Unasema: nanukuu
"Hakuna maisha baada ya kifo mpaka kwanza hukumu Rev 20
Hakuna mwanadamu anaendelea na function zake baada ya kifo".
Lakini mbona hutuelezi kuhusu waliokwenda mbinguni bila kufa hapa duniani, Je huoni kuwa uwepo wao huko tayari hoja yako inafall flat?
Kwa mfano biblia inasema Enoch aliondolewa hapa duniani bila kufa
Mkuu ndio maana nikasema exceptions zisitumike kudicredit hoja nzima.....
Henoko aliondolewa ila obvious hakwenda na mwili wa nyama huu mbinguni so at some point Roho yake ilitolewa mwili ukatupwa maana mwanadamu hawezi muona Mungu akaishi na hata Musa aliambiwa hivo na ndio maana hata baada ya resurrection ukisome 2 korinto 15 na Ufunuo 20-22 utaona tutavaa miili mipya ili kuishi milele na kumuona Mungu. Kama ingekuwa kila nafsi inaishi milele kivipi Yesu aahidi TUTAISHI MILELE baada ya UFUFUO Kwenye Yohana 6:40 if at all hata tukifa tunaishi milele hta sasa??
Nachosema ni hiki kwakuwa Bible inasema Wenye dhambi wataenda Motoni je ikitokea kuna mwenye dhambi ukimkuta Mbinguni utasema ndio Biblia imedanganya?? Nachosema kuwa kuna uwezekano wa exceptions mbili tatu mfano Mungu aliahidi kutowaacha wayahudi no matter what lakini wote tunajua Kabila la DANI lilifutwa kwenye list ya makabila ya Israel je ina maana Mungu aliwasaliti alichoahidi??
Margin of Error/ Exceptions/0.00001% na vitu kama hivyo haviwezi kudiscredit hoja ya kuwa wenye dhambi wataenda kuzimu ama binadamu hawezi ishi milele (Yaani before birth and after life)
NB: Hoja zako nzito mkuu I appreciate that
Nimejaribu kuainisha hizi aya za Melkizedeki kuhani mkuu ambazo ukizipitia kwa uangalifu wa kihekima unajifunza kitu na kugundua kuwa Melkizedeki kuhani mkuu ndio utangulizi Kristo kama neno la MunguHabari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.
Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni
UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.
Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH
View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.
Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki
Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??
Je huyu melchizedek ni nani hasa?
UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???
Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!
Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.
Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.
HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.
Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??
Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??
Je historia yake ni ipi??
Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?
Karibuni....
Mkuu kwa kuhitimisha labda niweke kitu sawaHahaha Zittojuniour
I rest my case
Ila kabla sijafunga mjadala
Ni vyema Tusilete assumptions zetu wenyewe bila back up ya maandiko
Si vizuri kuwaza kwa mfano Enoko alivyoondoka mwili wake ulivuliwa ikabaki roho au la, maadamu tunajua aliondoka na mwili basi ufahamu wetu unaishia hapohapo, nje ya hapo ni speculations tu.
Au tunajua Yesu aliondoka duniani na mwili wake ule ule, leo ukisema huko mbinguni aliuvua mwili akabaki kwenye state ya roho hiyo pia inabaki ni speculations tu hatuna ushahidi wa kimaandishi kuwa aliuvua mwili na alipouvua ameuweka wapi kwa hilo hatujui.
Niko tayari kuufungua Mjadala wa UMWANZO!
Mkuu kwa kuhitimisha labda niweke kitu sawa
1. Henoko hawezi kwenda na mwili sababu Bible imesema Kutoka 33:12 kuwa hatuwezi muona Mungu tukaishi. Jibu linatoka Yohana 4:24 Kuwa Mungu ni Roho so anakuwa approached Kiroho tu basi na hii inathibitika Ufunuo 22:4 kuwa tutamuona uso wake ila tukishapata MWILI mpya sio hii ya kibinadamu 2 Kor 15 sura nzima inaelezea miilo mipya. So kwakuwa Henoko hakuelezewa kama alipata mwili mpya hivyo we can conclude kwamba hakuna binadamu anamuona Mungu including Henoko.
Kuhusu Yesu iko wazi kabisa alipata mwili mpya baada ya kufufuka hta hyo sura ya 15 imeeleza kabisa.... Kwamba yye ndio kaset precedence ya watu kufufuka na mwili mpya na ndio maana hata aliporudi kuna watu hawakumtambua akiwemo Mama yake!! Hivyo lile mwili la nyama linalozeeka aliliacha anapojua yeye ila HAKUONDOKA NAO.
Hivyo hapa hamna speculation bali ni kufuata precedence tu ya matukio mengine kuconclude kuhusu life after Death.
UMWANZO!!!
Mathayo 13
Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano (Mafumbo)?
11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
12 Kwa maana ye yote mwenye kitu atapewa, naye atazidishiwa tele; lakini ye yote asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang?anywa.
13 Kwa sababu hii nasema nao kwa mifano; kwa kuwa wakitazama hawaoni, na wakisikia hawasikii, wala kuelewa.
14 Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likisema,Kusikia mtasikia, wala hamtaelewa;Kutazama mtatazama, wala hamtaona.
JIBU: Ili kuficha siri za ufalme wa mbingu kwa watu wasio wake
Ni sawa tu na mashirika ya usalama/Jasusi hutumia mafumbo kuwasiliana ili watu msio wa shirika lao msigundue wanachoongelea yaani siri zao!!
Huenda ni tafsiri za wasomaji Biblia katika katika utohoaji wa maana na lengo la maandiko kukinzana kulingana na mtazamo binafsi naamini mbinguni kinachoenda ni RohoYesu hakupata mwili mpya baada ya "kufufuka" ndiyo maana walipoenda kaburini siku ya tatu walikuta mwili wa Yesu uleule waliouzika haupo kaburini maana yake aliendelea kuwa na mwili ule ule
Na pia kitendo cha kuwaonyesha wanafunzi wake wamguse mwili wake wajionee ilikuwa ni kuwaonyesha yeye ni yesu yuleyule ili wasidhani ni mzimu!. Kama Yesu angekuwa na mwili tofauti na wa zamani basi ingekuwa sababu ya Wanafunzi wake kumuona kuwa siyo yule original
Pili hoja ya Kumuona Mungu,
Kama mnasema kuwa Melkizedeki ni Mungu aliyeshuka duniani akiwa ndani ya mwili wa kibinadamu basi kuna watu walimuona enzi hizo akiwa ni mfalme wa Salem, mtu mmojawapo aliyemuona ni Ibarahim, Kwa hiyo kama kweli Melkizedeki ni Mungu aliyekuwa ameshuka duniani akaonwa na watu basi hataEnoko naye pia huko aliko aweza kumuona!
The other thing, Kama Yesu ndiye Melkizedeki na Yesu pia mwasema ni Mungu, basi wanadamu akina Petro walimuona na hivyo basi hata Enoko huko aliko kama Yesu ni Mungu kweli basi huenda akamuaona kama vie akina Petro, mathayo, Mariamu magdalena walivyomuona hapa duniani, Sasa kwa nini Enoko mwenye mwili asimuone Yesu aliyepaa na mwili wakati wengine wamemuona huyo Yesu na hawakudhurika?
Mi nafikiri Enock, Melkizedek na Yesu ndiyo roho moja iliyokuja katika nyakati tofautiAndiko la bibilia chimbuko lake ni miaka 7000 iliyopita. Imebainika kuwa umri wa dunia ni miaka billion kadhaa iliyopita. Kwa hiyo kuna uwezekano dunia ilikaliwa na wakazi miaka million nyingi iliyopita.
UCHAMBUZI WANGU;
Kuna uwezekano kuwa dunia imekuwa ikifika mwisho na kuanza upya kila baada ya miaka elfu kadhaa na mara zote amekuwa akitokea super human mfano wa Yesu kuwatahadharisha watu habari za mwisho huo, kwa kusema ivi namaanisha kuwa Yesu amekuwa akija duniani kila mara kabla ya dunia kuumbwa upya na tarehe kuanza hesabu upya. Namaanisha nini hapa, ni kwamba Melchizedek, Nuhu na Yesu mwenyewe yawezekana ni mtu mmoja aliyerudi duniani kwa nyakati tofauti ila kwa lengo linalofanana. Mwisho wa dunia ni mwanzo wa dunia! Inaingia akilini hii theory??
1. Kuhusu Yesu kuwa na mwili tofauti nmekwambia soma 1 korintho 15 sura nzima inasema damu na nyama haziwezi gusa ufalme wa mbinguni ndio maana Yesu alipofufuka aliweza kutoweka na kutokea mahali pengine n.k tofauti na mwanzoni alipokua na element za kibinadamu kabisa.Yesu hakupata mwili mpya baada ya "kufufuka" ndiyo maana walipoenda kaburini siku ya tatu walikuta mwili wa Yesu uleule waliouzika haupo kaburini maana yake aliendelea kuwa na mwili ule ule
Na pia kitendo cha kuwaonyesha wanafunzi wake wamguse mwili wake wajionee ilikuwa ni kuwaonyesha yeye ni yesu yuleyule ili wasidhani ni mzimu!. Kama Yesu angekuwa na mwili tofauti na wa zamani basi ingekuwa sababu ya Wanafunzi wake kumuona kuwa siyo yule original
Pili hoja ya Kumuona Mungu,
Kama mnasema kuwa Melkizedeki ni Mungu aliyeshuka duniani akiwa ndani ya mwili wa kibinadamu basi kuna watu walimuona enzi hizo akiwa ni mfalme wa Salem, mtu mmojawapo aliyemuona ni Ibarahim, Kwa hiyo kama kweli Melkizedeki ni Mungu aliyekuwa ameshuka duniani akaonwa na watu basi hataEnoko naye pia huko aliko aweza kumuona!
The other thing, Kama Yesu ndiye Melkizedeki na Yesu pia mwasema ni Mungu, basi wanadamu akina Petro walimuona na hivyo basi hata Enoko huko aliko kama Yesu ni Mungu kweli basi huenda akamuaona kama vie akina Petro, mathayo, Mariamu magdalena walivyomuona hapa duniani, Sasa kwa nini Enoko mwenye mwili asimuone Yesu aliyepaa na mwili wakati wengine wamemuona huyo Yesu na hawakudhurika?