Meli inapozama si kwamba watu wote wanakufa maji kwajili ya kushindwa kuogelea, anaejua kuogelea atagombaniwa na kuzamishwa

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178



Na hii hali inatokea hata meli ikipinduka umbali mdogo tu kutoka nchi kavu.

watu huwa wanapanik sana meli ikipinduka kila mtu asiejua kuogelea anachowaza ni kupata sehemu yoyote ya kujiokoa.

Kwa wale wanaojua kuogelea hupata mtihani maana meli inapopinduka mnakuwa wengi sehemu moja, shughuli inakuja kwa wanaojua kuogelea kutoka sehemu hio iliyojaa watu wengi.

ukionekana tu unapiga maji unadakwa mkono, mwengine atakukumbatia mgongo, n.k. utawapiga sana ngumi na mateke watu watatokwa nundu lakini wapi, hakuna ataekuachia kamwe, utatumia nguvu kubwa zaidi kwa mda mchache na hatimae mnazama wote.

Kuchomoka kwenye hali hii

1. uwe mtaalam wa kupiga mbizi

2. kama unajua kupiga maji au una dumu ila si mtaalam wa mbizi ukipata nafasi hakikisha umeangukia eneo ambalo halina mkusanyiko wa watu na usije fanya kosa la kwenda kwenye mkusanyiko wa watu kisa umemuona mama yako, baba yako, mtoto wako, mke/mme, n.k. inauma lakini kubali tu ! .
 
Kwa nn uogelee kwenye kundi la watu , piga mbuzi kimya kimya
 
Kabisa! Na hata kwenye maisha halisi it is apply same way, ni kujifanya hujui tu huku una move mdogo mdogo wanakuja shtuka upo distance away ndio uangalie unawezaje mtoa mmoja baada ya mmoja
 
Na hata ukiwa na malii watakuganda mwisho wasiku wanakuangusha, binadamu ndivo tulivyo
 
Ungeweka ka picha mkuu,tuone inavyokuwaga.[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…