R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
Na hii hali inatokea hata meli ikipinduka umbali mdogo tu kutoka nchi kavu.
watu huwa wanapanik sana meli ikipinduka kila mtu asiejua kuogelea anachowaza ni kupata sehemu yoyote ya kujiokoa.
Kwa wale wanaojua kuogelea hupata mtihani maana meli inapopinduka mnakuwa wengi sehemu moja, shughuli inakuja kwa wanaojua kuogelea kutoka sehemu hio iliyojaa watu wengi.
ukionekana tu unapiga maji unadakwa mkono, mwengine atakukumbatia mgongo, n.k. utawapiga sana ngumi na mateke watu watatokwa nundu lakini wapi, hakuna ataekuachia kamwe, utatumia nguvu kubwa zaidi kwa mda mchache na hatimae mnazama wote.
Kuchomoka kwenye hali hii
1. uwe mtaalam wa kupiga mbizi
2. kama unajua kupiga maji au una dumu ila si mtaalam wa mbizi ukipata nafasi hakikisha umeangukia eneo ambalo halina mkusanyiko wa watu na usije fanya kosa la kwenda kwenye mkusanyiko wa watu kisa umemuona mama yako, baba yako, mtoto wako, mke/mme, n.k. inauma lakini kubali tu ! .