Meli kubwa ya mizigo yashindwa kukwamuliwa katika Mfereji wa Suez kwa siku ya tatu

Sijazifatilia kwa miaka ya karibuni ila upo mwaka tulikutana na meli ya ukubwa huo Hong Kong na dock ya Singapore mabaharia mnabaki mnashangaa tuu imebeba contenna utadhani viberiti...
Hii iliyokwama Suez ina uwezo wa kubeba ngapi chief.
 
Hii ishu italeta msongamano wa Meli na tujiandae kwa uhaba wa baadhi ya bidhaa.
 
Ishaso
Inatakiwa wawaite Wanorway hiyo kitu ni dakika chache tu wanaitoa. Walitaka kuitoa Kusik ile nyambizi ya Puttin akaona ni kudhalilika
Ishasogezwa hiyo pembeni ngoma zinapita hizo tug zina nguvu kama nyati zilikua karibu nane ngoma lazima isogee wakati dock inasogezwa na tatu tuu.
 
Kwa 40ft huwa zinapungua mpaka 12,000 boxes ila twenty ni 20,000 boxes kwa meli nyingi kubwa haiwezi kubeba idadi ya 40ft na 20 ft sawa
Inabeba 20,000 TEU's hizi ni 20 ft ina maana kama ni 40ft zinakuwa 10,000. Haiwezi kuwa 12,000.
 
Hapa nimekuelewa maana kuna meli kubwa sana za mafuta huwa zinakuja na kuishia kule kigamboni ambapo tpa wana pipe yao ya kunyonya mafuta kuyaleta huku pwani......ilo dude pale halipiti
Fikiria basi siku likaja halafu likakwama kuanzia kule wavuvi wanakoegesha madau yao mpaka kule meli za Bakhresa zinakopakia abiria wake.Sijui itakuwaje siku hiyo.Safari zote kwenda Kigamboni itabidi zipitie Kurasini kwa miezi kadhaa mpaka waje mabeberu kuikwamua.
 
Anavyosema imepewa uwezo wa kuingiza meli kubwa anamaana ya kuwa Meli kubwa inaingia na inaishia baharini kwenye mkondo wa maji makubwa,kisha inakuja meli yetu ndogo inapakua mzigo kisha unaenda kushusha bandarini,ndivyo uelewa wangu huo
Hapo gharama inaongezeka au inapungua ?
 
Ni changamoto kweli.Safari hii kimbunga cha mchanga inaonekana kimechangia kujaza kifusi ndani ya Suez.Wapunguze jeuri na kupitisha bidhaa haramu.Mwenyezi Mungu akikasirika anaweza kuufukia mfereji wote kwa dakika moja tu ikawa kama zamani.
Nguruwe za mchina na heineken za mholanzi zinapita hapo
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…