Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Huku eneo la Gaza likiwa limezingirwa na Israel na viongozi kadhaa wa Hizbullah na Hamas kuuliwa inatoa ishara ya ushindi kwa Israel. Hata hivyo kushambuliwa kwa meli za kivita za Marekani na kushambuliwa kwa miji mikubwa yote ya Israel hakutoi ishara nzuri kwa usalama wa mataifa hayo na mashariki ya kati kwa ujumla.
Kutokana na mendeleo makubwa ya kiteknolojia imekuwa ni rahisi kwa mwenye nguvu kumlenga na kumuua mtu wanayemuona ni adui kwao.Wakati huo huo imekuwa ni vigumu pia kupata ushindi kwa asilimia mia moja na pia ni rahisi kwa mtu ambaye ni dhaifu kuendeleza vita kwa muda mrefu.
Kinachoendelea mashariki ya kati kwa sasa kinatoa ufafanuzi wa wazi kwa wazo hilo hasa ukilingalia kwamba pamoja na nguvu kubwa za kijeshi walizonazo Marekani na Israel hazijawanyamazisha wala kuwahofisha makundi kama Hamas,Hizbullah na Houth kurusha makombora katikati ya Israel na uwelekeo wa meli za kivita za Marekani.
Ujasiri kama huo na uwezekano wa kufikia kuleta taharuki katikati ya Israel na kwenye miji yake mikuu haukuwepo kabisa.
Bila kubadilishwa sera za Israel na Marekani hali hiyo inatosha kuoesha kuwa vita baina ya mataifa hayo na maadui zake vitakuwa ni vita endelevu vitakavyokuwa vikibadilika kulingana na wakati tu,
Mwaka 2006 Hizbullah walipigana na Israel kwa teknolojia ya wakati huo ya kupiga vifaru tu na kuitia hasara kubwa.Mwaka huu pamoja na kuzidiwa kiteknolojia hasa ndege za kivita lakini bado wameweza kwa mara ya mwanzo kupiga mpaka katikati ya taifa hilo.
Kwa ujumla bila kubadili sera na malengo pamoja na kufuata maazimio ya kuleta suluhu,Israel haitaweza kujilinda na kubaki salama usalimini mpaka mwisho katikati ya majirani zake.