ninachoogopa, kama kweli Russia amesema ana maintain relations with hamas, ni kwamba, hizi ni siku za mwisho kabisa. Mfalme wa kaskazini aliyeandikwa kwenye Biblia (yaani Russia atashirikiana na uturuki, syria) ataungana na mfalme wa mashariki yaani Iran na nchi zingine za asia (kama china), wataishambulia israel, na israel itapigwa sana. lakini hata hivyo, Mungu atashuka na kuisaidia mwisho wa siku na majeshi yao hayo yote 3/4 watafutwa. ni Neno lililotabiriwa na ukiona wale wafalme wa kaskazini na masharini wanaungana, waelewa changamkeni, mwenye kanisa amekaribia kuja, Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana, Mungu wa kweli yupo malangoni.
Biblia imetabiri kwamba atakuja ghafla kama mwivi, kama mwenye nyumba angelijua siku ile mwivi atakuja, hakika angelikesha wala asingeiiacha nyumba yake kuvunjwa. siku za mwisho zimefananishwa na mtumwa mwaminifu
Lk. 12:43-59
43. Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.
44. Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote.
45. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa;
46. bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini.
47. Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana.
48. Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.