Melo ataja sababu za JamiiForums kufungiwa

Kabisa, hatuna haraka wala sababu ya kunyamaza. Muda wa kunyamaza upo mwingi sana baada ya kufa!
 
Halafu kuna Wapuuzi hawamuheshimu huyu jamaa,.
 
Yamefungia halafu yanaingia bado kuchungulia kwa VPN!

Kule X bado page za serikali zinapost sasa unajiuliza wanapost ili watu gani waone na wao wanasema mitandao imefungiwa kwa sababu haina maadili.

Hapa ndio nimeelewa kwanini Starlink waliwekewa mizengwe hadi wafungue ofisi maana yake walitaka wakiona mtu ambaye amepost kitu wasichokipenda basi wakavamie ofisi wapewe data zake ili wamteke.

Sasa mtu anaendesha kampuni yenye ukwasi wa mabilioni ya dollar ayumbishwe na kutaka kuharibiwa brand na kinchi ambacho kinataka data za mteja zitoke bila court order na sworn affidavit?

Walichofaya kufungia JF hakuna tofauti na tume iliyobadilishwa jina tu kuitwa huru ila bado iko vilevile kimuundo ni sawa na ubovu wa nyumba ndani useme umeutatua kwa kupaka rangi mpya nje.
 
Lile jamaa la Zimbabwe lina dharau kishenzi, yaani linafanya upuuzi ule na picha linapewa hivi ikulu hawana protocol raisi anapiga picha na watu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…