Uchaguzi 2020 Membe anaweza kutuvusha upinzani kuliko Lissu

Sikiliza, Lissu yupo vizuri lakini hana ushawishi kuliko Membe. Lissu bado wakati wake
Sasa hivi twende na Membe

ushawisha wa aina gani unaouzungumza mkuu?

Mana kwa ufahamau wangu Lissu ndie mwanasiasa mwenye wafuasi na mashabiki wengi zaidi Tanzania
 
Mmemuanda muda mrefu lakini tumestuka mapema, tupo mbele yenu hatua nyingi
 
Siasa zenye nguvu ni ushawishi na watu wa kutosha nyuma ya mtu sio kukaa muda mrefu tu ndani ya chama chako.
Kumbe huwa hamjifunzi tu? Why msirecruit wanachama wenu ambao mmetoka nao mbali na die hard fans wa vyama vyenu? Kwa kufuata huu upepo na gesi ya Pepsi,CCM itaiongoza nchi hii kwa miaka mingine 30 au 50 ijayo
 

Kwa mambo niliyojifunza toka kwawale waliotoka ccm na kuingia upinzani wakijifanya watu wema, mwishowe baada ya kukamilisha kilicho wapeleka upinzani wakarudi ccm, nashindwa kuwaamini kabisa wanasiasa kama hao.
Kama Membe ni mtaji, basi agombee huko huko ccm, na wapinzani waendelee kuwatumia wapinzani kuwania hicho kiti cha urais.
 
hebu orodhesha wapinzani wa kweli tuwajue na sisi
 
Bila shaka CHADEMA na vyama vingine vyote vya upinzani for that matter wataepuka aibu hii ya kwenda kuokota matapishi kutoka ile pande kila muda wa uchaguzi unapofika. Ni fedheha na aibu kubwa mno kwa chama β€˜makini’ kwenda kuokota makapi kutoka CCM.

Hamjajifunza tu kutoka kwa Lowassa na Mr. Zero? Akili gani hizi?
 
Membe ana nguvu kubwa sana nyuma yake, anatupeleka upinzani ikulu mwaka huu. Mark my words
Hana nguvu yoyote, ana maneno mengi yasiyo na vitendo. Yeye ni kama Lowassa, anacheza huu mchezo kwa faida ya CCM tu.

Few months after election hatutamskia tena. Inashangaza mtu ambaye sehemu kubwa ya maisha yake ya siasa kawepo CCM, ila ghafla anaingia upinzani kwajili ya madaraka tu.
 
kumbe hujui unachoongea, usifate mkumbo
Husinilazimishe kuamini unachoamini wala kusema unachokitaka.
Si kwamba sijui nisemalo, ila mwelekeo wako ndo ilisababisha hayo majibu kwani ndiyo yanalingana ma maswali yako.
 
That kind of experiment ilikwishafeli 2015

Wapinzani wakirudia ujinga huo nitawashangaa sana
 
Tuambie kidogo namna alivyotumia ujasusi wake kupora the so called CHANGE YA RADAR na yale mapesa ya LIBYA. Naamini mbinu alizotumia ni za kijasusi na zinaweza kutumika kutengeneza FILAMU nzuri sana na ikatupatia mapesa ya kutosha. Tukipata hilo ndiyo tuende kwenye uwezo wake kama MPINZANI na kama ni presidential material!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…