Uchaguzi 2020 Membe anaweza kutuvusha upinzani kuliko Lissu

Uchaguzi 2020 Membe anaweza kutuvusha upinzani kuliko Lissu

Angalau Membe anaweza akawa mtu sahihi, ila kwa lissu anaweza akawa na nia nzuri akiingia Ikulu sema atatumika na chama chake kupotosha mengi
 
Kumbe huwa hamjifunzi tu? Why msirecruit wanachama wenu ambao mmetoka nao mbali na die hard fans wa vyama vyenu? Kwa kufuata huu upepo na gesi ya Pepsi,CCM itaiongoza nchi hii kwa miaka mingine 30 au 50 ijayo

Tanzania itakuwa chini ya kwa zaidi ya miaka 50 ijayo,ndio ukweli ingawa unauma!! Huwezi kumtenganisha Membe na CCM!!! UPinzani ukiingia kwenye tego hilo basi
 
Kwa hiyo mnategemea vyombo vya ulinzi kushika nchi. Kama Mh. Rais kafanya mambo mazuri yanini mtegemee vyombo vya dola kuingia ikulu? kwanini msiache free and fair election izungumze..

Ukweli ni uleule bila mbeleko za vyombo vya ulinzi CCM ni mdogo sana kwa vyombo vya upinzani...
Ndugu yangu mimi ni CHADEMA damu! Nasema kuwa tutashinda na wasitutangaze, tutafanya nini? ndiyo hoja yangu
 
Ni kweli anaweza kuwavusha uko ccm sisi huku upinzani hatumuhitaji.

Kama kweli mnampenda mpeni nafasi huko ccm.

Mwaka huu upinzani ukipokea kapi ndio utakuwa umejizika rasmi.
Wewe Nani usie muhitaji? Kwani wewe Ni mbowe
 
Mwenye uamuzi wa Nani kuwa mgombea wa chadema Ni mwenye chama Chake mbowe hayo Mambo mengine Ni ramli tu
 
Magufuli amvushe nani, uchumi wa kati kwa vilaza ndio wanakolea na hiyo swagga.
Kwa kuwa akili ni nywele na kila mtu ana zake basi tubali kutokukubaliana katika hili bila shari wala chuki.
 
Tuliza akili bro, huyu jamaa ni jasusi na ana mbinu zote za kuwezesha upinzani kushinda uraisi mwaka huu. Ni karata turufu

Bahati mbaya hizo si sifa pekee za mtu kugombea hicho cheo. Labda kama huna malengo. Membe pamoja na sifa zote hizo, hana tofauti na Lowasa. Amini usiamini , jamaa atarudi CCM tu ,hata kama si leo. Maisha ya upinzani hapa Afrika si mchezo ndugu. Hawa broilers ukijumlisha unafiki hakuwezi
 
Naona Liumumba mna taka kuwapangia upinzani baada ya nyie kuandaa fomu moja
 
Membe tangu lini akawa mpinzani? Huyo ni jasusi wa CCM, agombee CCM b CUF na ACT wazalendo! Hatuhitaji kufanya makosa kama ya Lowasa, watia nia wenye sifa wameisha jitokeza, atachaguliwa mgombea kidemokrasia apeperushe bendera ya CDM kugombea Urais!!
 
Membe is good for an additional booster rocket, though our precious PAYLOAD remains the very same Commander LISSU!
👊 ✌✌✌💥
 
Imekua ni jambo la kawaida kusikia kwamba Membe ana nguvu kubwa sana nyuma yake, hebu toeni ufafanuzi
 
Back
Top Bottom