Uchaguzi 2020 Membe au Lissu msisahau kuusema uozo wa "undugunaization", tribalism na nepotism wakati wa Kampeni

Uchaguzi 2020 Membe au Lissu msisahau kuusema uozo wa "undugunaization", tribalism na nepotism wakati wa Kampeni

Tila-lila2

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2019
Posts
652
Reaction score
1,058
Juma hili hili mtoto wa JPM - Jesca Magu amehamishiwa REA kwenye mishahara mizuri wakati juzi JPM mwenyewe alimsifia Daktari mmoja wa Falsafa aliyekuwa akifanya CCM kuwa alikuwa anapata mshahara wa shilingi laki 5 cha ajabu Magu mwenyewe bila kufuata taratibu amemhamishia mwanae sehemu yenye neema bila kufuata taratibu. Kwa ujumla kipindi hiki JPM na Serikali yake imeajiri na kuhamisha hamisha wafanyakazi kwa kinyemela sana na bila kufuata taratibu. Wafanyakazi ndugu wa wakubwa wamewekwa sehemu nzuri nzuri tu. Wanakula mishahara mizuri na ndiyo maana Magu kagoma kata kata kupandisha mishahara. Wanae na wapwa wake kama akina Doto James hawafeel pinch yeyote ya hali ngumu waliyonayo wafanyakazi wengine.

Tafadhali Membe na Lissu mkianza kampeni hebu hojini kuhusu namna taratibu zilivyofuatwa na hawa wakubwa wakati wa kuajiri haw watato. Mnaweza kuanza na huyu Jesca Magu ni sababu gani zimeletekeza ahamishiwe REA? Je, alikuwa na vigezo? REA pia ina watoto wa wakubwa wengi akiwemo mtoto wa Majaliwa mwenyewe? Je, ni kweli waliajiriwa kwa taratibu na vigezo stahili?

Inavyoonekana Sekretarieti ya Ajira kwa sasa inatumika tu kama pambo kwamba inaendesha michakato ya ajira Serikalini. Kwa sasa hamna kabisa ushindani kwenye ajira za Serikali kwa sehemu zile nyeti. Wakubwa wanapeleka tu watu wao. Hata Benki Kuu ambayo ni Taasisi iliyopaswa kuwa huru kadri iwezekanavyo kwa sasa imeingiliwa - watu hawana hata competency ya kueleweka wanapelekwa pale. Tena wengine wanasiasa kabisaa - bora hata wangepelekwa watu wa Usalama wa Taifa lakini wanapelekwa wanasiasa

Kuna hili la ukabila ambao limeonekana kabisa kwa uwazi. Dar-es-Salaam pamoja na kuwa ni kama haina ukabila lakini inaonekana WaSukuma wengi wameandaliwa kugombea Dar. Jaribuni kuangalia majimbo yote ya Dar yalikuwa na wagombea WaSukuma na watu wa Kanda hiyo ambao mpango ni kuwapitisha wote wagombee isipokuwa Ubungo tu. Huu mpango upo na baada ya muda kidogo mtaamini ninachoandika hapa

Ili kurekebisha hali hii Memba au/na Lissu tafadhalini mliseme sana hili wakati mkiomba kura zetu. Viongozi hawa warudi kwenye misingi ya ushindani sahihi uliowekwa na Mkapa na Kikwete. Nafasi za kazi za vyeo hata Taasisi nzuri kama REA, SSRA, EWURA, TCRA, TIRA, PSPF, PSSF, TBS, TPA, TRA, BOT, TIC n.k zote zilikuwa zinatangazwa. Kwa sasa huoni Taasisi hizo zikitangaza nafasi za kuanzia Mameneja wala Wakurugenzi. Wanapelekwa tu wale wanaohusiana kindugu, kimahaba, kikabila, kirafiki n.k.

Ili kuongea hayo kwa evidence mnaweza kuanza na Taasisi hizo kuangalia wafanyakazi wote wenye vinafasi walioingia kuanzia Mwaka 2018 Machi, mtakuta uozo sana sana. Na taarifa hizo mtazipata tu kwani mwenyewe nimefanya utafiti na nitawaletea ukweli wote kwa namana ninayoijua mimi!.
 
Miaka ya nyuma haya mambo yalikuwa yakisikika zaidi Kenya ambapo huwezi kuwa Waziri Mkikuyu na ukawa unaendeshwa na dereva Mjaluo.lakini nasikia huko yameanza kupungua.Hapa kwetu Nyerere alijtahidi sana katika hili lakini malalamiko yalianzia awamu wa pili na kuendelea.

Hili si jambo jepesi kulizungumzia kwani,mosi kiongozi Mkuu wa nchi halazimiki kuchukua ushauri wa mtu yoyote (ana kinga ya kikatiba) na jambo la pili ni pale ambapo wanaowekwa wanakuwa na vigezo (Elimu,uzoefu n.k).

Kwa hili la ukabila na ukanda ni utashi wa Kiongozi Mkuu na ni imani yake pekee inayoweza kumfanya asifanye anachofanya lakini katiba na kanuni zingine zinampa kinga.

Binafsi ningependa tujadili kwa mfano hili la DAS kuteuliwa hadharani na wateuliwa wakiwa sio watumishi wa umma kama miongozo inavyoelezea.
 
unatumia wowowo kufikiria...


Rais alikuwa Mchagga?
Jibu hoja mkuu acha matusi.
Kuna kipindi wazuri Mramba aliulozwa bungeni kwamba "kwann wachaga wamejazana BoT, TRA Bandarini na nyingine zenye fedha"? Akajibu kwa nyodo kwamba ndiyo wenye sifa.

Sasa kitesa kwa zamu. Acha wagosha nao watese ndiyo muda wao.
 
Anzia kwa mwenyekiti wa Chadex kwanza ukiweza kumpa vipande akaachia kijiti na kuruhusu demokrasia itawale chamani ndio uje kwa wana Chichiem!

Swala la Nepotism nalipinga ila ikiwa waliosogezwa kwenye system kwa mbeleko ya Mwenyekiti wana sifa zote sioni kama kuna shida. Pambana na hali yako tu mzee. Huenda wewe ulianzia shinani sasa umefikia tindini unalia lia.

Kila zama na kitabu chake, hata jamaa alianzia tindini sasahivi yuko kwenye shina la muwa anainjoy glucose ya kutosha na wakwake.
 
Wanahamisha watoto/ndg zao kwa vimemo kwny vitengo vya maana halafu wakitoka hapo wanawaambia watoto wa masikini serikali haiwezi kuajiri watu wote nyie nendeni mkajiajiri,maana kuna vitambulisho vya wamachinga.

Kipenzi cha wanyonge bana.
 
Mangi mleta mada naona unatamani enzi zile zirudi ambako kila kona lugha ya mangi ilikuwa lugha ya taifa kwenye kila

kila ofisi aikambe aikambe ha ha ha .Sahau nyakati hizo zinapita kasi na usitegemee zirudi tena kwa heri ya kuonana jipange tu kisaikolojia
Mimi siyo mmoja wao, lakini akina mangi wako flexible na wana spirit ya juu, ona biashara zao zilivyotapakaa kila kona. Wengine waliokuwa na biashara kariakoo wamehamia Zambia, Malawi, DRC n.k. Hawa jamaa nawavulia kofia kwa uchakarikaji wao, wako kama wahindi na waarabu, hawako serikalini wala mashirika ya umma lakini mziki wa biashara zao wote tunauona.
 
Hili kweli kabisa Mana sitasahau tulivyo Fanya interview za REA. Tukaingia mpaka oral Ila waliokuja kuitwa aisee lo inauma sana. Psrs ni madudu tu. Watu wananeemeka wengine tunahausle. Tunajua kunawatu waliitwa kindugu na majina hayakuwa publish online kukwepa aibu ya ulasimu.

Yani pamoja na kufukuza watu wenye vyeti feki lakini hamna kitu kabisa.
 
Kwa sasa kila sekta utakuww mkubwa ni msuu... malizia na ...**** liko waz kabisa ushahidi wa kutosha angalia mashirika yote ya serikali saivi...kagua yote
 
Hili kweli kabisa Mana sitasahau tulivyo Fanya interview za REA. Tukaingia mpaka oral Ila waliokuja kuitwa aisee lo inauma sana. Psrs ni madudu tu. Watu wananeemeka wengine tunahausle. Tunajua kunawatu waliitwa kindugu na majina hayakuwa publish online kukwepa aibu ya ulasimu.

Yani pamoja na kufukuza watu wenye vyeti feki lakini hamna kitu kabisa.
Waliombiwa wana vyeti fake walifukuzwa ili ndugu wa watu wapate pa kushika
 
Wanahamisha watoto/ndg zao kwa vimemo kwny vitengo vya maana halafu wakitoka hapo wanawaambia watoto wa masikini serikali haiwezi kuajiri watu wote nyie nendeni mkajiajiri,maana kuna vitambulisho vya wamachinga.

Kipenzi cha wanyonge bana.
Looo
 
Mangi mleta mada naona unatamani enzi zile zirudi ambako kila kona lugha ya mangi ilikuwa lugha ya taifa kwenye kila

kila ofisi aikambe aikambe ha ha ha .Sahau nyakati hizo zinapita kasi na usitegemee zirudi tena kwa heri ya kuonana jipange tu kisaikolojia
Wewe ni kichaa uliotukuka na Ndo mana umepigwa chini na wana CCM wenzako kigamboni juzi.

CCM ya magufuli mmejaa kujitoa akili na ufahamu tu. Hamna lolote la msingi mnalofanya.

Na kwa jinsi mlivyoiharibu hii nchi kwa ukanda na ukabila nawaambia mwaka huu ndo mwisho wenu kutawala Tanzania
 
Back
Top Bottom