Miaka ya nyuma haya mambo yalikuwa yakisikika zaidi Kenya ambapo huwezi kuwa Waziri Mkikuyu na ukawa unaendeshwa na dereva Mjaluo.lakini nasikia huko yameanza kupungua.Hapa kwetu Nyerere alijtahidi sana katika hili lakini malalamiko yalianzia awamu wa pili na kuendelea.
Hili si jambo jepesi kulizungumzia kwani,mosi kiongozi Mkuu wa nchi halazimiki kuchukua ushauri wa mtu yoyote (ana kinga ya kikatiba) na jambo la pili ni pale ambapo wanaowekwa wanakuwa na vigezo (Elimu,uzoefu n.k).
Kwa hili la ukabila na ukanda ni utashi wa Kiongozi Mkuu na ni imani yake pekee inayoweza kumfanya asifanye anachofanya lakini katiba na kanuni zingine zinampa kinga.
Binafsi ningependa tujadili kwa mfano hili la DAS kuteuliwa hadharani na wateuliwa wakiwa sio watumishi wa umma kama miongozo inavyoelezea.