Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Hahaaa..... wapambe mmeshindwa kumchangua shujaa wenu msiba?

Yuko mwingine alisingizia watu madawa ya kulevya.

Kesi zake zitafunguliwa hata baada ya miak 30 mbele. Ajiandae tu.
Mkuu Bush, kumbe mafaili bado hayaja fungwa, yanasubili muda mwafaka ama?
 
Halafu huyo ndio alitaka kuwa kiongozi wa nchi mwenye kinyongo cha kutu. Basi atakufa bila kusamehe na Mungu naye hatamsamehe kwa chochote hata kama akitubu kwa kutoa machozi ya damu.

Kuna sababu maalum Mungu amekusudia kwa Membe kuwa na kiburi cha umimi wa kibinadamu kwamba aabudiwe. Huyu inawezekana ndio alishiriki mchezo mchafu
Shujaa wenu Magufuli alikuwa anasamehe?
 
Musiba kama musiba hakuna sehemu aliyonishangaza na kunifurahisha kama alivosema eti Magufuli ni Rais wa Leo,kesho na hata milele,Membe baba shikilia hapo hapo maana hii nchi tumezidi kuendekeza watu wajinga na mambo ya kijinga
 
kiongozi asiyesamehe hafai kuongoza watu membe huyu huyu je angekuwa raisi ingekuwaje ! kipimo cha akili ni karma
Mkuu ni kweli, kusamehe kupo lakini kunaendana na mazingira yenyewe. Kwa mazingira ya muhusika na aliyekuwa ana mtumikia nao neno "kusamehe" halikuwemo kwenye kamusi yao. Hiyo ndiyo "tit-for-tat
 
Duh..., kama mwandishi huyu, ambaye mimi nilimuona kama ni mwandishi kilaza, kanjanja na kichaa kabisa Kichaa mmoja, anaweweseka sana juu ya Zitto, kamtungia uongo, umebuma, Zitto tuko nae hapa Dodoma, anamiliki mali kama hizo!, then huyu jamaa ni kichwa sana!. Ametuheshimisha sana, hivyo najiunga na Maaskofu, Membe amsamehe tuu!.

Kitendo cha Membe kutowatii maaskofu kitamgharimu sana!. Kuna kiongozi fulani aliwahi kuwadharau maaskofu, najua ni nini kilikuja kumtokea, hivyo sitaki Membe yamkute ya kumkuta!. Amsamehe tuu Musiba!.

P.
Maaskofu hawa hawa credibility ya kuweza kuwana divine power labda kama wana ufahamu wa kuzimu.

Hawa ni makada tena machawa wa Magufuli na CCM watiifu, hivi uliwahi kiwasikia wakimuomba Magufuli asiteke, asifilisi watu, kushambulia kondoo zao?
 
Maaskofu wametimiza wajibu wao kama watumishi wa kanisa. Inaelekea Musiba ameshalitambua na kujutia sana kosa lake, ijapokuwa amechelewa sana kuomba msamaha kwa Membe, na kwa wengine. Ameng'amua njia iliyobakia pekee kwake ni kuwatafuta viongozi wa kidini wenye ushawishi ili wapate kumuombea msamaha kwa Membe.

Sisi sote ni binadamu, na wote tunatenda makosa. Kama Mungu angalituhesabia makosa yetu tuyafanyayo kila iitwapo leo, hakika hakuna miongoni mwetu ambaye angestahili kuishi. Lakini ni vyema Musiba asitake kuuzunguka mbuyu, atoke hadharani tu na kumuomba msamaha Membe na wengine wote aliowakosea, tena kwa namna ile aliyoifanya kupitia vyombo vyake vya habari.Natambua Membe ni muumini mzuri, na tena ana kicho mbele ya Mungu wake. Anitambua amri kuwa anapaswa kumpenda jirani yake kama vile ambavyo anajipenda yeye mwenyewe. Ndiyo! Ni kweli alikosewa mno na Musiba, na dunia yote inatambua hivyo, na hata mahakama imethibitisha hivyo, lakini kama binadamu yeyote yule mwenye nafsi hai, anaweza kutafakari nukuu ifuatayo kutoka katika kipande cha Neno la Injili,

MATHAYO 18

15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwambie kosa lake mkiwa ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako.

16 Kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili kusudi wawepo mashahidi wawili au watatu wa kuthi bitisha jambo hilo.

17 Akikataa kuwasikiliza, liambie kanisa. Kama akikataa kulisikiliza kanisa, basi mhesabu yeye kama ni mpagani au mtoza ushuru.
Hawa siyo watumishi wa kanisa bali ni makada watiifu wa CCM.
Siyo watumishi wa kanisa bali ni chawa wa Magufuli.

Hivi uliwahi kuwasikia wakikemea madhila ya wale walioumizwa na matendo ya Magufuli?
 
Mkuu

Kufunga goli dakika ya 89. Ni kauli ya kijasusi sana kuliko unavodhani!

Unafikiri kufukuzwa kwake ccm ni Bahati mbaya!!!?

Alipaswa abaki ILI mwendazake amshulikie akiwa NDANI kuliko nje!

Kachero akiwa nje ana uhuru wa kutosha wa kufunga goli na kweli alifunga KWA kwenda Dubai na kurudi nchini dakika za mwisho!

Na ACT kutakua chama kikubwa sana tena chenye ushawishi mkubwa baada ya chadema kufa!!!

Zito anaenda kuwa mwenyekiti wa chama mkuu wa upinzani nchini!!!

Ujio wa Membe ACT haukua wa Bahati mbaya!!
Wa kuiuwa CHADEMA nani?
NCCR mageuzi mlifanikiwa
CUF mkafanikiwa
Sasa mnaiombea CHADEMA kufa?
Poleni!!!
 
Musiba hakuwa na kosa maana alichokuwa anakisema walikitenda ila kwa kuwa ndio wenye nchi hawataki kudhalilishwa hadharani kwamba walikengeuka. Akiendelea kulipiza kisasi juu ya Musiba Mungu naye atalipiza kisasi kwa kuwa baya halilipwi kwa ubaya ili umfundishe aliyekunda ubaya ajifunze kuwa na kiasi.
1. Musiba alimtenda vibaya mlalamikaji
2. Musiba aliwatendea wema Watanzania wengi kwa kuweka wazi uovu wa viongozi wa kisiasi wanapopewa dhamana ya kuwatumikia wanajinufaisha wenyewe
Wewe ni Musiba nenda kalipe tuondolee upuuzi wako
 
Mahakama kujihusisha kuamua kesi za madai zenye mlengo wa kisiasa kunaenda kuua demokrasia, uhuru wa kutoa habari na maoni na kunaenda kuziba watu midomo kuibua kashfa mbalimbali za uhujumu nchini kwa kuhofia kuamuriwa na mahakama kulipa fidia za bilioni 9!!!
Kiungo unachotumia kufikiria kina walakini, nyie akina Musiba mlidhalilisha utu wa watu kwa kulindwa na shetani Magufuli sasa mmegeukwa.

Waluguru wanasema mulungu chimbidu maana kigeugeu kawageuka
 
Wakati dalali wa Mahakama kampuni ya Yono (vijana wa kazi) ikihesabu siku zilizobaki katika 14 (siku za kazi) alizolewa mtukanaji Cyprian Majura Musiba kumlipa fidia Kachero Bernard Membe jumla ya shilingi 9.2 Bilioni, Bwana Musiba amewaangukia viongozi wa dini Askofu Alex Malasusa (KKKT Diyosisi ya Pwani) na Kardinali Porlycarp Pengo kumwombea msamaha kwa Membe asipige mnada mali zake.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Membe nyumbani kwake Mikocheni zinaeleza kwamba Jumatatu ya tarehe 24/4/2023 majira ya saa 10 alasiri mjumbe kutoka kwa Pengo alifika kwa Membe kumpa ujumbe wa Pengo kumsihi amsamehe Musiba.

"Alikuja hapa padre wa moja ya makanisa yetu kuleta ujumbe huo lakini naona Mzee alimkatalia na kumwambia 'namheshimu sana baba Askofu Pengo lakini kwenye hili anisamehe yeye (Pengo) huyu kijana lazima alipe gharama ya matusi yake' " anasema mwanafamilia aliyetajwa kwa jina la Colleta na kuongeza:

"Lakini jioni yake ya saa moja Askofu Malasusa naye alimpigia simu Mzee kuongelea suala hilo hilo lakini naye Mzee alimpa majibu yale yale aliyompa mjumbe wa Pengo." Hata hivyo kwa maelezo ya Colleta ni kwamba si tu ni msimamo wa Mwanadiplomasia huyo Bali ni msimamo pia wa familia.

Hii inakuja baada ya jitihada za Askofu Mwamakula pia kugonga mwamba baada ya kumwandikia barua Membe ya msamaha kwa Musiba.

Wakati hayo yakijiri hapa Mikocheni, tayari kampuni ya Yono imeshatua jijini Dodoma itakapoanzia kazi ya mnada kwa kuanza na apartments za Musiba zilizoko Ihumwa, nyumba yake ya Chamwino, guest house yake ya Msalato na shamba la hekari 10 njia ya Singida.

Baada ya hapo Yono atatimba apartment ya Kigamboni, shamba la hekari 5 Bagamoyo kabla ya kugeukia mitambo yake ya uchapaji iliyoko jengo la Exim ghorofa ya 8 jirani na Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe kwamba huko nyuma Musiba alichapa magazeti yake kampuni ya Malindi Printing huko Mbweni ambayo ni mali ya TISS. Jambo hili lilileta ukakasi wa kisheria kwani sheria ya vyombo vya habari (2016) inamtaka mlalamikaji kumshitaki Mwandishi, mhariri, mchapaji na msambazaji. Kwa mantiki hiyo DG wa TISS angetakiwa kusimama kortini. Ili kuokoa jahazi Musiba "alinunuliwa" mitambo mingine Mpya kutoka Ujerumani na kwa "huruma" mwana TISS Membe aliridhia. Nayo itanadiwa baada ya siku 14 kutamatika pamoja na nyumba na mashamba yake ya kijijini nakadhalika.

My take: Vijana tujifunze kitu katika sakata hili la Musiba na Membe kwamba tuwe na akiba ya maneno. Lakini pia akili ya kupewa changanya na zako. Waliokuwa wakimpa akili karibia wote wamemkimbia tena ndio wamekuwa jirani na Membe. Amtegemeae mwanadamu mwisho huwa kama hivi. Musiba kwishney!
Viongozi wa dini wanaponyamazia mambo mabaya kufanyika kwenye jamii;alafu sheria zinaposimama kwenye mkondo wake hujitokeza kama hivi Sasa, inashiria kwamba walikuwa timu moja
 
Kiungo unachotumia kufikiria kina walakini, nyie akina Musiba mlidhalilisha utu wa watu kwa kulindwa na shetani Magufuli sasa mmegeukwa.

Waluguru wanasema mulungu chimbidu maana kigeugeu kawageuka
Acha kupandwa na mihemko wewe binti, kuwa na adabu.
 
Back
Top Bottom