Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mh Membe popote ulipo, tambua una KURA yangu tayari.Bernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.
Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.
"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.
Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
Miundombinu inajengwa kwa kodi za wananchi na sio hisani au mshahara wa rais. Hivyo miundombinu itajengwa na yoyote hata kama nchi itakuwa haina rais kwani mipango ya nchi ipo tayari.
Magufuri jembe
Sisi zetu kuni tuMbwa kala mwanae...hasa ule upinzani wa ndani ndio umeanza rasmi. Hebu chadema na AcT tuachieni uwanja tutifuate. Huu mtifuano hatutaki kugombelezewa....mtuache jameni.
Inaudhi kupita kiasi kwa wahusika, kuhusu 'vijimambo' vya namna hii vinavyochokonoa chokonoa, lakini haviumi vya kutosha kujibu mapigo.Self-explanatory.
Naona jamaa anaendelea tu kuwakata watu maini. Watajuuuta kumchokonoa!
View attachment 1173321
huu ni uhaini
Akili zimeanza kuwa siyo sawa baada ya kusema anagombea urais?Huyu mzee sidhani kama ana akili sawa sawa kwa sasa. Kwanza umri wake tu unasuggest anapitia serious mental condition ya midlife crisis.
Ukisikia uzee kuja vibaya ndio hivi sasa. Hizi ndoto za mchana, badala akae na wajukuu zake afurahie maisha anaanza upuuzi.
Ndio. Maana life expectancy ipo chini Tanzania sababu watu wakifika umri unaotakiwa wawe na utulivu wao ndio wanaanza fujo.
''KAMA NI MAENDELEO TUNGEWEZA KUYAPATA HATA CHINI YA MKOLONI, LAKINI UHURU WETU ULIKUWA NA MAANA KULIKO MAENDELEO YA WAKOLONI''Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.
Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.
We jamaa ujue una akili sana! YANI UMEJUA KUNITENGENEZEA SIKU YANGU !Miundombinu inajengwa kwa kodi za wananchi na sio hisani au mshahara wa rais. Hivyo miundombinu itajengwa na yoyote hata kama nchi itakuwa haina rais kwani mipango ya nchi ipo tayari.