Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

UVCCM mbona mpo kimya kuhusu waraka wa kina Kinana? si kawaida yenu.
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.
hivi unaijua CCM wewe? achana kabisa na hili kitu...Membe si mbumbumbu kama wana Lumumba walio wengi..anaijua CCM nje ndani.
 
hivi unaijua CCM wewe? achana kabisa na hili kitu...Membe si mbumbumbu kama wana Lumumba walio wengi..anaijua CCM nje ndani.
Sawa. Hata EL anaijua Chadema na CCM nje ndani.
 
Ni haki yake kikatiba kuna tatizo gani akiitumia? Maadam JPM anafanya kazi natumai kazi zake zitakuwa kigezo cha yeye kuchaguliwa tena ndani ya chama hivyo natamani kuona uchaguzi huru na haki ndani ya chama atakayeshinda ashinde!
Umenena vyema Sana mkuu
 
Kumbuka kuwa kama usemavyo kuwa pengine anatumia kanuni unazoziita za Colin Powell basi kama ni kweli Membe asisahau kuwa na EXIT strategy!!
 
Kuna la ajabu hapo mpaka usiamini, huoni juzi kakiri kuwa sauti iliyodukuliwa ni ya kwake? Kama ameweza kukiri yale atashindwa kuzungumza hayo? Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi hawaridhishwi na namna Magufuli anavyoongoza chama chao na nchi kwa pamoja kwani kajigeuza kuwa mkubwa kuliko chama na nchi. Sasa huyo Membe anachofanya ni kumuonyesha kwamba yeye sio mkubwa kuliko chama au nchi, hivyo yuko tayari kupambana naye ili kumuonyesha hana madaraka zaidi ya hayo anayopaswa kuwa nayo.

Mimi ninaamini Membe hawezi kuwa rais mzuri, lakini huyu wa sasa sio mzuri pia. Na pia tulishatoka kwenye kuongozwa kwa vitisho na kusujudia viongozi. Sasa hivi tunataka kiongozi anayeheshimu wananchi sio anayeogopwa na wananchi kisa anapandikiza hofu. Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni.

“Kama ni maendeleo tungeweza kuyapata hata chini ya wakoloni, lakini uhuru wetu ulikuwa na maana kuliko maendeleo ya wakoloni”[emoji419]
 
Kwanza anatakiwa kuchukuliwa hatua na Chama chake baadae ile sauti yake iliyodukuliwa kusambaa. Hii ya kugombea anasema ili wakimfukuza apate agenda ya kisiasa eti baada ya kuonesha nia ya kugombea urais 2020 ndo amefukuzwa chamani.

Membe anatakiwa kufukuzwa fasta CCM ili akastaafie siasa akiwa opposition.

[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Self-explanatory.

Naona jamaa anaendelea tu kuwakata watu maini. Watajuuuta kumchokonoa!


20190805_235007.jpg
 
Braza Membe, Ulipoapa kula kiapo cha Ujasusi tangu ukiwa kijana mbichi kabisa uliapa kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ulikula Kiapo cha kutoogopa mtu yoyote bali Taifa kwanza. Kwa sasa Tanzania inakuita ukainusuru isiendelee kuserereka kuelekea shimoni, shimo ambalo tukishagota chini itakuwa ni gharama kubwa sana kuweza kutoka!. Na sioni namna nyingine ya wewe kuipigania nchi yako zaidi ya Kuchukua fomu, kugombea na uwe raisi ili ukarekebishe makosa makubwa makubwa ambayo yamefanyika kwenye miaka hii minne.

Sina wasiwasi kuwa kama ni SGR utajenga, tena utaiongezea urefu hadi mikoa mingine
Sina wasiwasi kama ni Flyover utajenga, tena nzuri na nyingi zaidi
Sina wasiwasi kama ni umeme utaleta tena wa gesi ulio clean na wa maji pia
Kama ni barabara utajenga tena imara kufika hadi kila kata.
Kama ni elimu bure, utatoa hadi form six

ILA AMBACHO NI MUHIMU ZAIDI,SINA WASIWASI KABISA KWAMBA UTALINDA NA KUITETEA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA HAKI ZA RAIA NA KWAMBA KWENYE KUTIMIZA MAJUKUMU YAKO HUTAONEA WALA KUPENDELEA MTU KWA MUJIBU WA UDINI, UKABILA, UKANDA AU CHUKI ZA KISIASA!

Chukua Fomu Jemedari, Tuko nyuma yako!
 
Be the first to reply..........listen! Pick up I'm calling u brother Membe. Here we go..
 
Back
Top Bottom