Tetesi: Membe kupokelewa Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo?

Tetesi: Membe kupokelewa Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo?

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Aliyekuwa kada wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi, Waziri wa Mambo ya Nje, Kachero mbobezi kama anavyoitwa na wapambe wake, Ndugu Bernard Membe anatazamiwa kujiunga na Chama Cha ACT-Wazalendo pindi chama hicho kitakapofanya uchaguzi wa ndani kuchagua viongozi wakuu wa chama hicho.

Chama hicho kinapanga kumpatia Membe nafasi ya Mshauri wa chama ambayo kwa sasa inashikiliwa na Maalim Seif ambaye anaenda kuchagukiwa kuwa Mwenyekiti.

Mchakato wa Membe kujiunga CHADEMA umekuwa mgumu kwa sababu ya historia ya Mzee Lowasa na wenzake ambao walikitumia Chama hicho kugombea na hatimaye kurudi zao CCM.

Aidha Membe amehakikishiwa nafasi ya kugombea urais ndani ya ACT-Wazalendo ambako ndani ya CHADEMA walimuambia wao akienda aende pasipo masharti ya kugombea maana tayari wamemuandaa Tundu Lissu kuwa mgombea wao japo hawajafunga kabisa room ya majadiliano.

Na hizo ndizo mpya katika siasa zetu hapa bongo.
 
Siasa za Tanzania ni siasa za madaraka!

Sio chama tawala wala wapinzani, wote wanaongelea madaraka!

Hizi ni siasa za kibinafsi ndio maana kwenye masuala ya kulipwa mishahara, ruzuku na posho wote huwa kitu kimoja!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Siasa za Tanzania ni siasa za madaraka!

Sio chama tawala wala wapinzani, wote wanaongelea madaraka!

Hizi ni siasa za kibinafsi ndio maana kwenye masuala ya kulipwa mishahara, ruzuku na posho wote huwa kitu kimoja!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ndiyo siasa wewe ulitakaje labda mkuu?

In God we Trust
 
Wao wanaamini watamshinda Dr. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI.
Bila hii hirizi saa nne asubuhi tu chaliiii
FB_IMG_1582080397242.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Navyoona mimi wamuache atimize ndoto kama alivyoota wasimukatize ndoto yake ya urais. Uzuri wa ndoto ni pale asubuhi ukiamuka unajikuta bado uko kwako pale geto Sinza wala hukuwa Merikani kama ulivyoaminishwa kwenye ndoto. Then life goes on!!!!
 
Jamani huyu mzee mungemuacha sasa kwani lengo lenu la kumfukuza tayari limekwishatimia
 
Safi sana hii ni habari njema mno.

Mapambano ya kudai demokrasia ya kweli, kuondoa uonevu nchini na kunusuru uchumi wa nchi lazima yapiganwe kwa nguvu zozote popote pale nchini.
 
Nilisikitika kufukuzwa Membe CCM. Mtazamo wangu ni kuwa Membe hafai kuchukuliwa na wapinzani kubebe bendera yao kwa sababu ni mtumishi wa ile idara nyeti hivyo bado anatumikia CCM kama agent, Pili huyu jamaa ni muongo wa kupita kiasi. Nchi haiongozwi kwa uongo.
 
Back
Top Bottom