Tetesi: Membe kupokelewa Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo?

Tetesi: Membe kupokelewa Mkutano Mkuu wa ACT-Wazalendo?

Nilitonywa ili jumamosi ya juzi,sasa naanza kuamini.
Pili,mnyetishaji aliniambia baada ya yeye kwenda ACT na baada ya uchaguzi mkuu ACT itapata wabunge wengi kuliko chadema na ndio kitakuwa chama kikuu Cha upinzani maana kwa upande wa Zanzibar ACT itapata support kubwa kutoka kwa ACT.
Mwisho kabisa jamaa alinitonya kuwa CHADEMA ndio itakuwa kama NCCR au TLP Yani mbunge/wabunge wao watakuwa wachache Sana tena ni wa kutafuta na torch.Na ACT itapata support kubwa kutoka kwa CHAMA TAWALA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hizi ni propaganda za karne ya 15 ambazo kwa karne hii ni aibu kuziweka hapa.

CCM hawajawa wajinga kiasi hicho cha kuwahonga ACT wabunge wengi ili kiwe chama kikuu cha upinzani.

Ajenda kuu ya CCM ni wapinzani wasipate hata Kiti kimoja cha Ubunge 2020.

ACT itapata Wabunge Wengi Zanzibar tu bila ya Support yoyote kutoka Chama tawala.

Hii ndiyo shida ya Watanzania, Yaani Vijana wa Chadema baada ya kupambana na CCM basi munapoteza Nguvu kubwa kupambaba na ACT/Zitto Kabwe.
 
Hao Chadema wanapojiita chama cha demokrasia na maendeleo wanamaanisha nini? Kwa nini wameshapanga eti Tundu Lissu ndo mgombea wao wa Urais bila kutoa room kwa wanachama wengine kugombea?

Hata Membe alipaswa kuachwa ajiunge nao kama angeamua kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Urais wamruhusu kura za wanachama zingeamua maana hiyo ndo demokrasia ya kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko ndo kuminya democrasia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za Tanzania ni siasa za madaraka!

Sio chama tawala wala wapinzani, wote wanaongelea madaraka!

Hizi ni siasa za kibinafsi ndio maana kwenye masuala ya kulipwa mishahara, ruzuku na posho wote huwa kitu kimoja!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Sijui una umri gani wewe hapo ulipo. Wewe kwa akili zako unafikiri dhumuni la chama chochote cha siasa ni nini hapa duniani.

Au vinginevyo, unafikiri vilabu vyoote vya mpira duniani lengo lao hua ni kitu gani.
Please reset your mind.
 
Aliyekuwa kada wa muda mrefu wa Chama Cha Mapinduzi, Waziri wa Mambo ya Nje, Kachero mbobezi kama anavyoitwa na wapambe wake, Ndugu Bernard Membe anatazamiwa kujiunga na Chama Cha ACT-Wazalendo pindi chama hicho kitakapofanya uchaguzi wa ndani kuchagua viongozi wakuu wa chama hicho.

Chama hicho kinapanga kumpatia Membe nafasi ya Mshauri wa chama ambayo kwa sasa inashikiliwa na Maalim Seif ambaye anaenda kuchagukiwa kuwa Mwenyekiti.

Mchakato wa Membe kujiunga CHADEMA umekuwa mgumu kwa sababu ya historia ya Mzee Lowasa na wenzake ambao walikitumia Chama hicho kugombea na hatimaye kurudi zao CCM.

Aidha Membe amehakikishiwa nafasi ya kugombea urais ndani ya ACT-Wazalendo ambako ndani ya CHADEMA walimuambia wao akienda aende pasipo masharti ya kugombea maana tayari wamemuandaa Tundu Lissu kuwa mgombea wao japo hawajafunga kabisa room ya majadiliano.

Na hizo ndizo mpya katika siasa zetu hapa bongo.
Hivi kweli unafikiri shushushu mbobezi kama mnavyomuita! Anaweza kweli kuisaliti mamlaka iliyopo??? Kwa umri aliyofikia membe ni vigumu sana kuisaliti mamlaka iliyoko. Labda useme huko anaenda kikazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ACT ni ya kwake Membe wala aendi kujiunga labda kufukuza asiowataka kwenye hicho chama chake.
 
Waache wajidanganye na hizo ndoto zao.Magufuli yuko vizuri,atashinda asubuhi na mapema.💪
Yeyote yule kuanzia ngazi ya shina aliyepitishwa na ccm ni mzuri tuu wala hakuna kuangaika na anaweza kuwa mbaya wakati wowote akitemwa na ccm.
 
Sometime huwa najiuliza sana,ulaya mtu akigukuzwa chama anaweza staff au kama ni hujuma basi anajiengua mapema nakufanya mambo mengine,,,
Sisi ngozi nyeus!dah!tamaa ya madaraka.
Hivi kwani ukipumzika tu ukafanya mishe zako ukawaachia wengine utaoungukiwa ninj?ni lazima uwe mwanasiasa?
This is very logic,hebu tutafakar sana,hawa wanasiasa wetu ni watu fulan wenye kutafuya masrah yao binafsi kuliko wananchi wao
 
Navyoona mimi wamuache atimize ndoto kama alivyoota wasimukatize ndoto yake ya urais. Uzuri wa ndoto ni pale asubuhi ukiamuka unajikuta bado uko kwako pale geto Sinza wala hukuwa Merikani kama ulivyoaminishwa kwenye ndoto. Then life goes on!!!!
Mzee wa monduli na ndoto yake hajaamka tu. Kitambo sasa
 
Siasa za Tanzania ni siasa za madaraka!

Sio chama tawala wala wapinzani, wote wanaongelea madaraka!

Hizi ni siasa za kibinafsi ndio maana kwenye masuala ya kulipwa mishahara, ruzuku na posho wote huwa kitu kimoja!


Sent from my iPhone using JamiiForums
Nyuma ya madai ya demokrasia na Tume Huru ya Uchaguzi ni dhana potofu kuwa wanasiasa watapata madaraka kwa njia ya mkato ili kutimiza agenda na malengo yao binafsi.
 
Kikwete Atagombea Kupitia Chadema.

CCM itaangushwa na MwanaCCM
 
Back
Top Bottom