Mackanackyyy
JF-Expert Member
- Mar 26, 2019
- 2,338
- 5,271
Acheni kuweweseka basi Mataga, mlianza kuamini kuwa Lissu mmempiga risasi amekufa hakufa...Mkuu Lissu kajichanganya, watamfix kwa kuanza kampeni kabla ya wakati. Alikuwa na haraka ya nini kuanza kupanda majukwaani na kuanza kuuza sera za CHADEMA. Kama akichomoa basi itakuwa tu ni huruma ya Tume, vinginevyo anachomolewa saa moja asubuhi.
Mkaamini hawezi kurejea nchini kabla ya Uchaguzi akarudi
Mkaamini hawezi kuteuliwa na Chadema akateuliwa..
Mkaamini hawezi kupewa Form na Tume akapewa...
Mkaamini hawezi kupokelewa mikoani na wananchi, akapokelewa kwa maelfu..
Sasa mnaamini hawezi kuteuliwa na Tume, Ujinga tu unawasumbua...
Tamasha la Wasanii wa CCM Uwanja wa Uhuru ilikuwa ni kitu gani? Kampeni ama si kampeni?
Hofu ya nini bandugu???
Magu alipowaambia Wapentekoste wasimchague Lissu ilikuwa ni Kampeni ama si Kampeni?
Aliponunua Jogoo kwa sh. 100000 ilikuwa ni Kampeni ama si Kampeni?
Alipoahidi kupanua barabara ya Dumila baada ya kula mahindi ya kuchoma ilikuwa ni kitu gani anafanya?