Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Mkuu Lissu kajichanganya, watamfix kwa kuanza kampeni kabla ya wakati. Alikuwa na haraka ya nini kuanza kupanda majukwaani na kuanza kuuza sera za CHADEMA. Kama akichomoa basi itakuwa tu ni huruma ya Tume, vinginevyo anachomolewa saa moja asubuhi.
Acheni kuweweseka basi Mataga, mlianza kuamini kuwa Lissu mmempiga risasi amekufa hakufa...

Mkaamini hawezi kurejea nchini kabla ya Uchaguzi akarudi

Mkaamini hawezi kuteuliwa na Chadema akateuliwa..

Mkaamini hawezi kupewa Form na Tume akapewa...

Mkaamini hawezi kupokelewa mikoani na wananchi, akapokelewa kwa maelfu..

Sasa mnaamini hawezi kuteuliwa na Tume, Ujinga tu unawasumbua...
Tamasha la Wasanii wa CCM Uwanja wa Uhuru ilikuwa ni kitu gani? Kampeni ama si kampeni?

Hofu ya nini bandugu???

Magu alipowaambia Wapentekoste wasimchague Lissu ilikuwa ni Kampeni ama si Kampeni?

Aliponunua Jogoo kwa sh. 100000 ilikuwa ni Kampeni ama si Kampeni?

Alipoahidi kupanua barabara ya Dumila baada ya kula mahindi ya kuchoma ilikuwa ni kitu gani anafanya?
 
Barbarosa,

Hakuna kitu kama hicho Tundu Lissu lazima agombee.

Mlisema hatakuja, kaja toka Belgium.

Mlisema msaliti hana mvuto wa kisiasa, imebainika siyo kweli.

Mlisema siku ya Sikukuu ya Nane Nane Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Dodoma itakuwa imefungwa, Tundu Lissu alikuta ipo wazi.

Mlisema hati yake ya Kiapo haitasainiwa na Jaji wa Mahakama Kuu Dar es Salaam , jana fomu zake za kiapo zimesainiwa.

Mmepanga kumuita Kisutu tarehe 26 August 2020, Tundu Lissu hawezi kutokea kwa udhuru wa jambo muhimu ktk mchakato wa kuelekea uchaguzi 2020.

Mnasema tarehe 26 August 2020 hatatambuliwa kama mgombea rasmi wa Urais kupitia CHADEMA 2020, Tundu Lissu atatambuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa na ndiyo itakuwa siku ya kusitisha tuhuma zote za mahakamani mpaka baada ya uchaguzi tarehe 28 Oktoba kumalizika.

Wagombea wanaotambuliwa na Tume ya Uchaguzi 26 Agosti tuhuma za mashtaka yao yatasitishwa kwa kinga maalum ili sisi waTanzania tuweze kushiriki kumpigia kura maana tuhuma ya kesi siyo kigezo cha kumuondolea haki yake kuchaguliwa kwani tuhuma siyo ukweli mpaka pale tu atakapo hukumiwa ndiyo sifa inakosekana.
 
We amini unachoamini na mwingine ataamini anachoamini na serikali itafanya inavyoona.
 

Kampeni ni kampeni na kutafuta wadhamini ni kutafuta wadhamini. Hivyo viwili ni tofauti.

Lissu alikuwa mfu aliyefufuka. Kila anapokwenda watu wana nia ya kumwona na kusalimiana naye.

Hiyo ndiyo tofauti kuu kati ya Lissu na wagombea wengine.

Membe anajizungumzia yeye kama mtu ambaye hakuwa mfu.

Suala la Lissu ni tofauti hayupo asiiyeijua tofauti hiyo.
 
We amini unachoamini na mwingine ataamini anachoamini na serikali itafanya inavyoona.

Hapo sio suala la kuamini au kutokuamini, bali ndio ukweli wenyewe.
 
hivi kwenye hiyo hoja ya kuanza kampeni mapema mnatumia nguvu nyingi sana kuitetea? two wrongs doesn't make right
 
hivi kwenye hiyo hoja ya kuanza kampeni mapema mnatumia nguvu nyingi sana kuitetea? two wrongs doesn't make right
Kipengere kitakachomtoa Lissu kama watamwekea pingamizi ni No. 16 kwenye orodha ya NEC ya Pingamizi. Lissu haruhusiwi kuwa Mbunge kwa muda wa miaka mitano na moja ya sharti la mgombea Urais lazima awe anauwezo wa kungombea ubunge!
 
Mwinyi alipopokelewa kama rais "mteule" haikuwa kuvunja kanuni eti?
 
Ni kweli kabisa, hiyo ni kwakuwa Magufuli anajua hawezi kushindana na Lisu, na namna pekee ni kuhakikisha hakutani naye.
Lissu kaoa lakini au unataka kuwa mke wa pili
 
CHADEMA wepesi sana mnakua kama hamzielewi siasa za bongo....uchaguzi uliopita mlimalizwa na Lowasa huu mtamalizwa na Membe
 

Acha nicheke kwa nguvu, nimehamasisha wasijiandikiahe kupiga kura kisha wakafika 29m+! Je nisingehasisha watu si wangefika 55m? Kuna maajabu gani boss, zaidi ya tabia binafsi za magu kwenye kunajisi chaguzi za nchi hii? Nikikuambia kuwa idadi ya 29m+ ni ya kupika, sikosei kwenye hilo. Sasa kama wapiga kura wako 29m+ kisha hawatakuta majina yao vituoni, kwanini mpike data kubwa hivyo mpaka mnaonekana majuha? Halafu kwa maelezo yako inaonyesha hamkubaliki, bali mnategemea figisu kushinda.
 
Membe ni transplant ya sisiem ! Kachero hawezi kuacha kuwa kachero!
 
Nilishasema humu kuwa huyu membe ni pandikizi huyu?
 
Membe ni mjinga hana nguvu yoyote wala ubavu wa kupata kura 100,000.
 
Upuuzi mtupu nani aliongea Zanzibar na kusema atawatoa mashehe wa uhamsho akichaguliwa kuwa Rais?

Wanatufanya watanzania wote wapumpavu kama wao.
Membe nilikuwa namuwaza lkn kuanzia sasa nimesham delete mawazoni mwangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…