Membe: Musiba na Mchange anayewatuma kunichafua kwanini hamnipeleki mahakamani? Kama mnaweza kunirekodi mmeshindwa nini kutoa huo ushahidi

Membe: Musiba na Mchange anayewatuma kunichafua kwanini hamnipeleki mahakamani? Kama mnaweza kunirekodi mmeshindwa nini kutoa huo ushahidi

Anaandika Bernard Membe.
Rondo- Lindi.

Sikuingia kwenye mitego yao hiyo. Mimi kama Watanzania wote wenye akili za kawaida nilishangazwa sana na ukimya wa Serikali huku damage na rumours zikiwa zimetanda kote nchini bila kuzitolea maelezo kwa siku 3 mfululizo! Mhe. Rais ni kiongozi wa Umma. Inapotokea sintofahamu au upotoshaji wowote ule, ulikuwa ni wajibu wa Msemaji wa Ikulu au wa Serikali kukanusha na kuweka mambo sawa kama wanavyofanya siku zote.

Vinginevyo wale wenye akili za mbilikimo na makuhani wa unafiki wanachukua mwanya huo kutunga ya kwao ili kumfurahisha Mhe. Rais.

Ben Membe.
Rondo- Lindi.View attachment 1241102View attachment 1241103
1.tunashukuru balozi na jasusi mbobezi mimi ninaona ni vyema ukaomba nafasi ya kutoa ushauri kwa hiyo idara husika ili habari zile zinatoka unavyoona wewe.
2.kuhusu haO wanafika aka zana za kilimo na group lake walikuwa wanatoa taarifa za uongo ili kumfrahisha Raisi?? Yaani Raisi anapenda habari za uongo na uzushi?? Basi naona 2020 uje wewe
 
Wewe membe,
Wenye akili tunaweza kuona mlinganisho wa maneno uliyoyatumia jinsi yanavyoshabihiana na yaliyotumika kwenye mitandao yenu na hiyo kigogo.

Kauli ni hizo hizo,halafu jazba ni hiyo hiyo,povu ni hilohilo,so pls usituyumbishe wananchi.
Wewe yumbayumba mwenyewe.

Halafu kumbe ulijichimbia huko mwezi mzima ok......tunaweza kuunganisha doti.

Kauli yako kwamba huwezi kutumia simu kwa sababu inadukuliwa,je kwa ujasusi wako mbobezi unataka kutuaminisha watanzania kwamba huwezi sajili simu au kutumia laptop ya mmojawapo wa hao au huyo uliemuajiri kukujenga mtandaoni.

Hivi kuna mahali uliandikiwa kwamba lazima uwe rais wa nchi hii.
Huwezi kujipima tu na kuona kwamba upepo uliishabadili mkondo?

Mbona mzee lowassa pamoja na kuwepo makubaliano na uncle wako lakini mlishindwa kumtimizia ahadi mpaka mbowe akalamba mshiko na kumuacha mzee hoi?

Au una uchungu wa yale mabegi ya hela yaliopotea kwa kubambwa pale dodoma?

Ila pia namalizia kwa kujiuliza hivi waraka huu ni wa kwako membe kweli?

Na kama ni wa kwako nauona umejaa hasira na visasi kupindukia,kiasi kwamba kama ungeupata urais basi nikikumbuka na lile onyo ulilowahi kulitoa la *maadui zako watafute pa kukimbilia basi napata picha ya kuogofya sana.
Najua matusi ya wafuasi wako lakini wacha nitukanwe ila nimesema ya moyoni na ni haki yangu kikatiba.
Ahsante na ninasimama na ...
JPM 2020 =2025 [emoji1241][emoji818]
 
Hivi Membe shida nini? unataka nini zaidi?

Nashauri utulie sometime kukaa kimya ni busara.

Acha kuuadaa Umma Ili upinzani waje 2020 wafanye kama walivyofanya 2015 kwa Lowassa
 
Sikubaliani na Membe.

Ilichokifanya serikali nadhani ndicho kilikuwa sahihi.

Kwamba, tetesi za kijuha na kipumbavu, ni vyema kuzipuuza kwa maneno lakini pia kuzijibu kwa vitendo ndani ya muda mzuri.

Rais kujitokeza na kuendelea kufanya kazi zake, lilikuwa ni jibu murua kabisa kwa majuha wote walioshiriki kutunga na kueneza uzushi wao.

Hivyo ndivyo inavyotakiwa.

Msemaji wa serikali akianza kujibu kila aina ya uzushi, kufanya hivyo ni kuubariki na kuuhalalisha uzushi huo. Serikali itafanya hivyo kwa mangapi? Maana uzushi na uongo ni sehemu kubwa sana ya hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga.

Safi sana serikali. Safari hii mmetenda vyema.
Binafsi sikubaliani nawe, serikali ina msemaji wake, rais kupitia ikulu wana msemaji.hivi serikali kutoa general statement kuhusu rais kuna tatizo gani? Kwani tetesi za kwenye mtandao si zinatolewa na RAIA pia? Kwa mtazamo wangu Msigwa hajawatendea haki watanzania Na hata rais mwenyewe aliyemteua.kwa mtazamo wangu alipaswa kuwajibishwa.
 
Serikali ilivyofanya ndiyo njia sahihi kabisa kwa mavuvuzela huoni sasa yanaona aibu sana tu mpaka yamekimbia kwenye mitandao nenda huko tweeter ukaone huyo kigogo wako alivyotukanwa matusi ya nguoni!!
 
Hivi Membe shida nini? unataka nini zaidi?

Nashauri utulie sometime kukaa kimya ni busara.

Acha kuuadaa Umma Ili upinzani waje 2020 wafanye kama walivyofanya 2015 kwa Lowassa
Mkuu una chuki na member, ana haki ya kujibu, kaguswa na Musiba
 
Serikali ilivyofanya ndiyo njia sahihi kabisa kwa mavuvuzela huoni sasa yanaona aibu sana tu mpaka yamekimbia kwenye mitandao nenda huko tweeter ukaone huyo kigogo wako alivyotukanwa matusi ya nguoni!!
Mkuu hapana, taharuki ilikuwa kubwa mno kwa sababu ya uzembe Wa Msigwa, kumbuka analipwa kwa ajili hiyo....kazi yake pia Ni kutoa ratiba ya rais na kuondoa hofu....Kwa mtazamo wangu Msigwa alipaswa kufukuzwa.
 
Binafsi sikubaliani nawe, serikali ina msemaji wake, rais kupitia ikulu wana msemaji.hivi serikali kutoa general statement kuhusu rais kuna tatizo gani? Kwani tetesi za kwenye mtandao si zinatolewa na RAIA pia? Kwa mtazamo wangu Msigwa hajawatendea haki watanzania Na hata rais mwenyewe aliyemteua.kwa mtazamo wangu alipaswa kuwajibishwa.

Sawa.

Huo ni mtazamo wako.

Kwa bahati mbaya, mtazamo wako haukuwa mtazamo wao, pia.
 
Membe haya anaytaka mwenyewe sio siri ,sijui anawashwa nini
Huyu mzee ana lake jambo. Alitaka serikali itolee ufafanuiz ujinga wa mtu mmoja tena wa kutunga? Rais kwani alipotea siku ngapi? Nawapongeza sana Ikulu kwa kumpuuza huyo mjinga. Kukanusha au kutoa ufafanuzi ingekuwa kama kuchezwa muziki na huyo mjinga. Membe ameandika haya kwa sababu anaona huyo Kigogo amedharaulika na hataaminika tena siku sijazo. Serikali ingejibu ujinga kama ule kesho angekuja na jingine. Walifanya vizuri sana kuendelea na shughuli zao bila kutetereka. Membe anataka kutuambia kuwa rais akiwa kwenye matatizo basi habari huwa inatolewa kwenye Internet tena na mtu anayetumia jina la bandia? Naona huenda na yeye alishatarisha suti zake lakini akapigwa na butwaa na aibu kubwa...
 
Mkuu hapana, taharuki ilikuwa kubwa mno kwa sababu ya uzembe Wa Msigwa, kumbuka analipwa kwa ajili hiyo....kazi yake pia Ni kutoa ratiba ya rais na kuondoa hofu....Kwa mtazamo wangu Msigwa alipaswa kufukuzwa.
Sema ilikuwa kwenye mitandao ya kijamii huko mitaani ilikuwa hata haijulikani mkuu.
 
Membe anaakili lkn hatoweza kumuwahi StoneCold Jomagu...bora apige tizi asizeeke ili agombeage 2025
 
Back
Top Bottom