Sikubaliani na Membe.
Ilichokifanya serikali nadhani ndicho kilikuwa sahihi.
Kwamba, tetesi za kijuha na kipumbavu, ni vyema kuzipuuza kwa maneno lakini pia kuzijibu kwa vitendo ndani ya muda mzuri.
Rais kujitokeza na kuendelea kufanya kazi zake, lilikuwa ni jibu murua kabisa kwa majuha wote walioshiriki kutunga na kueneza uzushi wao.
Hivyo ndivyo inavyotakiwa.
Msemaji wa serikali akianza kujibu kila aina ya uzushi, kufanya hivyo ni kuubariki na kuuhalalisha uzushi huo. Serikali itafanya hivyo kwa mangapi? Maana uzushi na uongo ni sehemu kubwa sana ya hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga.
Safi sana serikali. Safari hii mmetenda vyema.