Membe: Musiba na Mchange anayewatuma kunichafua kwanini hamnipeleki mahakamani? Kama mnaweza kunirekodi mmeshindwa nini kutoa huo ushahidi

Membe: Musiba na Mchange anayewatuma kunichafua kwanini hamnipeleki mahakamani? Kama mnaweza kunirekodi mmeshindwa nini kutoa huo ushahidi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Anaandika Bernard Membe.
Rondo- Lindi.

Watanzania Wenzangu! Nawasalimia! Kwa siku tatu mfululizo magazeti ya makuhani wa fitina na unafiki Musiba na Mchange na wenzao wamekuwa wakinishambulia kwa uchochezi wa sintofahamu iliyotokea kuanzia Alhamisi tarehe 17 Octoba siku ambayo Mhe Rais ameondoka Lindi kuelekea Dar hadi Jumapili ya tarehe 20. Mimi nipo Kijijini kwangu Rondo kwa mwezi mmoja sasa.

Ni nini hicho nilichokisema au kukiandika kwenye mitandao ya kijamii? Kwa kuwa mawasiliano yangu yote nayafanya kwa simu yangu ambayo inasikilizwa na kudukuliwa, naviomba vyombo vinavyohusika vitoe hadharani mazungumzo na maandishi yangu ili watu wasikie, wasome na wanihukumu. Napenda niuhakikishie umma kuwa Mimi sikuwa mjinga! Nilijua kuwa nikisema au kuandika vibaya, wabaya wangu wataninyooshea vidole.

Sikuingia kwenye mitego yao hiyo. Mimi kama Watanzania wote wenye akili za kawaida nilishangazwa sana na ukimya wa Serikali huku damage na rumours zikiwa zimetanda kote nchini bila kuzitolea maelezo kwa siku 3 mfululizo! Mhe. Rais ni kiongozi wa Umma. Inapotokea sintofahamu au upotoshaji wowote ule, ulikuwa ni wajibu wa Msemaji wa Ikulu au wa Serikali kukanusha na kuweka mambo sawa kama wanavyofanya siku zote.

Vinginevyo wale wenye akili za mbilikimo na makuhani wa unafiki wanachukua mwanya huo kutunga ya kwao ili kumfurahisha Mhe. Rais. Good governance requires quick response to rumours. Rumours left unattended damages governance! Narudia! Naviomba vyombo husika vitoe hadharani nilichokisema au kupost kwenye mitandao ili nihukumiwe na Wananchi wenyewe na sio na Wabwekaji wa Taifa.

Ben Membe.
Rondo- Lindi.
FB_IMG_1571754042448.jpg
FB_IMG_1571740676421.jpg
 
Sikubaliani na Membe.

Ilichokifanya serikali nadhani ndicho kilikuwa sahihi.

Kwamba, tetesi za kijuha na kipumbavu, ni vyema kuzipuuza kwa maneno lakini pia kuzijibu kwa vitendo ndani ya muda mzuri.

Rais kujitokeza na kuendelea kufanya kazi zake, lilikuwa ni jibu murua kabisa kwa majuha wote walioshiriki kutunga na kueneza uzushi wao.

Hivyo ndivyo inavyotakiwa.

Msemaji wa serikali akianza kujibu kila aina ya uzushi, kufanya hivyo ni kuubariki na kuuhalalisha uzushi huo. Serikali itafanya hivyo kwa mangapi? Maana uzushi na uongo ni sehemu kubwa sana ya hii mitandao ya kueneza na kujazana ujinga.

Safi sana serikali. Safari hii mmetenda vyema.
 
Haahaa dunia kweli duara, aliyekuwa waziri Wa mambo ya nje Leo analalamika kama sie RAIA.hili Ni somo kwa waliopo madarakani Leo wasidhani watadumu mamlakani milele.Ila membe kwa misemo hatari, eti wabwekaji Wa taifa.
 
Back
Top Bottom