Membe: Sijaumbwa kuwa Rais wala sina tamaa ya Urais, mimi sitaki nionekane kibwengo

Membe: Sijaumbwa kuwa Rais wala sina tamaa ya Urais, mimi sitaki nionekane kibwengo

Aliyekuwa Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo Bernard Membe amesema amejaribu kwa wakati kugombea Urais na sasa wakati hauko upande wake tena hivyo anawatia moyo vijana kugombea.

Membe amesema yeye hana tamaa na wala hajazaliwa ili awe Rais ndio maana anabakia kuwa mshauri. Ni fisi tu ndiye mwenye tamaa lakini hana mikakati ndio maana tamaa yake inamponzaga hivyo mikakati ikifika mwisho na bado ukawa una tamaa basi utaonekana ni kibwengo.

Membe amewataka vijana wanaotaka kugombea Urais waanze maandalizi mapema lakini wawe waangalifu sana wasije wakafukuzwa kama yeye.

Chanzo: Clouds TV

Maendeleo hayana vyama!
Member ana maneno mengi yasiyo na tija.
Si akae kimya tu?
U steringi hauwezi!
 
Huyu ni kachero aliyefeli mission ya kuibomoa Chadema, karudi kwa mwajiri wake kichwa chini baada ya Kamanda Mbowe kumpa za uso
 
Membe alikuwa overrated. Pongezi kwa Ben Mkapa (RIP) na wale wote waliohakikisha hawi Rais mwaka 2015. Ingekuwa disaster kubwa zaidi

Kwa kuwa technically ACT walishamfukuza kabla hata kura moja haijapigwa, anasubiri nini kurudi CCM?
 
Kapata akili sasa ee?

Membe alikuwa anashabikiwa na kundi dogo sana tena mitandaoni tu.

Chaajabu na yeye akawa kama Lisu akalewa sifa kwamba anakubalika sana.
Nilikua nawaambia wapambe wake ,wakawa wabishi
 
Membe alikuwa overrated. Pongezi kwa Ben Mkapa (RIP) na wale wote waliohakikisha hawi Rais mwaka 2015. Ingekuwa disaster kubwa zaidi

Kwa kuwa technically ACT walishamfukuza kabla hata kura moja haijapigwa, anasubiri nini kurudi CCM?
Sasa namuamini Musiba
 
Bora akili yake imemrudia sasa
Membe ana courage lakini hakujipanga mapema,kwenda upinzani.
Hata pale alipopewa uwanja akajikuta amebanwa na viongozi wake,wakimkana kwenye majukwaa ya kampeni.
Lakini alipata kura nyingi kiasi bila kupiga kampeni.
 
Huyu jamaa Bado nazn hajui anatak nn au sisi ndio Hatujui Lengo lake.
 
Binafsi huwa napata wakati mgumu kumuelewa MEMBE, hana kanuni kama mawimbi yanayo tokana na Tsunami - leo hii atakwambia yeye ana sifa zilizo pitiliza kuwania kiti cha Urais, kesho anakwambia msiniulize maswali mengi nakwenda kwenye Hoteli ya kifahari na mama watoto kula chakula kizuri, kesho kutwa anasema mtu anayetaka kuwaniani Urais anakuwa driven na tamaa ya fisi - sasa tuchukulie lipi tuache lipi - simusemi vibaya lakini wakati mwingine mtu unabaki unajiuliza maswali mengi hivi
huyu mwenzetu aliwezaje kuongoza Wizara ya mambo ya nje kwa term mbili!! Je,kama agefanikiwa kushinda kiti cha Urais Tanzania ingekuwa katika hali gani?
That why wanamuita Jasusi mbobezi
 
Back
Top Bottom