Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Ila pamoja na yote jamaa hana msimamo kweli na mkakati mzito na ana watu nyuma isije akawa kama ya Nape nnauye alifukuzwa uanachama ccm ila mwisho akarudishwa na kikwete kuwa alionewa.
 
CCM bana vichwa vyote wapigania kampeni karibia wote wamewatoa ktk serekali bado sijaona mbadala Tanga Januari makamba, Singida Mwigulu, kusini Nape, Membe, na wakuunganisha na busara mzee Kinana.
 
Mungu alishaamua kuwa nchi hii ataiongoza Bernard Membe. Mtaweweseka lakini hamtaweza kubadili chochote. Membe is there na atawanyoosha atakaposhika hatamu.
 
Kuna mtu anaandaa mazingira ya kuwekwa kizuizini atakapoachishwa madaraka. Tusubiri tutashuhudia kwa macho yetu ya nyama
 
Sioni tofauti ya Membe kuachia jimbo la Mtama, Emmanuel Nchimbi kuachia jimbo na Regina Lowassa baada ya uchaguzi CHADEMA walipompa ubunge wa viti maalum alipowaambia hiyo nafasi anastahili mtu mwingine sio yeye. Kuna watu washashiba.

Kama ni uraisi huyo Lowassa wakati kama huu 2015 alishaanza na ziara rasmi za kuonyesha nia, alikuwa ni rich backers na wapambe kibao wa wazi kama Nchimbi wenye jukumu ku-mobilise support ya ndani tena hapo nafasi ilikuwa inaenda kuwa wazi maana raisi alikuwa anamaliza muda wake.

Sasa how on earth Membe ambae mpaka sasa udhani kama kuna jitihada zozote za kushawishi humo ndani angeweza msumbua Magu.

Kama ni mkakakati wa mtu mmoja basi ni sawa na upuuzi tu na kama ni mkakati wa wengi wako wapi watu wake na sidhani kama leo angekuwa anatimuliwa pekee.

Kuna watu washashiba Membe mwenyewe baada ya kustaafu anazungukia vogue toleo jipya kufukuzwa CCM ambayo aimlipi pension ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu tu.

The only motive behind this ni kwamba CCM is cooking something I don’t know what.
 
Mwamba wa pande za Kusi, mwanadiplomasia nguli Bernard Membe ameunguruma baada ya kutoswa na CC ya CCM.

Ngoma bado mbichi kabisa hii.

Kwa undani zaidi, jipatie nakala yako ya "The Citizen" hapo kesho Jumamosi 29 February.

View attachment 1372047,
Wacha wafyekane hawa wote ni waovu tu ndio wametifikisha hapa kama nchi. Akina kinana na Makamba waliozoea kuwaandikia makalipio makali wenzao. Sasa kibao kimegeuka. Ni namna fulani ya fundisho kabla hawajafa.
 
Back
Top Bottom