Membe: Sikushangazwa kufukuzwa. Niliendelea kusimamia nia yangu kugombea Urais 2020. Mwenyekiti na Katibu wameratibu mimi kufukuzwa

Mag3,
Hongera kwa post yako hiyo.

Kama swala ni kuhesabu kura za ushindi, Membe hana kura ndani ya CCM tena kwa vile kama nilivyosema kwenye post hiyo, wajumbe wengi wa CCM waliopo leo sio wale waliokuwa upande wa Membe wakati ule; hilo ni swala la wazi kabisa.

Kinachotokea ni kwa Membe kutaka kuweka mvurugano ndani ya CCM kwa njia ya makundi kusudi aendele kuwa relevant. Makundi ya kisiasa ndani ya chama chochote siyo mazuri hasa wakati wa Uchaguzi hata kama yanahusisha kikundi kidogo sana. Kikwete aliliona hilo wakati wa kmuhula wake wa kwanza ndiyo maana akaja naa sera za kujivua gamba.

Swala la tetesi litabaki kuwa tetesi tu; mimi sikuwamo kwenye kikao hivcho kwa hiyo sijui ni wajumbe gani wengi walipinga uamuzi, ila la muhimu ni kuwa uamuzi wa kikao ulipita. Iwapo angekuwa na wajumbe wengi, ni wazi kuwa hapo ndipo ilikuwa sehemu nzuri ya kuonyesha kuwa hawataki afukuzwe kusudi waje wamchague wakati wa Uchaguzi ujao.
 
Sheria za wapi mazee? Ona kumbe hata huelewi unachozungumzia. Ni hivi: bila Chama kumpitisha mgombea tume ya uchaguzi hawezi kwenda kuchukua fomu. Hatua ya kwanza ni kuchuukuwa fomu ya chama... upo?

Unaongea nini ww mtoto? Hapa tunazungumzia kuchukua fomu ya kugombea rais ngazi ya taifa au kuchukua fomu ili kupitishwa na chama Kwanza? Halafu ww dogo ukae kwa kutulia maana hapa unachanganya mada tu.
 
Kichuguu,
Hakuna mwanachama yoyote wa ccm sasa hivi ana ubavu wa kupinga atakacho mwenyekiti, hata wajumbe wangepinga bado uamuzi wake ndio ungekuwa wa mwisho.

Kumbuka nguvu yake huko ccm ni kupitia kofia ya urais, na hiyo kofia ya urais ndio nguvu halisi ya ccm. Iwapo ataamua kuifumbua macho ccm automatically itakufanya.
 
Hivi kweli Membe anaamini alikuwa tishio kwa JPM ndani ya CCM?

He can’t be serious.

Siyo Membe aliyeamini kuwa yeye ni tishio bali jpm ndiye anamuona ni tishio kwake. Vinginevyo angeachwa ajionee mwenyewe. Kwa hali ya kisiasa iliyopo sasa mtu yeyote ndani ya ccm mwenye nia ya kugombea urais ni tishio.
 

Kama ni hivyo, basi hata kwenye uchaguzi wa mgombea ingekuwa ni hivyo tu. Lakini kabla sijafunga post nikufahamishe tena kuwa list ile ya wajumbe ina wafuasi wengi wa Magufuli kuliko wanaompinga; huo ndio ukweli mchungu ambao Membe anatakiwa akubaliane nao. Ile riporti ya uhakiki wa mali za CCM ilisababisha wapinzani wengi wa Magufuli wapukutike na hivyo kumfanya ajisimike zaidi kwenye mafiga ya CCM
 
JokaKuu,
Ni ishara ya kuwa na mpangilio kuliko kumuacha mtu mmoja anakuja na ya kwake. Ana papala ndo maana alijikuta anamshindwa mgonjwa Lowasa. Kiundani Membe anadhani ni super, brainy, kumbe hovyo tu! Hana landmark yoyote ktk uwaziri wake.
 
Siasa sio rahisi namna hiyo!


Katika uchaguzi za kisiasa hupaswi kabisa kumdharau mpinzani wako.

Pamoja na sifa zote alizonazo JPM hana uhakika kwenye uchaguzi wa ndani ya chama chake kama atashinda.

Alichofanya Jpm kumchinjia mbali Membe ni hesabu sahihi kabisa kwake kama mwanasiasa ingawa inaweza ikawa si sahihi kwa wanademokrasia na wapenda usawa.

Katika miaka minne ya uenyekiti wake ametengeneza labda maadui wengi wa kisiasa kuliko marafiki, kama angemruhusu Membe agombee nae asingekuwa na uhakika wa nafasi ya kateuliwa. Hii ni kanuni ya siasa si yangu.

Wenda siku ya uchaguzi upepo ukavuma upande wa Membe kutoka kwa wajumbe na yeye Mwenyekiti wa sasa kutupiliwa mbali.


Hili Jpm analijua vzr tu ndio maana anataka ajihakikishie kateuliwa pekeyako pasipo hatari ya kuruhusu mgombea mwingine.


Yeye mwenyewe ni mnufaika wa jambo kama hili katika uchaguzi wa ndani ya chama mwaka2015.
 
Kichuguu,
utasemaje mtu analeta mvurugano wakati anatumia haki yake kikatiba?Membe ni mwanachama,haridhishwi na kinachoendelea chamani,na lipo kundi linaamini kama yeye,na katiba ya chama kwa kutambua hilo iko wazi kuruhusu challenge,sasa mtu akichallenge mnasemaje analeta mgawanyiko?

kwani mgawanyiko dhambi?si ndio demokrasia?mnataka muwe pamoja hata kama baadhi yenu hawaridhiki, je,huo si udikteta? hivi mifumo ya uongozi ya nchi hii najiuliza ikitokea kuna kiongozi mbaya hafai,na ndani ya system kajaza watu wake wa kumsapoti katika namna ambayo haitakuwa rahisi wananchi kuwategemea hao kumuwajibisha anapokosea,lakini tayari ana madaraka, mnaweza kumbadili kweli?maana naona mko tayari kuua chama na nchi kuliko kufanya mabadiliko pale inapobidi.Ni uoga tu wa kuweka precedence itakayokuwa mwiba kwenu hata baadae,maana hakutakuwa na ujinga tena kama hili likiruhusiwa.

And this goes down the roots of african culture.Mkubwa anavuruga familia lakini members wa family hakuna wa kunyooshea kidole,kisa ni baba,babu,mjomba etc.Tutabaki nyuma hadi hizi akili za kichizi zituondoke kwanza.
 
Wanasema huyu jamaa alikuwa Shushushu mkubwa? He is not to be trusted.
 
BADO MMOJA,
Umeandika kweli tupu lakini ishu ya BM imeonyesha picha halisi ya ccm ambayo kila siku wanaipinga kuwa kwao hakuna udikteta, wanajidai ndani ya chama hakuna udikteta kumbe upo, kumfukuza mtu kisa ameonyesha nia ya kuchuana na mwenyekiti.
 
Haaaa!!
Eti kutokana na nia ya kutaka kupambana na mwenyekiti wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…