Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Mag3,
Hongera kwa post yako hiyo.
Kama swala ni kuhesabu kura za ushindi, Membe hana kura ndani ya CCM tena kwa vile kama nilivyosema kwenye post hiyo, wajumbe wengi wa CCM waliopo leo sio wale waliokuwa upande wa Membe wakati ule; hilo ni swala la wazi kabisa.
Kinachotokea ni kwa Membe kutaka kuweka mvurugano ndani ya CCM kwa njia ya makundi kusudi aendele kuwa relevant. Makundi ya kisiasa ndani ya chama chochote siyo mazuri hasa wakati wa Uchaguzi hata kama yanahusisha kikundi kidogo sana. Kikwete aliliona hilo wakati wa kmuhula wake wa kwanza ndiyo maana akaja naa sera za kujivua gamba.
Swala la tetesi litabaki kuwa tetesi tu; mimi sikuwamo kwenye kikao hivcho kwa hiyo sijui ni wajumbe gani wengi walipinga uamuzi, ila la muhimu ni kuwa uamuzi wa kikao ulipita. Iwapo angekuwa na wajumbe wengi, ni wazi kuwa hapo ndipo ilikuwa sehemu nzuri ya kuonyesha kuwa hawataki afukuzwe kusudi waje wamchague wakati wa Uchaguzi ujao.