Member wa JamiiForums mpo wapi?

Member wa JamiiForums mpo wapi?

Ila hii ni kweli.. nimeshawahi kuwaona wawili tu, aliyenishawishi kuingia na mdada mmoja mzuri mzuri niliyemuona akiitumia katika daladala mwanza...

Wengine wote ni kuishtukia ID, unakuja kumuuliza in real life na inakuwa kweli
 
Kuna dada moja nilipanda nae daradara toka mwanza town kwenda igombe to Kayenze

Alikuwa amekaa siti moja na jamaa fulani hivi akawa anamuelezea jinsi mtandao wa jamiiforum ulivyo

Yule dada nilivyomuona na alivyokuwa anaelezea atakuwa ni member maarufu sana majukwaani maana anajua mpaka usiri wa members na pm zao.

Nilihisi alikuwa ni Evalyn Salt
 
Nishawahi kuwaona mara kadhaa.
1. Nilipanda basi la mkoani pembeni alikaa mdada wa makamo alikuwa anacheki jamii forums uzi wa tunda la kimasihara.
2. Nishawahi kupanda bajaji ya kuchangia pembeni alikuwepo jamaa kanyoa ndevu staili ya O yupo anacheki jamiiforums.
3. Nimewahi kupanda mwendokasi kuna mtu mzima anabonge moja la para alikuwa anaperuzi JF.
4. Nilikuwa nakarabati pc ya mpenzi wa bro wa rafiki yangu kwenye history nilikuta hiyo pc anazurura nayo jf.


Kwenye daladala kama watatu, mmoja ni Mwanamke mtu mzima. Na wawili ni wanaume wa kama miaka 50.

NB: Mimi nina macho ya haraka sana. Nikisimama nikishika bomba nikisimama nyuma naona kila kitu.
 
Sisi wakulima huwa hatuna stress kabisa kwani tunapost tukiwa mashambani huko tukipalilia majaruba ya mpunga.
 
Kuna wengine wanayo tu ila sio members wa jf yani hawajajiunga ni wapenzi watazamaji tu, kama mimi nilivyo kaa nayo kwenye simu yangu kwa muda wa zaidi ya miaka sita bila kujiunga na kipindi hicho nilikuwa naifungua popote pale bila kujali.
Sawa
 
mi bi mkubwa yupo humu sana ila sidhani kama ana id au siijui labda. mwengine ni mfanyakazi mwenzangu nilienda mezani kwake nikakuta jf page na id inaonekana ila ni wale member wakimya hawajulikani sana. kwenye mabus humo sijawahi ona ila nimeona id kadhaa twitter sasa sijui ni wale wale au majina tu watu wamecopy hadi avatar.
 
Back
Top Bottom