Member wa JF huwa mnajificha wapi mnapo tumia JamiiForums.!??

Member wa JF huwa mnajificha wapi mnapo tumia JamiiForums.!??

Hawa wengine mbona kama watu wasiojulikana vile?
 
Mi nikiwa kwenye daladala nikitaka kuperuzi JF huwa naificha simu kwenye blauzi huku najisomea, watu wa kwenye daladala vimeo tupu

[emoji23][emoji23][emoji23] shida hiyo yote ya nn mkuu
 
me waifu wangu anajua tu nikiwa bize na pc anajua tayari natupia mavitu JF,ila hajui hata ID yangu
Wee dont underestimate us.. Ni ma fbi wazuri tu siku atakushangaza.. Namuonaga tu wangu anavyojisifu siijui id yake. Kumbe najua id yake hadi password. Password ya tigo na mpesa. Pattern na password ya simu niko vzr namcheki tu nasubir siku antibue...
 
Mi niko highway ya arusha Moshi naendesha na huku na chat kwa kujiiba natokea Moshi naenda Njiro we ukow api
 
Nipo kwenye mwendokas sa hiz njoo uone navyokujib huu uzi wako
 
Hahahahaha lol! Mnoko huyu alikuwa busy kutaka kujua ID yako.
Mnoko sana. Anachungulia kweli kweli. Sasa kisogoni nikawa nahisi kuna mtu ananikaribia sana kwa muda mrefu.

Nilipogeuka, Jamaa bado tu linakodolea macho kwenye simu. Hahaha!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Habari zenu wadau wa JF.?

Naam wadau kama nilivyo andika hapo juu. Napenda kujua hiv nyie wanajukwaa huwa mnatumia huu mtandao wa JF mkiwa maficho gani maana sijawahi kutana wala kuona ata member mmoja akitumia JF hadharani.

Mfano ukiwa kwenye Daladala watu kutumia mitandao kama vile Facebook, Instagram, Twitter, WhatsApp n.k ni jambo la kawaida ila sasa shughuli inakuja kwenye mtandao wa JF. Yaani sijawahi ona wala kukuta mtu anatumia JF hadharani.

Tatizo ni nn wakuu mnaogopa ama ni nn.???
Wewe huwa unatumia hadharani? Watu huwa tunatumia ila huwezi kutuona
 
Mi nipo hapa magogoni,karibu kabisa na mlango anapoingilia Mkuu wa Kaya au Baba Jesca, karibuni tuonane hapa hahaha
 
Kuna workmate mmoja alinikuta natumia paaap mimi siogopagi akaniuliza huu mtandao gani nikamwambia JF.

Mbona kila nikikuona unautumia unacheka saana nikamwambia kuna raha na karaha humu ingia ujionee.

Haya nifungulie account.. nikamwelekeza nikampa na sheria za mchezo akaanza kujiachia alivyozoea akaniuliza wewe ndiye nanii? Nikamwambia hapana mimi ni Saint Ivuga[emoji23] [emoji23] sijui kama ivuga hakuwahi kumtumia text. [Basi leo umenijua ila tuhifadhiane wote watu wazima]
 
Umenikumbusha kitu,.kuna siku nilikuwa muhimbili hospital nipo katika kumsubiri daktari akaja kaka wa makamo hivi akaa pembeni yangu,muda si punde akatoa simu yake na moja kwa moja akafungua JF na kuanza kutupia comments zake,. Nilijaribu saana ku zoom jicho langu angalau nimfahamu kwanza halafu ndio nimsalimie na kumwambia kuwa na mm ni member wa JF..hahahah nilishindwa aiseee.....but mm natumia popote isipokuwa kwenye sehemu zenye purukushani.
 
Watz wamezoea mitandào ya mapicha picha, udaku na umbea. If iko tofauti, ni mtandao wa kusoma kutafakari na kuelewa. Watz wengi ukitaka uvunje uhusiano nao weka maandishi mengi yanayotakiwa kusomwa kwa umakini, utaona wanavyokimbia.
 
Kuna workmate mmoja alinikuta natumia paaap mimi siogopagi akaniuliza huu mtandao gani nikamwambia JF.

Mbona kila nikikuona unautumia unacheka saana nikamwambia kuna raha na karaha humu ingia ujionee.

Haya nifungulie account.. nikamwelekeza nikampa na sheria za mchezo akaanza kujiachia alivyozoea akaniuliza wewe ndiye nanii? Nikamwambia hapana mimi ni Saint Ivuga[emoji23] [emoji23] sijui kama ivuga hakuwahi kumtumia text. [Basi leo umenijua ila tuhifadhiane wote watu wazima]
Ukaamua kumpa kesi ivuga. We Daby na ivuga ndio watu wa kwanza kuwafaham nilivyo jiunga humu. Unakumbuka ule mkono wako
 
Ukaamua kumpa kesi ivuga. We Daby na ivuga ndio watu wa kwanza kuwafaham nilivyo jiunga humu. Unakumbuka ule mkono wako
Nakumbuka aseeh... Sasa hivi mkoloni kabana akirudi tutaanza.
 
Mie popote pale ila nikiwa na ndugu, jamaa na marafiki sipendi kuingia huku ili wasijue ID yangu humu. Siku moja nilishangaa kujua ndugu wengi wamo humu na baadhi yao ni MACCM ya kutupa lakini hayamfagilii uchwara. Siku hiyo walikuwa wakijadili mijadala mbali mbali ya humu.
Takbiiir...!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna Siku nilimwona mdada mmoja kwenye daladala anafungua jf nkawa namchungulia nmwone atalog in na id gan bahat yake alijificha na kava la simu nisione
 
Back
Top Bottom