Mimi ni moja ya watu wanaopenda sana kufatilia reaction katika mabandiko ya watu,huwa nikiona post imepata likes nyingi na kati ya hizo likes kuna ka dislike kamoja huwa napenda sana kujua ni nani huyo alie dislike post iliyopokea likes zaidi ya 100.
nikishamjua muhusika basi wala sina la kumfanya huwa napenda tu kumjua muhusika inatosha,kadhalika nikiona mtu ka comment au kaanzisha uzi uko very serious halafu nakutana na ka reaction cha kucheka,huwa lazima niguse kugundua huyu aliecheka ni nani wakati mtu kaandika kitu serious namna hiii.
sasa katika kagua kagua zangu kuna member wawili ndani ya JF sio kwamba nawafatilia ila nakutana nao sana kwenye reaction za kicheko,huwa nikiona post ina likes 30 halafu kuna ki emoj cha [emoji23] au cha [emoji1787] huwa tayari nakua najua hizo emoj zimetoka kwa watu gani,maana wao ndio wacheka cheka humu JF.
Nadhani bandama zao zina fanya kazi vizuri,kuna wakwanza anajiita carleen huyu kaweka dp ya mdada wa bongo movie sijui,huyu member bwana anapenda kucheka sio kidogo ila ninachompendea huyu yeye anacheka panapostahili kucheka nadhani ni moja ya watu wenye raha sana,kuwa na huyu mtu nadhani ticket ya kwanza inabdi uwe mchekeshaji.
Lakini kuna member mwingine ambae sijawahi kuelewa kwanini anacheka cheka,yani kuna muda react emoj ya kicheko kwenye post iko very serios yeye huyo unamuona kacheka yani nashndwaga elewa huyu member n mwezi mchanga au huwa inatokea tu na yeye ana raha sana,yani mtu anaweza fungua thread akaomba ushauri wa dawa ya kutibu TUMBO kwenye comment akatokea mtu akashauri, "nenda katumie flagile na unywe maji mengi" akija huyu member utamuona ana tupia reaction ya [emoji1787] yani ananiboaga kisengerema hajui tu,sasa ana cheka nini hapo?
Au mtu anaweza akafungua thread akaomba msaada wa TV nzuri,kwenye comment mtu akamshauri "nenda katafute tv inaitwa sony huwa ni nzuri sana" akija huyu member akiona hiyo comment utamuona anatupia [emoji23] basi natamani angekua karibu nimuulize hivi brooo unacheka cheka nini? huwezi kujikaza wewe?
Member huyo si mwingine ni jamaa anaitwa extrovert we jamaa najua ukiona hii post utacheka kama kawaida ako,bahati nzuri member wapenda kucheka ninaowajua 1 ni me 1 ni ke hawa naamini wanaweza tengeneza couple nzuri sana mjini maana wao kucheka ndio kitu wanazingatia ktk maisha yao,sema extrovert maswala yako ya kucheka cheka kwenye viitu serious uache unazingua halafu mpk nahisi kuna watu unawaboa sema ndio hivyo hujui tu.Badilika ILA kwa dada carleen wewe mama kula maisha endelea kukenua kwa raha zako.