Members wenzangu niliowatapeli humu JF nisameheni leo natubu

Members wenzangu niliowatapeli humu JF nisameheni leo natubu

Wakuu salaam.

Baada ya salamu naomba kusema kwamba maisha yana Mambo mengi,, wakati mwingine unaweza fanya mambo kinyume kabisa na Tabia yako.

Ipo hivi,. Miaka michache iliyopita kipindi cha utawala wa JPM Mambo yaliniwia ugum Sana , yaani moja ilikuwa haikai wala mbili haisomeki.

Siku moja nilijikuta katika hali ngum zaidi kipesa nikawa sina namna nyingine bali kutumia mbinu ya ziada.

Nikapata wazo Kwa kuwa Watanzania wengi tunapenda Sana ngono basi naweza nikaitumia hii kama fursa.

Nikaanzisha Thread kwamba Mimi nipo Dar na kazi yangu ni udalali WA madem, hivyo Kama unahitaji dem mkali na mbichi njoo PM lakin malipo Kwanza then nakuunganisha nae. PM ikafurika vijana wa hovyo

Ukweli ni kwamba nilikuwa sijawahi hata kufika Dar nilikuwa mkoani Chaka Ila nilichokuwa na kifanya ni kuwa ukija PM na ukikamilisha malipo Mimi nakutumia namba ya Malaya wa Hitwe uhangaike naye.

Hela kweli nilipata Ila najiona sikuwa muungwana.
Aisee😀
 
Ndo wewe ulinitapeli elf 5 nikalala njaa?

OK nimekusamehe mkuu lakin naomba tuonane nikuongezee elfu 20 lakini sharti tuonane nikupe hiyo hela mkononi maana we ni muungwana sana
 
😂 Dalali nafsi imekusuta kweli au ni mbinu nyingine hiz unafanya
 
Back
Top Bottom