RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
Mhadhara - 45:
Right Marker
Dar es salaam.
Asilimia kubwa ya MEME zinazosambaa kwenye MITANDAO YA KIJAMII na kupostiwa na watu kwenye STATUS UPDATES zinaandikwa na watu (vijana) wenye fikra finyu na wasiojitambua.
Unapaswa kufahamu kwamba hakuna changamoto yoyote inayotatuliwa kwa kutumia MEME. Kila changamoto inayokukumba kwenye maisha inahitaji juhudi zako kwa vitendo.
Siku hizi mtu akivurugwa kidogo kwenye jambo fulani anatafuta MEME inayofanana na jambo husika kisha anapost. Hebu jaribu kupost MEME zinazoendana na umri wako, heshima yako, cheo chako, utu wako, kazi yako, n.k
ZINGATIA:
1. Kama umemkosea mtu muombe msamaha. Acha utoto wa kupost MEME ambayo inatetea ujinga wako ukidhani kuwa utaonekana mwamba.
2. Kama umeachika kwenye mahusiano, ndoa yako inasumbua, umetoa au umepewa talaka - jaribu kuwa mtulivu na mvumilivu huku ukizidi kulinda heshima yako. Acha utoto wa kupost MEME inayofanana na tukio ulilopigwa kwenye mahusiano ukidhani kuwa unajifariji, kumbe unajichoresha kwa watu ambao walikuwa hawana habari yoyote.
3. Kama humpendi achana nae tafuta ustaarabu mwingine, au baki mkimya. Acha utoto wa kupost MEME za kejeli kwa mwenzako, MEME ambazo zimeandikwa na watu wenye fikra finyu tena wasiojua maisha.
4. Kama umeingia kwenye ugomvi wa kfamilia, au ugomvi wa majirani; hebu jaribu kutafuta njia za kumaliza ugomvi wenu. Wewe ni mtu mzima, acha utoto wa kupost MEME zilizoandikwa na wavulana na mabinti wanaobalehe ambazo hazitosuluhisha ugomvi zaidi ya kuchochea moto.