Mende anaogopesha jamani, acha tu...

Mende anaogopesha jamani, acha tu...

Mende na kunguni ni wadudu ambao hata kuwaona spendi, ukitaka siku yangu iende vibaya bas nionyeshe mende na kunguni...hao wadudu Wana sura mbaya achilia mbali kutia kinyaa
mi nikisema naonekana mwanaume wa dar

huo ndio ukweli,hivi vidudu vinatisha

na ni vichafu in nature,stakagi hata vinipitie karibu
 
Leo mida flani nilikua kazini ghafla nikaskia haja yani hadi nikahisi naweza Jinyea leo

Nikakimbia choo cha ofisini RRRRR nasukuma ndani mtu akakohoa

Nikasema leo ndio leo Nafwaaa

Haya toka speeeed sana hadi nnje vuka barabara kuna LODGE opposite nikaenda straight

Maana najua vyoo vya hapo vilipo

Kufika sukuma mlango Umefungwa shika kitasa kigumu

Mdada mmoja akaniambia "Mlango umefungwa kaka" kachukue funguo kaunta

Naenda kaunta sikuti mtu aiseeeeeeeeeee (acheni kabisa bandugu)

Kimbia kimbia zile nikaponea Choo cha BAR moja hivi ipo kule mbele mbele

Kadri ninavyokaribia chooni ndio huku nyuma mzigo kama unasukumwa uje mzima mzima

Nashukuru mungu kufika eneo la tukio (chooni) nikakuta pako wazi nikazama funga mlango chuchumaaa (nikawa napata burdaniiiiii)

Nikiwa kwenye starehe yangu si akatokea mshua MENDE sijui alitokea wapi nikamsikia anapanda kwenye vidole daaaah

Si unajua nilivaa sendo Nikaskia kitu kinapita kwenye vidole vya miguuu,Kucheki hivi Kiruuuuu Jamaaa bonge la MENDEEE

asee niliruka juuuu nikasema kama noma na iwe noma Huyu mende sio wa kawaida

Basi nkachukua mop nikampga akakufa,nikarudi kuburudika

Mende acheni jamani...mwaka 2019 nadhani leo ndio namuona mende tangu mwaka uanze

anatisha kabisa,siwacheki tena wale wakuitwa Wanaume wa DAR

Halafu utasikia mtu anasema hawa wadudu wanaliwa watamuuuu...AAAAAH nife njaaa tu kwakweli
View attachment 1218220
Bwana vichekesho
 
Kwa uoga ulio nao unatakiwa kuwa kaburin ukiwa umeisha kufa, hata Mwenyezi Mungu anachukia sana watu waoga
 
Kwa uoga ulio nao unatakiwa kuwa kaburin ukiwa umeisha kufa, hata Mwenyezi Mungu anachukia sana watu waoga
ila mimi Mungu hanichukii,anaelewa situation ilonkuta pale toilet

anajua ujasiri wangu vizuri tu
 
Miaka ya nyuma nikiwa kinda mmoja wa baba zangu wadogo alikuwa muoga sana wa mende kiasi alikuwa anatoka jasho na moyo unaenda mbio mende akikatiza,wazee wakakaa chini wakamuoza mke sijui ule uoga wa mende ulienda wapi!
 
Miaka ya nyuma nikiwa kinda mmoja wa baba zangu wadogo alikuwa muoga sana wa mende kiasi alikuwa anatoka jasho na moyo unaenda mbio mende akikatiza,wazee wakakaa chini wakamuoza mke sijui ule uoga wa mende ulienda wapi!
anao hadi kesho

hawa viumbe sio kwamba nawaogopa ila ni sababu ni wachafu

Hapo tu ndio wanaponichefua
 
Lol! Nimechekaje 😀 Mi nyoka tu simuogopi, kama haruki naweza muua pekeyangu sembuse mende.
 
Back
Top Bottom