Beki wa zamani wa Manchester City Benjamin Mendy anasema alikopeshwa pesa na wachezaji wenzake wakati huo Raheem Sterling, Bernardo Silva na Riyad Mahrez wakati klabu hiyo ilipoacha kumlipa baada ya kushtakiwa kwa ubakaji na unyanyasaji wa kingono, aliiambia mahakama ya ajira.
Beki huyo wa Ufaransa anadai mshahara wa £11.5m ambao haukulipwa tangu aliposhtakiwa Agosti 2021 na kusimamishwa bila malipo na City.
Mendy, 30, aliondolewa mashtaka mwaka wa 2023 dhidi ya msururu wa mashtaka ya ubakaji na kujaribu kubaka.
Klabu hiyo iliendelea kumlipa Mendy baada ya kukamatwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 2020, lakini walidai kuwa hawakulazimika kufanya hivyo baada ya kushtakiwa kwa kuwa masharti yake ya dhamana, moja wapo yalimzuia kwenda karibu na uwanja wa klabu au uwanja wa mazoezi na shirikisho la soka lilimaanisha kuwa kwa kusimamishwa kwake asingeweza kutekeleza majukumu yake ya kimkataba.
Nyaraka za mahakama zilisema Mendy "aliishiwa pesa haraka sana" na ilimbidi kuuza jumba lake la kifahari la Cheshire ili kulipia ada za kisheria za kesi, malipo ya matumizi na matunzo ya watoto baada ya kuzuiliwa kwa mshahara wake.
"Raheem Sterling, Bernardo Silva na Riyad Mahrez wote walinikopesha pesa ili kunisaidia kujaribu kulipa ada yangu ya kesi na kusaidia familia yangu," Mendy alisema katika taarifa yake ya shahidi.
Mnamo Novemba 2022, Mendy alituma ujumbe wa Whatsapp kwa Omar Berrada, ambaye alikuwa afisa mkuu wa uendeshaji wa kandanda wa City kuanzia Septemba 2020 hadi Julai 2024, kuuliza ni lini atapokea mishahara yake isiyolipwa lakini hakujibiwa.
Source: BBC Swahili
Soma pia:

View attachment 2673981
Mwanasoka wa Manchester City, Benjamin Mendy (28) anatuhumiwa kwa kosa la kumbaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka 28 na kumwambia msichana huyo “ni sawa, kwani ameshafanya ngono na wanawake 10,000”.
Mendy anatuhumiwa kumshambulia mwanamke huyo, wakiwa kwenye jumba lake la kifahari huko Mottram St Andrew, Cheshire, Oktoba 2020.
Aidha anatuhumiwa kwa jaribio la kumbaka msichana mwingine, mwenye umri wa miaka 29 ambaye pia alimshambulia nyumbani kwake miaka miwili iliyopita.
Baada ya kusomewa mashtaka yote mawili katika Mahakama ya Chester na Jaji Stephen Everett, mwanasoka huyo alikanusha kuwa hakufanya makosa hayo.
Chanzo: Wasafi TV
Mahakama imetoa hukumu leo kuhusu kesi ya udhalilishaji wa ngono ambao mchezaji wa zamani wa Manchester City, Benjamin Mendy anahusishwa kufanya na wanawake nchini Uingereza.
Mahakama imemkuta Benjamin Mendy kutokuwa na hatia yoyote na hivyo kumuachia huru mchezaji huyu wa Ufaransa.
Mchezaji huyo ameishukuru Mahakama kwa kufanya kazi kubwa kufatilia ushahidi wa matukio haya badala ya kusikiliza uzushi unaoibuliwa na wanawake hao ambao inasemekana alifanya kitendo hicho mwaka 2020, akishtakiwa kuwabaka wanawake wawili, mmoja akiwa na miaka 24 na mwingine akiwa na miaka 29.