Mendy asema alikopeshwa pesa na wachezaji wenzake wa zamani wa Manchester City

Omukisa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
642
Reaction score
1,305
Beki wa zamani wa Manchester City Benjamin Mendy anasema alikopeshwa pesa na wachezaji wenzake wakati huo Raheem Sterling, Bernardo Silva na Riyad Mahrez wakati klabu hiyo ilipoacha kumlipa baada ya kushtakiwa kwa ubakaji na unyanyasaji wa kingono, aliiambia mahakama ya ajira.

Beki huyo wa Ufaransa anadai mshahara wa £11.5m ambao haukulipwa tangu aliposhtakiwa Agosti 2021 na kusimamishwa bila malipo na City.

Mendy, 30, aliondolewa mashtaka mwaka wa 2023 dhidi ya msururu wa mashtaka ya ubakaji na kujaribu kubaka.

Klabu hiyo iliendelea kumlipa Mendy baada ya kukamatwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 2020, lakini walidai kuwa hawakulazimika kufanya hivyo baada ya kushtakiwa kwa kuwa masharti yake ya dhamana, moja wapo yalimzuia kwenda karibu na uwanja wa klabu au uwanja wa mazoezi na shirikisho la soka lilimaanisha kuwa kwa kusimamishwa kwake asingeweza kutekeleza majukumu yake ya kimkataba.

Nyaraka za mahakama zilisema Mendy "aliishiwa pesa haraka sana" na ilimbidi kuuza jumba lake la kifahari la Cheshire ili kulipia ada za kisheria za kesi, malipo ya matumizi na matunzo ya watoto baada ya kuzuiliwa kwa mshahara wake.

"Raheem Sterling, Bernardo Silva na Riyad Mahrez wote walinikopesha pesa ili kunisaidia kujaribu kulipa ada yangu ya kesi na kusaidia familia yangu," Mendy alisema katika taarifa yake ya shahidi.

Mnamo Novemba 2022, Mendy alituma ujumbe wa Whatsapp kwa Omar Berrada, ambaye alikuwa afisa mkuu wa uendeshaji wa kandanda wa City kuanzia Septemba 2020 hadi Julai 2024, kuuliza ni lini atapokea mishahara yake isiyolipwa lakini hakujibiwa.

Source: BBC Swahili

Soma pia:

 
Mimi kama mendy tuu, boss akisitisha kunilipa.
Lazima nitawakopa wafanyakazi wenzangu.

Tatizo mimi sina nyumba ya kuuza, labda niuze TV.
 
Madem wa kizungu ni hatarii!
Muulize Eboue..
Wanatunzwa na kulelewa kwa ajili ya kuwawinda professional football players tu! Hasa Wakiafrika!
 
Madem wa kizungu ni hatarii!
Muulize Eboue..
Wanatunzwa na kulelewa kwa ajili ya kuwawinda professional football players tu! Hasa Wakiafrika!
Wanakuja kimkakati kwa mgongo wa mapenzi.
 
Madem wa kizungu ni hatarii!
Muulize Eboue..
Wanatunzwa na kulelewa kwa ajili ya kuwawinda professional football players tu! Hasa Wakiafrika!
Kama alijichanganya akaforce kupewa mzigo huo ni ushamba wake.
hata hawa wachezaji nao ni binadamu wana makosa pia.
Sio kila kesi wanawindwa.

Refer kesi ya Mason Greenwood.
 
Kama alijichanganya akaforce kupewa mzigo huo ni ushamba wake.
hata hawa wachezaji nao ni binadamu wana makosa pia.
Sio kila kesi wanawindwa.

Refer kesi ya Mason Greenwood.
Unachosema ni kweli lakini pia wanawake kuja kimkakati kwa watu maarufu ni kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…