Meneja kivuko cha Busisi-Kigongo, nakuburuza Mahakamani. Hii kero imekuwa sugu!

Meneja kivuko cha Busisi-Kigongo, nakuburuza Mahakamani. Hii kero imekuwa sugu!

Gati za pande zote mbili kwenye ardhi imekuwa ni kero ya muda mrefu sana kwa magari ya chini (saloon cars).

Hiki kivuko ukiwa unaingiza gari au ukiwa unashuka, ni lazima ukwangue bampa la mbele la gari. Hata uwe makini namna gani kukwepa, lazima uburuze bampa!

Mark X ya jamaa yangu ishawahi kutoka bampa lote la mbele upande wa Kigongo ikiwa inashuka kutoka ndani ya kivuko!

Last week nimeshuhudia Subaru Impreza inang'oka bampa hapo hapo.

Nimeazima Crown la watu kwenda Sengerema, wakati naingia kwenye kivuko, bampa limesaga ardhi! Wakati nashuka kwenye kivuko bampa la mbele limeacha rangi yote pale! Nimeumia mnoo, gharama kureplace rangi crown la watu.

Nina hasira sana na uongozi wa hiki kivuko. Hivi hamuoni wateja wenu wa magari ya chini wanavyoumiza magari yao hapo? Wenye magari ya chini wanalalamika sana mrefu ila mmeziba masikio na mnakusanya tu tozo!

Hivyo vituta vya ardhi pale kivuko kinapogota mmekosa kabisa akili ya kuvithibiti ardhi ikawa flat?

Mnatucharge TSH 6,500 kwa gari ndogo, na baada ya hapo mtu afikie kwenda gereji kurekebisha bampa!

Tumechoka na kero hii!

Wewe Meneja wa kivuko cha Busisi-Kigongo, jiandae kisaikolojia.

Very soon tunakutumbua kisha nakuburuza Mahakamani. Lazima ulipe fidia kwa hizi hasara nilizoingia kwasababu ya uongozi wako wa kizembe hapo kivukoni.

Mapato makubwa ya kivuko lakini mnashindwa kutatua kero ndogo ndogo zinazoumiza wateja wenu. Hamfai kukalia hivyo viti.

Nimemaliza. Hopefully message sent and delivered.
Simple mkuu. Usitumie hicho kivuko zunguka Shinyanga, kahama, ushirombo, Lunzewe, Geita kisha Sengerema. Utarudisha gari la kuazima likiwa kama ulivyoliazima.
 
Hiki kivuko ukiwa unaingiza gari au ukiwa unashuka, ni lazima ukwangue bampa la mbele la gari. Hata uwe makini namna gani kukwepa, lazima uburuze bampa!

Mark X ya jamaa yangu ishawahi kutoka bampa lote la mbele upande wa Kigongo ikiwa inashuka kutoka ndani ya kivuko!

Last week nimeshuhudia Subaru Impreza inang'oka bampa hapo hapo.

Nimeazima Crown la watu kwenda Sengerema, wakati naingia kwenye kivuko, bampa limesaga ardhi! Wakati nashuka kwenye kivuko bampa la mbele limeacha rangi yote pale! Nimeumia mnoo, gharama kureplace rangi crown la watu.

Wenzetu ughaibuni wanajitahidi sana kufanya mazingira kuwa user friendly lakini huku kwetu tunafanya kinyume chake tunafurahia majanga wanayopata wadau, usishangae hapo huyo kiongozi anafurahia kuwa amefanya kazi yake vizuri kwakuwa watu wana suffer
 
Back
Top Bottom