Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kutoa malalamiko kuwa kuna changamoto ya maji ndani ya Stendi ya Mabasi ya Magufuli (Magufuli Bus Terminal) kwa siku mbili Agosti 28 na 29, 2024, ufafanuzi umetolewa.
Kusoma alichokiandika Mdau bonyeza hapa ~ Stendi ya Mbezi Magufuli hakuna maji siku ya pili leo
Uongozi wa Bagufuli Terminal na Halamshauri ya Ubungo umetoa ufafanuzi na kueleza kilichotokea pamoja na mipango yao:
UFAFANUZI WA MENEJA WA MAGUFULI TERMINAL
Meneja wa Stendi hiyo ya Mabasi, Isihaka Waziri anasema:
Sisi tunatumia huduma ya DAWASA, maji yalikatika Saa Nne Asubuhi jana (Agosti 28, 2024), sisi tulikuwa na hakiba ambayo inatufikisha Saa sita usiku.
Hakukuwa na tangazo lolote kutoka DAWASA kuwa huduma haitakuwepo, kama kungekuwa na tangazo shida ya upungufu wa maji (katika Kituo cha Magufuli) isingekuwepo.
Baada ya maji kutotoka hadi Saa nane Usiku ndipo tukaagiza maji kwenye maboza, nao walipoenda kutafuta maji kwenye vioski hawakupata kwa kuwa hayakuwepo, wakaanga kuhangaika kutafuta kwenye visima hali iliyochukua muda mrefu, wakafanikiwa kupata asubuhi Saa tatu na sasa maji yapo kwenye Vyoo na sehemu nyingine.
Sasa hivi DAWASA ndio wametoa taarifa kuwa huduma ya maji itakosekana kwenye maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.
Kawaida DAWASA wakitupa taarifa mapema, nasi tunajiandaa mapema kwa ajili ya kujaza maji ya akiba.
MAELEZO YA HALMASHAURI YA UBUNGO
Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Joina Nzali anasema:
Wananchi wanatamani tuchimbe kisima ili tuwe na maji mengi zaidi ya akiba, utaratibu kisima kipo cha akiba, kinatumiwa inapotokea kuna tangazo la DAWASA kuwa maji yatakatika.
Kisima hicho cha akiba kinaweza kutumika kwa Saa 72 au inapotokea ni wakati wa high season inaweza kuwa Saa 48.
Tukipewa taarifa mapema huwa tunaagiza maji mapema kwenye maboza ili kutumika.
Jambo lingine ni kuwa tulipanga kuchimba visima zaidi lakini Wataalam walipopima wakasema eneo hilo la Stendi tukijimba visima maji hayatafaa kutumiwa na Binadamu.
Manispaa tukafikiria kuchumba visima tuvune maji ya mvua, pale kuna matenki 11 ya Lita 10,000 ambayo yanaweza kutumika kama akiba pia. Hivyo kama tutavuna maji ya mvua inaweza kuwa njia nzuri ya kupunguza changamoto.
Kwa tukio la jana na leo (Agosti 28 na 29, 2024) DAWASA hawakutoa taarifa ndio maana ikatokea changamoto hiyo, tunafahamu umuhimu wa huduma ya maji ilivyo muhimu eneo hilo kuliko hata huduma ya kununua pipi.
Pia soma;
~ Maji yamerejea Stendi ya Magufuli punde baada ya JamiiForums kutoa taarifa ya kukosekana
~ Pwani na Dar wapata Upungufu wa Maji kutokana na hitilafu ya Umeme Mtambo wa Ruvu Juu