Meneja wa Tarura mkoa wa Mwanza na mhasibu wake wamekuwa watu wa ovyo kwenye majukumu yao.
Hawa watu wawili wanaifanya Tarura Mwanza iwe sehemu ya hovyo sana kwa sababu wana madudu mengi. Wanashirikiana kuiba fedha za serikali kwa kigezo cha meneja huyo kuwa na ukaribu na mtendaji mkuu Eng Victor H Seif, hivyo hizo fedha zote wanazochukua kutoka account ya Tarura Imprest wanampelekea mtendaji mkuu.
Vitendo vyao vya kupiga fedha ya serikali vimeanzia kwenye kujiandikia posho za kazi hewa wao wenyewe kwa kigezo cha fedha hizo kupelekwa kwa mtendaji mkuu, ila watumishi wanaotakiwa kulipwa posho za kazi mbalimbali wanaambiwa fedha hakuna ila wao na watumishi wengine wa idara ya uhasibu wakihitaji fedha zipatikana.
Meneja huyo amekuwa akimsikiza mhasibu tu na sio mtu mwingine hali inayopelekea mameneja wa wilaya kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa kukosa fedha za kununulia mahitaji yao kama mafuta,shajala na vifaa vingine. Hii inatokana na fedha walizozitenga kukosekana bila kujua fedha hizo zimeenda wapi na wakiuliza wanajibiwa kuwa ni fedha za accounting officer(meneja mkoa) hivyo ana mamlaka yote ya kutumia fedha atakavyo. Mameneja wa wilaya wamekuwa ni watu wa kuomba omba hususani wilaya ya ukerewe. Tangu mwaka wa fedha 2023/2024 uanze hadi umeisha hajawahi kununuliwa shajala kabisa na kuishia kuomba wilaya jirani.
Fedha zao zinachukuliwa bila wao kupewa taarifa na wakihoji sana meneja na mhasibu wanawatishia watawafanyia uhamiasho kwani wana mawasiliano ya karibu sana na mtendaji mkuu hivyo ni vitendo cha dakika tu. Mameneja wilayani wanavilio kuwa fedha zao za vifungu kutumika ndivyo sivyo kwa amri ya meneja akishirikiana na mhasibu. Kazi za wilayani hazifanyiki na mara nyingine kuchelewa kwa sababu ukosefu wa fedha.
Aidha meneja amekuwa akijinadi mara kadhaa kuwa yeye kwenye uongozi wake anataka kufanya kazi na watu majambazi kama mhasibu wamekuwa wakichukua fedha nyingi za serikali kwa matumizi yao binafsi na mara nyingine kusema fedha zinaenda kwa mtendaji mkuu dodoma makao makuu ya Tarura.
Wawili hao pia wamekuwa wanashirikiana kuwalazimisha wakandari watoe fedha kwa nguvu mara baada tu ya malipo,wakandarasi wakigomaa kutoa rushwa hizo wanawatishia kuwa malipo yao mengine yatachelewa kutoka hadi watoe hizo fedha na wamekuwa wanahitaji asilimia kadhaa kwenye kila malipo.
Mbaya zaidi wana mpango wa kuhama ofisi ya sasa iliopo Isamilo na kuhamia capri point kwenye gharama kubwa za pango na ofisi hizo hazina hadhi ya kiwango hicho. Ofisi za sasa zinalipiwa mil 14 kwa mwaka na wanahamia ofisi za mil 36 mara 2 ya gharama za ofisi za awali. Fedha hizo za ziada za kulipa pango zinatoka kwenye kifungu cha posho ambacho watumishi wanatakiwa kulipwa ikiwa ni malipo ya muda wa masaa ya ziada ya kwenda wilayani kufanya kazi. Ofisi zenyewe hazina mazingira rafiki kwa watumishi kwanza ni ndogo ikiwemo na ufinyu wa vyumba ambao utapelekea watumishi wengine kukaa kwenye Kontena.
Madirisha ni madogo hayapitishi hewa vizuri. Vyumba havina mwanga wa kutosha na vyoo vyake sio salama kwa matumizi ya watumishi wote pia dosari nyingine nyingi ambazo zinahitaji marekebisho kupelekea gharama kuongezeka. OSHA waliangalie hili suala vizuri.
Watumishi Tarura Mwanza wamechoshwa na vitendo hivyo vya meneja mkoa na mhasibu wake. Wamekuwa wanaripoti kwa mtendaji mkuu lakini hakuna jambo lolote linalofanyika. Taarifa hii iwafikie viongozi wa Tarura makao makuu Dodoma na TAMISEMI kuwa meneja mkoa na mhasibu wake wachukuliwe hatua maana wanaichafua Mwanza kwa utendaji wao mbovu wa kazi.
Hii ni moja ya baadhi ya wizi unaofanywa na meneja na mhasibu. Watumishi hapo wamelipwa nusu ya fedha walizoandikiwa. Zilizobakia zinaenda kwa mtendaji mkuu na kuna baadhi ya watumishi hapo hawahusiki kabisa na zoezi hilo.
====
Pia soma: Katavi: Ubovu wa barabara katika Manispaa ya Mpanda, TARURA yanyooshewa kidole