Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Screenshot 2024-07-02 193402.png

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
 
Kama aina hii ya watu ndio Watumishi wa Umma tena wenye dhamana kubwa,unategemea Kodi ya Wananchi itakuwa salama?
---
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo.

Mutegeki amekamatwa na nyara hizo za Serikali wilaya ya Kibondo Julai 2,2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya tembo kutoka wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.

Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mauaji ya tembo katika misitu na hifadhi zilizopo katika wilaya ya Kibondo na Kakonko.

Taarifa kutoka wilayani humo inaonyesha kuwa kuna jitihada za kuficha suala hilo kwa kutengenezwa mazingira ya rushwa ili kulimaliza jambo hilo ambalo ni uhujumu uchumi.

My Take
Sitaki kuamini kama wenye pesa Huwa wanafungwa,Wacha tuone.
 

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo...
Aisee! Tuseme kwamba mshahara anaopata pamoja na marupurupu ya Cheo Cha Umeneja wa TRA havitoshelezi mahitaji yake ya msingi ya kiuchumi? Is it??

Ama kweli kwamba Ufisadi ni tabia, Wala siyo kwa sababu ya kipato kidogo kisichokidhi mahitaji.
 
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2,2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
 
Back
Top Bottom