Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Siku hizi TRA hakuna maokoto ya kutosha mpaka viongozi mnafanya biashara haramu?

top level manager kabisa, umezingua sana
District manager, labda kama waliuboresha muundo kilikuwa ni cheo cha usimamizi tu kisichokuwa na maana yeyote ile.

Pole kwa afisa tozo wa wilaya. Ila waliimchoma Mungu anawaona 😀
 
Hivi hizi ni tamaa, ujasiri wa kipumbavu, au kitu gani?

Meneja wa TRA kabisa unafanya huo upimbi? Mimi pamoja na kazi yangu ambayo ni almost sawa na ujobless siwezi kufanya huo upumbavu.
 
Hii biashara za mihogo ina mambo mengi,ukiletewa mezani
Mipesa yake inatamanisha sana
Ni biashara unayotakiwa kuwa na mtandao mpana
Longtime sana,ndy nakutana na malkia wa pembe za ndovu hotelini kwake pale beijing opp na shoppers plaza
Pale si kulikuwa na wageni wengi kutoka China wanafikia,kumbe yule mama alikuwa anaona sana pilika zangu nkiingia pale kuwafTa wageni wangu wachina....ananisoma tu....
Sasa kuna siku yule mama akaniita akasema nna maongezi na wewe,tukapanga siku ya meeting pale ....
Siku naonana naye sasa akaanza kuniambia ebwana ehh yule mama alikuwa anajuwa kila kitu nachofanya na wale wachina 😄
Yule mama wa kichina naye,baada ya kuona pilika zangu na ufaster wangu kwa wale wageni wa kichina akavutiwa na mm sasa,kukawa na ukaribu
Yule mama alikuwa anajuwa dili bana Ana michakato kibaooo
Hawa sjui wakubwa marpc polisi anaongea wakat wowote
Sasa kuna siku hyo aliinita akaniambia kwake watakuja wageni kutoka China na nia yao waende kongo wakanunue dhahabu na wanakuja na mshiko mkubwa,sasa yeye anasema wakifika anataka kuwapiga helaa
😄 nakumbuka issue ilisikilizwaa lakini mwisho wa siku wale wageni kutoka China hawajaja kwake walionganisha juu kwa juu 😄
Yule mama alilaani sana akasema hawa walisoma nyakati
Sasa tukawa una ukaribu fulani akiwa na issue tunaongea,nakumbuka wakat balloon gari zinatoka alinunua alikaa nayo wiki tu akaibiwa,polisi wana haha kumpigia masimu wamsaidie kuitafuta mama anasemaa achaneni nayoo tu
😄
Sasa kuna siku nmekaa naye ndy akawa ananielezea kuhusu biashara ya pombe za ndovu na kama alitaka kuniingiza,nkasema hapana hii issue syo badaye huwa inabuma,sema kama mtu wa tamaa na hujuwi kucaLculate
Risk ....unapoteaaa

Ova
Aisee.. wachina ndio wafanyabiashara wazuri wa hizi kitu.. 😅
 

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Mwamba kachomwaaa
Kajaaa kwenye mfumooooo
 
Huyo Manager ilitakiwa aje afuzu Chuo hapa Johannesburg hizo mambo za watu wakitaka uondoke angeelewa mapema sana maana alikua kikwazo kwenye dili za watu watu wanakupa dili na Mteja wa kutengeneza na pesa unalipwa baadae unaambiwa fata ingine sasa kwa kuwa ishu ya mwanzo ilikua ya kugawana mpunga inabidi afanye peke yake akiamini yupo salama kumbe anaenda kukamatwa hakuna bisahara haramu inafanyika na mtu mmoja hakuna...
 
Ila wanawake mnaombaga tu hela wanaume...laiti mngejua hustle lake!!?

Dah! Died trying
 

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Kama hakuwaonea huruma tembo wasiokuwa na hatia, alikuwa akizionea huruma Kodi za Watanzania?
 
Back
Top Bottom