Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Yani kama ndo hivi basi mimi nitakufa masikini.Yani meneja TRA kabisaaa,wakati mimi nikipata nafasi hii nitakuwa mwadilifu sanaaaa.

Huyu kijana atakuwa ni tajiri sana sana,maana huku TRA anapiga huku meno daaah.
Ni njaa gu inakufanya uamini ukiwa mfanyakazi utakuwa mwadilifu ila ukweli ni kwqmba kila Mtanzania anaajiriwa kwa lengo la kuiba
 
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya Tembo.

Mutegeki Bagasheki amekamatwa na nyara hizo za Serikali Wilaya ya Kibondo Julai 2, 2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya Tembo kutoka Wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.
Dah huyu ni kijana mdogo sana na huwezi kumzania kwa mda niliowahi kukutana nae kibondo dah ni mtu poa sana sana nazani pia kachomwa na walikua wana mfuatilia bila yy kujua dah!pole yake
 
Kama aina hii ya watu ndio Watumishi wa Umma tena wenye dhamana kubwa,unategemea Kodi ya Wananchi itakuwa salama?
---
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo.

Mutegeki amekamatwa na nyara hizo za Serikali wilaya ya Kibondo Julai 2,2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya tembo kutoka wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.

Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mauaji ya tembo katika misitu na hifadhi zilizopo katika wilaya ya Kibondo na Kakonko.

Taarifa kutoka wilayani humo inaonyesha kuwa kuna jitihada za kuficha suala hilo kwa kutengenezwa mazingira ya rushwa ili kulimaliza jambo hilo ambalo ni uhujumu uchumi.

My Take
Sitaki kuamini kama wenye pesa Huwa wanafungwa,Wacha tuone.
Bora Yusuph Mwenda kateuliwa kuwa kamishna haya yote yataisha.
 
Sasa huko kibondo kuna mapato gani hadi dili likubali?
Kibondo hakuna udhibiti, hakuna usimamizi imara kwani haijulikani mamlaka za utawala ziko wapi kati ya Burundi Rwanda na Tanzania.... Ndio maana watumishi na mamlaka zake wako huru kufanya watakalo.
Huyo meneja TRA na wengine wengi wanajali na kuendesha miradi yao binafsi kwa mtaji wa Serikali kuu. Haishangazi sana hii kwa sababu ndio chanzo cha wilaya hiyo kongwe kubaki nyuma kimaendeleo. 🧐 🙄
 
Unaweza ukahisi watu wako smart kumkamata kumbe utakuta alikuwa Akila hatoi zaka Kwa wadau. Watu wakachomoa nyaya
 
kama uchunguzi utafanyika vizuri..watakamatwa wengi. huyo Manager wa TRA hayupo peke yake kwenye hiyo biashara haramu.
Viongozi wakikamatwa na uhalifu huwa natamani adhabu yao iwe kunyongwa
 
Inawezekana, una maana alifilisika? Maana alikuwa tajiri mkubwa Burundi. Siku hizo Bakhresa bado anauza viatu mtaa wa Uhuru.

imi nafahamu kaka wa mchambuzi ni yule Captain wa ndege aliyeshikwa na Dhahabu, enzi za Mrema alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
Sina uhakika kama alifilisika ama la, kwa sababu sijui background yake. Kikubwa ana biashara zake zinaendelea pale Mabamba Kibondo. Kumiliki matingatinga ya kujenga barabara si mtaji mdogo. Mpaka nilijiuliza, mtu wa kipato kile anawezaje kukaa kijijini Mabamba na aache kukaa mjini Kigoma, ama basi Kibondo mjini? Lazima kuna magumashi ana deal nayo.
 
Kama aina hii ya watu ndio Watumishi wa Umma tena wenye dhamana kubwa,unategemea Kodi ya Wananchi itakuwa salama?
---
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma linamshikilia Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wilayani humo Irving Mutegeki kwa tuhuma za kukutwa na meno ya tembo.

Mutegeki amekamatwa na nyara hizo za Serikali wilaya ya Kibondo Julai 2,2024 akiwa kwenye gari binafsi majira ya usiku na anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Meneja huyo wa TRA anadaiwa amekuwa akifanya biashara ya meno ya tembo kutoka wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwemo Burundi.

Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mauaji ya tembo katika misitu na hifadhi zilizopo katika wilaya ya Kibondo na Kakonko.

Taarifa kutoka wilayani humo inaonyesha kuwa kuna jitihada za kuficha suala hilo kwa kutengenezwa mazingira ya rushwa ili kulimaliza jambo hilo ambalo ni uhujumu uchumi.

My Take
Sitaki kuamini kama wenye pesa Huwa wanafungwa,Wacha tuone.
"Kama aina hii ya watu ndio Watumishi wa Umma tena wenye dhamana kubwa,unategemea Kodi ya Wananchi itakuwa salama?", huo ndio urefu wa kamba yake, lakini ujue zipo nyingine za elastiki yaani zinavutika, huyu alitumia ya elastiki.
 
Wazaramo wanasema usilonge ukamala, i.e. usiongee ukamaliza kila kitu. Unaweza kuta huyu meneja kazuia deal za watu pale TRA Kibondo, wakaamua wale naye sahani moja kwa kumpakazia meno ya tembo. Hii wilaya ipo mpakani mwa Burundi na Tanzania (just 30 kilometres kutoka Kibondo mjini mpaka Mukarazi mpakani mwa Burundi na Tz) Hakuna linaloshindikana hapa duniani, hasa kama unaingilia deals za watu.
 
Back
Top Bottom