Meneja wa TRA Kibondo akamatwa na meno ya tembo

Jamaa wakiamua kumlinda watamlinda wakitaka, ila wakiamua kumtoa sadaka pia wanaweza.

Kama kina Bashe waliotupiga zaidi ya huyo bado wako salama mpaka leo, huyo mjasiriamali nae anaweza kupona akiwa na connection.

Lakini kama hana connection, ndio "sheria itachukua mkondo wake".
 
Nchi hii bila magumashi huwezi kuwa tajiri. Hongera kwake mpambanaji, get rich or die trying.
Akipata dhamana hapo akimbilie kwa mganga huko huko Kigoma kesi inayeyuka kama hewa hiyo. Tangu lini Jamhuri ikawa na mawakili imara kushinda kesi.
 
Hadi kukamatwa plus huo muonekano wake (alivyochakazwa) vyote vinaashiria kwamba alikuwa na visa na hao Polisi, akawa anaminya deals zao na Polisi wakawa wanamtafuta wamminye mahala.
Tukija kustuka tutakuta hata hayo meno ya Tembo walimchomekea kwenye gari
 
Aisee! Tuseme kwamba mshahara anaopata pamoja na marupurupu ya Cheo Cha Umeneja wa TRA havitoshelezi mahitaji yake ya msingi ya kiuchumi? Is it??

Ama kweli kwamba Ufisadi ni tabia, Wala siyo kwa sababu ya kipato kidogo kisichokidhi mahitaji.
Hii nchi imekuwa ya hovyo, mtu anayelipwa milioni 3 kwa mwezi gross anakatwa kodi karibia laki 6 na ushee.....wakati wafanya biashara wakubwa wenye mitaji ya milion 50 na zaidi hawalipi kodi ipasavyo. Serikali inawabana sana watumishi private na public kwa kodi kubwa ya PAYE. Na ndio kodi wanayoitegemea sana.
Bora kutafuta suluhu mtaani. Mwamba kapambana.
 
Aisee! Tuseme kwamba mshahara anaopata pamoja na marupurupu ya Cheo Cha Umeneja wa TRA havitoshelezi mahitaji yake ya msingi ya kiuchumi? Is it??

Ama kweli kwamba Ufisadi ni tabia, Wala siyo kwa sababu ya kipato kidogo kisichokidhi mahitaji.
Vijana wa ovyo ndo hawa sasa wanataka mafanikio ya haraka haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…