zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Habari za asbuhi wana jukwaa moja kwa moja niende kwenye mada husika.
UTANGULIZI
Mfalme menelik II a.k.a Dagmawi sahle maryam menelik alikuwa mtawala wa Ethiopia kati ya 1889 hadi 1913 ambapo alianza kama mtawala wa eneo la shewa kuanzia 1866-1889. Alizaliwa mwaka 1844 na kufariki mwaka 1913 na inaelezwa alitoka kizazi cha uzao wa Queen of sheba (Makeda) na Mfalme suleiman. Menelik II alikuwa na uwezo wa kuongea lugha 7 ikiwemo kiingereza,kifaransa na kiitalia pia inaelezwa alikuwa msomi wa masuala ya usimamizi wa fedha(Finance) na ndio maana aliweza kuwekeza kwenye hati fungani huko marekani na kuwekeza kwenye migodi ya wabelgiji. Pia katika utawala wake alikuwa kwenye ndoa mara 3 ingawa hakuwahi kupata mtoto kwenye ndoa zote tatu lakini alizaa watoto nje ya ndoa na wote walikuwa mabinti.
UMAARUFU WAKE
Mfalme Menelik I anakumbukwa zaidi kwa kupambana na ukoloni wa kizungu katika nchi yake ambapo toka ashike madaraka mpaka anaondoka wazungu walishindwa kabisa kuitawala Ethiopia maana kila wakijaribu walikutana na nchi yenye dola kamili na kujitambua hta wakashindwa kujipenyeza na walipojaribu kuvamia walikutana na kipigo kikali. Pia menelik II anakumbukwa kwa kuitanua ethiopia hata kufikia mipaka kama iliokuwa nayo ufalme wa kush wa zamani uliofahamika kama Axum/Aksum.
VITA YA ADOWA
Kati ya mambo makubwa anayokumbukwa Menelik II ni vita ya Adowa ambapo Italia ilipokuwa amekuja Afrika kuchukua makoloni baada ya mikutano ya Berlin aliiteka somalia na Eritrea na hivyo alitaka na kuiteka Ethiopia ili kupanua utawala wake Afrika.
Italia ikaandaa Jeshi la watu 18,000 viliojipanga kwa brigedi 3 huku Ethiopia ikiwa na wanajeshi wenye uweledi,mafunzo na nidhamu zaidi ya 70,000 na viliongezeka hadi 120,000 vikiongozwa na ma Ras mbalimbali akiwemo mwanamama shujaa Taytu Betul ambaye aliongoza vikosi vya kutoka kaskazini akisaidiwa na kina Ras Makonnen na wengineo.
Usiku wa February 29 1896 vikosi vya Italia viliingia ndani ya Ethiopia katika eneo la Adowa hivyo waethiopia walipopata taarifa wakawazingira milimani wakiwasubiri kuwapa kipigo cha mbwa koko!!!
Brigedi ya Albretone kilikuwa cha kwanza kushambulia ila kilikutana na mizinga ya kutoka urusi iliotumiwa na jeshi la Ethiopia iliowadhoofisha sana na hata msaada ulipotoka kwa brigedi zingine za Italia chini ya Arimondi haukusaidia na maelfu walichinjwa pale huku Albertoni akikamatwa.
Brigedi ya mwisho kuleta msaada, chini ya Dabormida ilikuwa njiani kuja adowa ila majeshi ya kabila la Oromo chini ya Ras Mikael walimzunguka pande zote na kutoa amri wazungu wote wachinjwe kwa upanga na wote akiwemo Dabormida walikatwa vichwa!!!
Kufikia saa 6 mchana vikosi vyote vya Italia kikiwemo cha baratieri kule Mlima bellah vilisambaratishwa na wengi kujisalimisha kiufupi ndio vita iliishia hapa kwa kipigo kikali kwa wazungu.
MAFANIKIO
Tukiachana na vita ya Adowa pia Menelik I alijenga treni ya kisasa kutoka Ethiopia hadi Eritrea, Pia mfumo wa benki ulianza kwenye utawala wake bila kusahau umeme,magari na mfumo wa simu za mawasiliano yote haya Ethiopia walikuwa nayo kipindi bado nchi karibu zote za Afrika tulikuwa tupo gizani tukiuzwa utumwani!!!
UTUMWA
Menelik II hakupendezwa na biashara ya utumwa na katika wakati wake alikuwa akikushika unafanya biashara hii ya utumwa adhabu ilikuwa kukatwa mikono na chuki hii ya biashara ya utumwa ndio ilimchochea zaidi kuchukia ukoloni wa wazungu hapa Afrika akiwa tofauti na watawala wengine wakafrika walioona sawa kuuza waafrika wenzao utumwani.
HITIMISHO
Kupitia mfalme Menelik I Afrika tunapata fundisho kwamba maendeleo hayaletwi na mkoloni tu au misaada ya wazungu ndio maana Menelik II licha ya kuwakataa wakoloni ila bado aliweza kulinda uhuru wa nchi yake na kuwapa maendeleo ya kisasa bila kusubiri mzungu alete misaada na mikopo ya kinafiki, hili liwe somo kwa viongozi wa kiafrika kwamba tukiamua Afrika tunaweza kuwa bara la kuogopeka na lenye ushawishi kama alivyokua Menelik II hadi kupelekea nchi za wazungu kujaza balozi zao pale
Naomba kuwasilisha

Last edited: