Menelik II: Mtawala wa kiafrika aliyekomesha ukoloni wa wazungu

Menelik II: Mtawala wa kiafrika aliyekomesha ukoloni wa wazungu

Habari za asbuhi wana jukwaa moja kwa moja niende kwenye mada husika.

UTANGULIZI
Mfalme menelik II a.k.a Dagmawi sahle maryam menelik alikuwa mtawala wa Ethiopia kati ya 1889 hadi 1913 ambapo alianza kama mtawala wa eneo la shewa kuanzia 1866-1889. Alizaliwa mwaka 1884 na kufariki mwaka 1913 na inaelezwa alitoka kizazi cha uzao wa Queen of sheba (Makeda) na Mfalme suleiman. Menelik II alikuwa na uwezo wa kuongea lugha 7 ikiwemo kiingereza,kifaransa na kiitalia pia inaelezwa alikuwa msomi wa masuala ya usimamizi wa fedha(Finance) na ndio maana aliweza kuwekeza kwenye hati fungani huko marekani na kuwekeza kwenye migodi ya wabelgiji. Pia katika utawala wake alikuwa kwenye ndoa mara 3 ingawa hakuwahi kupata mtoto kwenye ndoa zote tatu lakini alizaa watoto nje ya ndoa na wote walikuwa mabinti.
View attachment 824104

UMAARUFU WAKE
Mfalme Menelik I anakumbukwa zaidi kwa kupambana na ukoloni wa kizungu katika nchi yake ambapo toka ashike madaraka mpaka anaondoka wazungu walishindwa kabisa kuitawala Ethiopia maana kila wakijaribu walikutana na nchi yenye dola kamili na kujitambua hta wakashindwa kujipenyeza na walipojaribu kuvamia walikutana na kipigo kikali. Pia menelik II anakumbukwa kwa kuitanua ethiopia hata kufikia mipaka kama iliokuwa nayo ufalme wa kush wa zamani uliofahamika kama Axum/Aksum.

VITA YA ADOWA
Kati ya mambo makubwa anayokumbukwa Menelik II ni vita ya Adowa ambapo Italia ilipokuwa amekuja Afrika kuchukua makoloni baada ya mikutano ya Berlin aliiteka somalia na Eritrea na hivyo alitaka na kuiteka Ethiopia ili kupanua utawala wake Afrika.

Italia ikaandaa Jeshi la watu 18,000 viliojipanga kwa brigedi 3 huku Ethiopia ikiwa na wanajeshi wenye uweledi,mafunzo na nidhamu zaidi ya 70,000 na viliongezeka hadi 120,000 vikiongozwa na ma Ras mbalimbali akiwemo mwanamama shujaa Taytu Betul ambaye aliongoza vikosi vya kutoka kaskazini akisaidiwa na kina Ras Makonnen na wengineo.

Usiku wa February 29 1896 vikosi vya Italia viliingia ndani ya Ethiopia katika eneo la Adowa hivyo waethiopia walipopata taarifa wakawazingira milimani wakiwasubiri kuwapa kipigo cha mbwa koko!!!
View attachment 824133

Brigedi ya Albretone kilikuwa cha kwanza kushambulia ila kilikutana na mizinga ya kutoka urusi iliotumiwa na jeshi la Ethiopia iliowadhoofisha sana na hata msaada ulipotoka kwa brigedi zingine za Italia chini ya Arimondi haukusaidia na maelfu walichinjwa pale huku Albertoni akikamatwa.

Brigedi ya mwisho kuleta msaada, chini ya Dabormida ilikuwa njiani kuja adowa ila majeshi ya kabila la Oromo chini ya Ras Mikael walimzunguka pande zote na kutoa amri wazungu wote wachinjwe kwa upanga na wote akiwemo Dabormida walikatwa vichwa!!!

Kufikia saa 6 mchana vikosi vyote vya Italia kikiwemo cha baratieri kule Mlima bellah vilisambaratishwa na wengi kujisalimisha kiufupi ndio vita iliishia hapa kwa kipigo kikali kwa wazungu.

MAFANIKIO
Tukiachana na vita ya Adowa pia Menelik I alijenga treni ya kisasa kutoka Ethiopia hadi Eritrea, Pia mfumo wa benki ulianza kwenye utawala wake bila kusahau umeme,magari na mfumo wa simu za mawasiliano yote haya Ethiopia walikuwa nayo kipindi bado nchi karibu zote za Afrika tulikuwa tupo gizani tukiuzwa utumwani!!!

UTUMWA
Menelik II hakupendezwa na biashara ya utumwa na katika wakati wake alikuwa akikushika unafanya biashara hii ya utumwa adhabu ilikuwa kukatwa mikono na chuki hii ya biashara ya utumwa ndio ilimchochea zaidi kuchukia ukoloni wa wazungu hapa Afrika akiwa tofauti na watawala wengine wakafrika walioona sawa kuuza waafrika wenzao utumwani.

HITIMISHO
Kupitia mfalme Menelik I Afrika tunapata fundisho kwamba maendeleo hayaletwi na mkoloni tu au misaada ya wazungu ndio maana Menelik I licha ya kuwakataa wakoloni ila bado aliweza kulinda uhuru wa nchi yake na kuwapa maendeleo ya kisasa bila kusubiri mzungu alete misaada na mikopo ya kinafiki, hili liwe somo kwa viongozi wa kiafrika kwamba tukiamua Afrika tunaweza kuwa bara la kuogopeka na lenye ushawishi kama alivyokua Menelik I hadi kupelekea nchi za wazungu kujaza balozi zao pale

Naomba kuwasilisha
View attachment 824131
Menelik II a.k.a Dagmawi

hawa mashujaa wa kiafrica ndio walitakiwa wawe topic kwenye historia zetu, kama waliweza kukuza nchi bila ya wazungu ni dhahiri kabisa hata sasa uwezekano upo japo tumechelewa.

chief samahani niulize swali....huyu jamaa alikua na mtangulizi wake ambaye aliitwa "Menelik I" au hayo ni majina tu?!
 
Italy mbona walikuwa na jeshi dhaifu tu hao hata Kinjeketile Ngwale angewapiga.

Ethiopia ashukuru Mungu aiseee angekutana na wajukuu wa Adolf Hitler mbona huyo Menelik kichwa chake kingekuwa makumbusho ya Munich sahivi.

Mjerumani mkatili sana
unaweza kuwa katili lkn hauna mbinu/akili za kivita hivyo unaweza ukapigwa kirahisi na ukatili wako.
 
Kama ilikuwepo basi kwa jina jingine ila unaposema RAS TAFARI ni jina la kuzaliwa la Mtawala Haille Selassie ni sawa na CCM na TANU kwamba huenda kulikuwa na imani ya kama hyo lakini haikuitwa Ras Tafari sababu Ras Tafari imeanza kuitwa hilo jina miaka ya 1940 baada ya Haille Selassie kupambana na waitalia chini ya Benito Mussolini kwenye vita kuu ya pili ya dunia

Ngoja nimuite nyabhingi atupe nondo zaidi
Watalaam wanasema Imani ya Rasta imeanzia pale Babeli chini ya mfalme Nimrod (Wanasema alikua black).
 
Menelik II a.k.a Dagmawi

hawa mashujaa wa kiafrica ndio walitakiwa wawe topic kwenye historia zetu, kama waliweza kukuza nchi bila ya wazungu ni dhahiri kabisa hata sasa uwezekano upo japo tumechelewa.

chief samahani niulize swali....huyu jamaa alikua na mtangulizi wake ambaye aliitwa "Menelik I" au hayo ni majina tu?!
mfano wa nilichokuuliza ni hiki chief...
haya majina ya I, II, III na kuendelea mara nyingi ni huanzia kwa babu baba alafu mjukuu...

na kila mmoja anakua na utata/uwezo wake uliomfanya aache historia.
 
Yes kulikuwepo na Emperor Menelik I ila alitawala kati ya miaka 950 BC zamani sana na hyu mwingine alijiita Menelik II sababu naye pia anadai alikuwa ni mzao wa upande wa kiume kama ilivyokuwa menelik I kutoka queen of sheba na solomon.
 
Mkuu Menelik I ndio alimtangulia menelik II japo wamepishana miaka mingi mingi sana, historia inasema alikua ni mtoto wa Queen Shebba na King solomon. Alitawala 950 BC anakumbukwa zaidi kwa kuipeleka Sanduku la Agano Ethiopia.
 
mfano wa nilichokuuliza ni hiki chief...
haya majina ya I, II, III na kuendelea mara nyingi ni huanzia kwa babu baba alafu mjukuu...

na kila mmoja anakua na utata/uwezo wake uliomfanya aache historia.
.
20180801_113816.jpg
 
Yes kulikuwepo na Emperor Menelik I ila alitawala kati ya miaka 950 BC zamani sana na hyu mwingine alijiita Menelik II sababu naye pia anadai alikuwa ni mzao wa upande wa kiume kama ilivyokuwa menelik I kutoka queen of sheba na solomon.
asante chief!

hivi kumbe queen of sheba alizaa na solomon?
 
Mfalme menelik II a.k.a Dagmawi sahle maryam menelik alikuwa mtawala wa Ethiopia kati ya 1889 hadi 1913 ambapo alianza kama mtawala wa eneo la shewa kuanzia 1866-1889. Alizaliwa mwaka 1884 na kufariki mwaka 1913 na inaelezwa alitoka kizazi cha uzao wa Queen of sheba (Makeda) na Mfalme suleiman.

hapo kwenye mwaka wa kuzaliwa mkuu weka kumbukumbu vizuri alizaliwa1884 hapo hapo ambapo alianza kama mtawala wa eneo la shewa kuanzia 1866-1889
 
Hahaa eti kipigo cha mbwa koko daah

Hizo hati fungani zake mpaka sasa vipi?
Nchi karibu zote zinafanya hii mambo sema kwa kipindi hicho mambo ya finance hayakuwa yamejulikana sana hapa duniani ila wajanja wachache kama kina menelik II ndio walikuwa wanafanya hizo mambo enzi hizo maeneo mengine bado yalikuwa yanafanya barter trade yaani mnabadilishana kiroba kimoja cha mahindi kwa ajili ya kupewa maharage!!! Hivyo kwa enzi hizo kufanya haya mambo ya hati fungani ilikuwa dili sana na kuonyesha jinsi alivyokuwa exposed na masuala ya kiuchumi
 
Last edited:
Mkuu Menelik I ndio alimtangulia menelik II japo wamepishana miaka mingi mingi sana, historia inasema alikua ni mtoto wa Queen Shebba na King solomon. Alitawala 950 BC anakumbukwa zaidi kwa kuipeleka Sanduku la Agano Ethiopia.
asante chief!

kwahiyo inawezekana Menelik II akawa ni mjukuu au mtoto wa Menelik I.
 
asante chief!

hivi kumbe queen of sheba alizaa na solomon?
Yes walizaa naye hata kuna mazalia yapo Ethiopia na baada ya vipimo vya DNA kufanyika ikakubalika kuwa nao ni moja ya makabila yaliyopotea ya kutoka Israel.... Inaaminiwa walikuja huku Afrika baada ya interaction ya kimapenzi ya solomon na makeda/sheba
 
Mfalme menelik II a.k.a Dagmawi sahle maryam menelik alikuwa mtawala wa Ethiopia kati ya 1889 hadi 1913 ambapo alianza kama mtawala wa eneo la shewa kuanzia 1866-1889. Alizaliwa mwaka 1884 na kufariki mwaka 1913 na inaelezwa alitoka kizazi cha uzao wa Queen of sheba (Makeda) na Mfalme suleiman.

hapo kwenye mwaka wa kuzaliwa mkuu weka kumbukumbu vizuri alizaliwa1884 hapo hapo ambapo alianza kama mtawala wa eneo la shewa kuanzia 1866-1889
Ahsante mkuu kwa kunisahihisha hapo ni 1844 sio 1884 ngoja niedit
 
asante chief!

kwahiyo inawezekana Menelik II akawa ni mjukuu au mtoto wa Menelik I.
Ni bloodline tu ya Menelik I lakini jina la Menelik II ilikua AKA tu aliyoitwa jina lake ni Sahle huku baba yake akiwa mfalme Haile Malakot. Menelik I na II wamepishana miaka kalibia 2000
 
Wapigane tena sa hivi ... Tuone nan mshind
Hahahaha walipigana tena vita kuu ya pili ya dunia..... Italia alishinda ile ya 1935 ila 1942 kina haille selassie wakishirikiana na waingereza walimtandika muitalia na kumfukuza Afrika.
 
Back
Top Bottom